Serikali yaiagiza TCRA kuchunguza madai ya Wizi wa Fedha za Wateja wa Simu

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,310
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Nchini, TCRA kuchunguza madai ya muda mrefu ya watumiaji wa simu za mikononi kuibiwa muda wa maongezi na fedha za mitandaoni.

Wizi huo unadaiwa kufanywa na mitandao ya wizi ikishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hizo za simu.

Chanzo: Radio One
 
yaani mpaka sasa wameshaatufilisi ndo wanakuja huku mim voda nilitupa chip yao baada ya kuniibia
 
Nilifunga biashara yangu kwa hii michezo, hadi leo huwa siamini number zangu za simu maana mtu anaweza kuchezea atakavyo.
 
Serikali inatakiwa kuwasadia wananchi kwani huu wizi ni wa kiteknologia kiasi kwamba mwananchi wa kawaidi hawezi hata siku moja ni jambo gani linaendelea.
Ukweli ni kuwa wizi ni mkubwa sana. Mbaya hzaidi hazilipiwi Kodi. Hivyo ni mwananchi anaibiwa lakini pia serikali huibiwa.
 
Hakuna mtandao unaongoza kwa kuibia wateja wake wale mawakala kama tigo.na tena wanaofanya wizi huo ni hao watumishi wa tigo wanaoitwa superdealers,haiwezekani mtu ambae sio mfanyakazi wa tigo ajue ukipiga namba furani na furani pesa inahama kwenye simu ya wakala.
 
Kama Vodacom wanaiba kuliko kampeni zote za mitandao yote Tanzania
 
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Nchini, TCRA kuchunguza madai ya muda mrefu ya watumiaji wa simu za mikononi kuibiwa muda wa maongezi na fedha za mitandaoni.

Wizi huo unadaiwa kufanywa na mitandao ya wizi ikishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hizo za simu.

Chanzo: Radio One

kwani kazi ya tcra ni nini kama kila kitu mpaka serikali iwaagize?bora ivunjwe iundwe mpya,mijitu imeanza kuiba kitambo tcra wapo tu kama makuu
 
Kiukweli mitandao inaiba sana unanua kifirushi kina dakika 80 ukitumia hata dakika hamsini hazifiki wanakwambia Salio lako limeisha na huna wa kumuuliza wala sehemu ya kwenda kushitaki.
Hakika hata hivi vifurushi vichunguzwe ni vidogo kwa gharama kubwa hata hicho kidogo tubaibiwa havikamiliki.
Hii ni ajabu.
 
Nina hasira na voda
Walimpa mtu mwingine namba yangu hadi leo sielewi hela zangu zilizokuwa M-pawa nazipataje
 
Inamaana kwamba huyo msemaji wa serikali yeye hatumii hii mitandao iliopo Tanzania na kubaini yalalamikiwayo, Only in Tz.
 
Hawawezi kwani hayo malalamiko ni kitambo hakuna alionyesha kulishughulikia. Pili watajikagua wenyewe maana kuna tetesi kuwa haya makampuni ya mobile phones wakubwa wana hisa humo.
 
Suluhisho recharge card zionyeshe expected airtime (voda to voda/voda to airtel etc)in minutes na siyo gharama ya kadi tu.
 
mlolongo wa kufatilia ni mkubwa sana ukienda kulalamika tcra wanakwambia rudi kwa mwizi wako aliyekuibia namaanisha mtandao unaoutuhumu hivi tangu lii mwizi akakubali yeye ameiba
 
tcra ni wazembe wakubwa,,, haya makampuni ya simu yameanza wizi mudac mrefu wako kimya, sasa hivi ndio wanajifanya kushtuka
 
Naomba msada kwa Tcra. Mimi nililipia maji kwa AIRTEL money, lakini fedha hiyo haikufika katika mamlaka husika ikabidi nilipe Mara ya pili kupitia mtandao mwingine. Niljaribu kudai fedha hizo lakini sikurudishiwa wala sikupata ushirikiano kutoka airtel. Naomba msaada was Mimi kupata haki yangu na inawezekana kuna waathirika wengi waliopata tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom