Serikali yaichukua rasmi kampuni ya reli (TRL) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaichukua rasmi kampuni ya reli (TRL)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  KUNUNUA HISA ZA RITES, KUITAFUTIA MBIA MWINGINE
  Waandishi Wetu

  SERIKALI itachukua hisa zake kutoka kwa mbia wake kwenye kampuni ya TRL, kwa lengo la kuzinunua hisa 51 za RITES katika kampuni hiyo ili kuinusuru kampuni hiyo iliyogubikwa na migogoro mingi.

  Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Baraza la mawaziri ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza la mawaziri, serikali imeamua kuzichukua hisa hizo ili kuiokoa kampuni hiyo ambayo ni muhimu kwa uchumi wa nchi.

  "Baraza la Mawaziri leo, (jana), katika kikao chake kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam, chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, limejadili hali ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kufanya maamuzi ya msingi kwa kukubaliana kama ifuatavyo maamuzi makuu mawili ya msingi,"alieleza Luhanjo.

  Taarifa hiyo ya serikali imesema uamuzi wa kwanza wa msingi ni kwamba serikali ianze mara moja kujadiliana na RITES, mbia wa Serikali katika kampuni ya TRL, kwa lengo la Serikali kununua hisa 51 za RITES katika kampuni hiyo.

  Uamuzi mwingine ni kwamba baada ya hapo, serikali ifanye matayarisho ya msingi ikiwa ni pamoja na kurekebisha kasoro na kuangalia mustakabali wa TRL, na kuiandaa kampuni hiyo kwa ajili ya kutafutiwa mbia mwingine wa kushirikiana na serikali katika kuendesha TRL.

  Maamuzi hayo yanachukuliwa takribani siku tano baada ya Rais Kikwete kusema hatma ya shirika hilo kongwe ingejulikana juzi.

  Kikwete alisema hayo mkoani Tabora alipokuwa akihutubia mamia ya watu wa kada tofauti kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi katika kilele cha maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani.

  Shirika hilo limekumbwa na matatizo makubwa ya kiundeshaji tangu serikali iingie ubia na kampuni ya Rites ya India na wafanyakazi wameonekana kutoikubali menejimenti mpya ambayo imekuwa ikishindwa kulipa mishahara kwa wakati, hali ambayo imekuza migogoro kutokana na kuwepo kwa migomo ya mara kwa mara.

  Mbali na matatizo hayo ya kiundeshaji, shirika hilo lilikumbwa na matatizo zaidi baada ya kulazimika kusimamisha safari zake kutokana na mafuriko yaliyotokea katika mikoa ya Morogoro na Dodoma kuharibu miundombinu ya reli.

  Hali ya shirika hilo limekuwa mjadala wa wadau mbalimbali lakini halikuweza kujadiliwa kwenye Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kutokana na kile kilichoelezwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa taarifa zake zilikuwa hazijaiva na sasa litawasilishwa na kujadiliwa katika Mkutano wa 19 wa Bunge uliopangwa kufanyika Aprili.

  Serikali ilisaini mkataba wa miaka 25 na Rites Oktoba 2007 ikiwa na matumaini mengi ya kuboresha huduma za usafiri wa reli ambao umekuwa muhimu kwa maisha ya wananchi waishio mikoa ya kati na Kanda ya Ziwa pamoja na uchumi wa taifa.

  Kuzorota kwa shirika hilo kumeongeza ugumu wa maisha kwa wananchi wa maeneo hayo kutokana na bidhaa mbalimbali, yakiwemo mafuta kupanda bei huku taifa likipoteza mabilioni ya fedha yatokanayo na usafirishaji wa mizigo kwenda mikoa hiyo na nchi jirani.

  TRL ni shirika linaloendeshwa kwa ubia baina ya serikali, inayomiliki asilimia 49 ya hisa, na kampuni ya Rites ya India inayomiliki asilimia 51.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18495
   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Kwani hao waliolitoa hilo shirika kwa wahindi ni nani?nafikiri na umbumbumbu wangu baraza la mawaziri chini ya mkulu ndio liloridhia hilo shirika wapewe wahindi,watu walipega kelele toka mwanzo lakini wakubwa wakaweka pamba masikioni,je hiyo hasara mtaifidia vipi kama si kuwaumiza tu wananchi ,ah yaani jamani wakubwa hiyo ten pasenti inapeleka pabaya nchi yetu,hii ni nchi yetu sote na sio nyie wakubwa na familia zenu na wapambe wenu,mnatakiwa muwe na soni!
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Utawala wa kubahatisha bahatisha. These people can't shoot straight. They should have done a due diligence study first. Na makubaliano yajadiliwe na Bunge kabla ya kuwekeana mkataba.

  Who can have confidence in this kind of government? Na wanataka wapewe kipindi kingine tena! Hawana soni?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Miye naomba serikali inipe mwezi tu niandame my own "TRL Rescue Plan".. ambayo haitamhusisha mwekezaji wa nje halatu tulinganishe na plan yao; itakayoungwa mkono zaidi na Watanzania ndiyo ifuatwe!. I"m serious. Nitamtafuta Kawambwa kama atakubali kunisikiliza.. we can't let these people sell even the little things we have!
   
 5. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Nchi za Afrika na nyingine duniani zinazopiga hatua za kwenda mbele kwenye maendeleo, zimebaini jambo hilo, kwa vumbi kutimka, au kwa watu kuzungumza.

  Nchi zote ambazo nchi huonekana ni mali ya watu fulani wachache, ni vigumu kuwa na maendeleo.
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tutafika December 2010 plan ya serikali itakuwa haijatoka......
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  This was supposed to be done 18 months a go, sasa walisubiri hadi watu wateseke namna hii ndio wawatoe hawa wahindi? Hivi mtu akisema huyu mhindi ndiye alileta Mahindra 4x4 mkatumia kwenye uchaguzi 2005 mtabisha?

  Contract gani isiyo na exit clause? nani alisign contract hiyo kwa niaba taifa kutuweka kwenye shida kiasi hiki?

  Hivi CCM kipi mtajivunia mmekifanya kwenye miaka hata hii 5?, inapofikia wananchi kuhoji hata strenght zenu hili ni tatizo kubwa. Na mbaya zaidi hamna utamaduni wa kukosoana, mwanachama wenu yeyote akinyenyua mdomo tu kusema kitu mnamkata ngebe (mnammaliza), hiki chama mmeshakiua wenyewe kifupi haifai kuongoza dola. Mtashinda chaguzi just because majority of Tanzanians are still ignorance na hiyo ndiyo only advantage mliyonayo.
  .
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sidhani kaa kuna jambo la kushangilia hapa. Maana wanataka kumtoa mhindi wa RITES wamtafute 'mlaji' mwingine..kaz kwelkwel. Hizo hisa probably zitauzwa kwa hasara, na atatafutwa 'mwekezaji' mwingine na mambo yatakua yaleyale. Corruption cycle.
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  MM, watanzania wengi tu wangeweza kusaidia hili kama serikali kupitia wizara yake ingetoa nafasi, ushishangae hata wewe ukajibiwa kwamba hilo ni suala la wizara na litafanyiwa kazi ya Tume husika.

  Tume ambayo itatumia pesa ya mlipa kodi maskini.....
   
 10. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #10
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tataendelea mpaka lini tulitoa ATC kwa Africa kusini tukairudisha,Tukawapa Richmund Tukairudisha shirikala simu,kiwira n.k na mengi kuyataja ni gharama gani tunazitumia ktk michezo hiyo ni bora ktk kuyarejesha makampuni ziaandamane na kuchukuliwa hatua kwa walioshiriki ktk kupitisha maazimio hayo vinginevyo tutakua tuanashiriki ktk mduahara usio isha na kuwapa nafasi wakina JK na washiriki wake kupata mwanya wa kutuibia INATOSHA INATOSHA !
   
 11. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Advocate Jasha!
  You are absolutely right hawa Cabinet wamekaa mkao wa kula. Kwa sababu walijua watapitisha sheria hovyo ya kubana wapinzani na shirika alipewa Rostam Aziz na washirika wenzake wametaka Serikali iwalipe hao RITES hewa pesa ili wakafanyie uchaguzi. Just imagine kama mahakama hazijatengewa enough money kwenye bajeti tegemezi hizo pesa za kumlipa huyo Banyani feki? JK na Genge lake la mawaziri uchwara watazitoa wapi hizo ngawira za kuwalipa. Watz hivi hamchoki kudanganywa na hiki chama hiki hovyo. Why don't we forget about democracy and test other means. Rwanda walikuwa na genocide they learned it the hard way na leo hii hakuna longo longo and are forging ahead. Kenya with their 2007 disturbance bajeti yao sio tegemezi why tusichague mojawapo of course sio nzuri. Ila likija la kutokea hell will turn us updown ni bora tukachagua moja. Definately I hate both ,ila Jakaya unatupeleka wapi!!!! Humwogopi Mungu na wala pombe hunyu au kuna kitu umatumia kinakupatia nishai mabya!!! Mkapa alikuwa mlevi wa whisky perhaps ilimtoa kwenye track ila wewe nabakia mdomo wazi!!!!!
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Serikali yaichukua rasmi... = Serikali itachukua... ?
   
 13. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huwa najiuliza sana ni lini serikali hii itajifunza kutokana na makosa yake, au "wao" hawaamini katika msemo huu! CCM ni sawa na wale nguruwe wa riwaya ya shamba la wanyama, wanafikiri wao ndio suluhu ya matatizo yetu, wanafikiri wao ndio thinking tank ya nchi hii, na sisi sote hatuwezi fikiri juu ya fate ya nchui yetu! nafikiri it is a high time now to act, because if we need to act the time is now because there is no time like today!
   
 14. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2010
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  All the so called leaders who were involved in this scum should be "Court Martial". They deserve nothing less. They have done more harm than good to this country. I am tired of this non-sense day-in day-out.
   
 15. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Huu ni mfano wakureward failure. Hizo fedha za kununua hisa watatoa wapi? Na bei ya manunuzi itakuwaje? Balance sheet ya kampuni hii ikoje? Bei ya manunuzi ni lazima iakisi mwenendo mzima wa vitabu vya akaunti vya TRL. Unajua inawezekana kampuni ilikuwa inaelekea kufilisika in which case a court appointed administrator angeingia na kuweka mambo sawa kabla ya umiliki kubadilisha mikono. Wakijaga administrators kampuni hununuliwa karibia na bure
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  TRL ina mchango mkubwa sana kuliko ATCL.they should rush to privatise ATCL 100%.
  TRL should be totally owned bu the Gov
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tatizo ni kuwa walioiingiza serikali kwenye mkenge huu wala hawatachukuliwa hatua zozote
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Nadhani hili shirika lina matatizo ambayo pia yanachangiwa zaidi na upande wa serikali

  -Ni kwa nini wasielekeze resources za NSSF huko na asilimia chache wawape wabia ili ku-harmonise welfare na profit making strategy?
   
 19. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Na huu ndio ukweli, lile shirika halikuuwawa na RITEs, limeuwawa na Serikali.

  1. Kutochangia hisa zake on time.
  2. Kutoandaa wafanyakazi wa shirika kwamba litaendeshwa kibepari.
  3. Kukubali too much interference ya Trade Unions.
  4. Kuliendesha kisiasa, as shareholder huwezi kuwasiliana na wafanyakazi wewe mwenyewe wakati mwenzako hayuko... ni majungu.... unacceptable in business world.
   
 20. K

  Kachero JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa za uhakika hao RITES hizo hisa 51 hawakulipa chochote,badala yake wakatumia rasilimali za TRL kwenda kuomba mkopo wa Dola Mil 100 toka World Bank ili kuendesha TRL.Sasa kwa umbumbumbu wa Serikali yetu watataka kujadiliana nao ili eti wazinunue hizo hisa asilimia 51 za RITES.

  Majadiliano ya nini wakati RITES hajaweka chochote zaidi ya kukopa World Bank.Rasilimali ni za Tanzania,TRL ni ya Tanzania mkopo ni wa kampuni ya Tanzania.RITES waanze tuu watuachie TRL yetu na hatutaki wawekezaji toka nje hisa wauziwe watanzania wenyewe wenye uchungu na nchi yao.
   
Loading...