Serikali yaguswa na siku 100 alizopewa Kikwete

Status
Not open for further replies.

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Akizungumzia waraka uliosambazwa wa kumpa Rais Jakaya Kikwete siku 100 awe ameachia madaraka, waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha amesema wanaufanyia kazi ili kuwabaini waliohusika kuuandaa, kwa kuwa unaashiria uvunjifu wa amani.

“Kauli kama hizi ni jambo ambalo halikubaliki na tunaendelea kulifanyia kazi na kukusanya taarifa za siri ili tuweze kuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria” alisema.

::HabariLeo::
 
Amani ipo mikononi mwetu. Nawasihi tuitunze kwa nguvu zote.

Yeyote anayehatarisha AMANI ya nchi yetunaswa kumpinga kwa nguvu zote.
 
Amani ipo mikononi mwetu. Nawasihi tuitunze kwa nguvu zote.

Yeyote anayehatarisha AMANI ya nchi yetunaswa kumpinga kwa nguvu zote.

ndio ipo mikononi mwetu ila sasa watakao anza kuivunja ni ccm wako hao kwa kutosikiliza kilio cha wananchi na maamuzi yao hasa issue ya katiba.
 
Amani ipo mikononi mwetu. Nawasihi tuitunze kwa nguvu zote.

Yeyote anayehatarisha AMANI ya nchi yetunaswa kumpinga kwa nguvu zote.

Amani siku zote huwa inaendana na haki, serikali isikilize wananchi.
 
Ni kweli yale maandiko ni ya kutisha na ninaomba serikali tawala ilifanyie kazi suala hili haraka bila kusita. Wahuni wanampa raisi wa nchi siku 100 za kuachia madaraka na kuondoka nchini?. Uhuru wa habari usivuke mipaka.
 
Du hii sasa kali! Ukiona Moshi unafuka mahali mmmmmm usijiamini kupita kiasi lazima uchunguze kunani nimesoma mpaka nimechoka! But something is wrong somewhere ndani ya system ya mkulu wetu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom