Serikali yagusia kinachoendelea kati ya Tanzania na Malawi

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,315
2,000

Serikali ya Tanzania imesema itafanya uchunguzi kuhusu habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Malawi vinavyodai majasusi wanane wa Tanzania wametiwa mbaroni wakifanya ujasusi katika mgodi mmoja wa urani katika nchi hiyo.Gazeti la kila siku la The Citizen la hapa nchini limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, taarifa za kutiwa mbaroni watu hao ziliripotiwa kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi na vyombo vya habari vya Malawi vikadai kuwa, majasusi wanane wametumwa na serikali ya Tanzania kwenda kuchunguza iwapo Malawi inaunda silaha za nyuklia kwa kutumia urani kwenye mgodi wa Kayerekera uliopo Wilayani Karonga ama la.

Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga ameliambia gazeti la The Citizen kuwa hana habari kuhusu ripoti hizo na kuahidi kufuatilia.“Ndio kwanza nasikia habari hii kutoka kwako. Haya ni madai mazito. Nitafuatilia jioni hii. Nitawasiliana na ubalozi wetu Malawi na maafisa wetu wa intelijensia kujua zaidi kuhusu madai hayo. Haya ni madai mazito sana,” amesema Dk. Mahiga.

Vyombo vya habari vya Malawi vimezinukuu duru za usalama bila ya kutaja majina zikisema kuwa, baadhi ya Watanzania hao wamekamatwa na vifaa vinavyotia wasiwasi zikiwemo kamera zenye uwezo mkubwa wa kupiga picha.

=======

Tanzania investigates Malawi ‘spies’ reports

Dar es Salaam. The government says it will investigate claims reported by the Malawian media yesterday that eight alleged spies from Tanzania were arrested while trying to illegally enter a uranium mine in the neighbouring country.

Reports of the arrests were first published last Thursday, and the Malawian media yesterday suggested that the eight were spies sent by the Tanzanian government to investigate if the country “is developing nuclear weapons from uranium at Kayerekera mine site in Karonga District”.

The group also allegedly entered Malawi without travel documents, according to reports posted on the nyasatimes.com, blantyrepost.com and maravipost.com websites.

The Minister of Foreign Affairs and East African and International Cooperation, Dr Augustine Mahiga, told The Citizen yesterday that he was unaware of the reports and promised to make a follow-up.

“I’m hearing this the first time from you. These are serious allegations. I will make a follow-up this evening. I will get in touch with our embassy there and our intelligence people to see if they know anything about this...these are very serious allegations,” said Dr Mahiga.

The Malawian media quoted anonymous security sources saying some of those arrested had “suspicious” devices, including a “heavy camera”.

“The question is why visit Kayerekera Uranium mine site out of different structures here in the district, and the other thing is that the group are failing to disclose the reason behind their coming. It seems the Tanzanian government thinks that Malawi is preparing something big and it is trying its best to be alert,” said one of the source.

The reports also suggested that “the Tanzanian government is frustrated with Malawi’s position of being unshaken with the issue of Lake Malawi border dispute between the two neighbouring countries.”

But Karonga deputy police spokesperson, Mr George Mlewa, dismissed the border link and uranium allegations allegation when contacted, saying they were treating the suspects as trespassers.

“While our investigation is underway on the matter, I can tell you that we don’t have such information so far...those are just mere rumours,” he said.

Police said villagers at Kayuni village were surprised to see the Tanzanians loitering around the mine.

“When they asked them what they wanted at the mine, they failed to give convincing answers,” said Mr Mlewa.

He said this is when the villagers’ suspicion grew and called the police, who swiftly came and arrested the eight foreigners.

Mr Mlewa said the eight would appear before in court soon to answer charges of criminal trespass, but said the case may change according to evidence that would be obtained through the investigation.

Meanwhile, the suspects were transferred from police custody to Mzuzu prison.

Recently, according to Malawian media reports, a group of university students from Tanzania under the Moravian Church were also blocked from visit the mine site, which is currently closed.

Chanzo: The Citizen
 
Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,170
2,000
Yaana serikali hawajui kama kuna majasusi Malawi?.....

Walitumwa na nani?......

Hapa kilichotakiwa ni kujibu kuna majasusi au hakuna? .....

Kama unachunguza maana yake walitumwa na nani?.......

Serikali ilitakiwa kuja na jibu sio kuchunguza majasusi wake kama wapo uko.........

Haya mambo yanatokea Tanzania pekee bora angekaa kimya......
Ni aibu kusema majasusi wetu wamekamatwa kama kuku wa kisasa.
Jibu amelitoa kidiplonasia zaidi,kuliko angesema ni kweli wapo na walitumwa kwa kazi hiyo.
 
chardams

JF-Expert Member
May 1, 2012
2,415
2,000
Yaana serikali hawajui kama kuna majasusi Malawi?.....

Walitumwa na nani hivi kwa nini usifanye uchunguzi kwanza ndio ukaja kutoa majibu?......

Hapa kilichotakiwa ni kujibu kuna majasusi au hakuna? .....

Serikali ilitakiwa kuja na jibu sio kuchunguza majasusi wake kama wapo uko.........

Haya mambo yanatokea Tanzania pekee bora angekaa kimya......
Huna unachojua kaa kimya. Jasusi akikamatwa nchi nyingine serikali lazima imkane.
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
Yaana serikali hawajui kama kuna majasusi Malawi?.....

Walitumwa na nani hivi kwa nini usifanye uchunguzi kwanza ndio ukaja kutoa majibu?......

Hapa kilichotakiwa ni kujibu kuna majasusi au hakuna? .....

Serikali ilitakiwa kuja na jibu sio kuchunguza majasusi wake kama wapo uko.........

Haya mambo yanatokea Tanzania pekee bora angekaa kimya......
Hapana mkuu technically hapa natofautiana na wewe.

Mambo ya "Ujasusi" kati ya nchi na nchi siyo ya kuyajibu kichwa kichwa tena ktk media.Kama kweli hao ni "watu wetu" na tukisema tuna taarifa nao,basi ndio tunazidisha mgogoro.Kumbuka kuwa hao kama walitumwa,maanake ilikuwa waende bila kujulikana na warudi bila kujulikana...Kama wamekamatwa basi ujue "Mission not accomplished"

Tena kwa nchi nyingine mnawakana kabisa...Kwamba hawa hatuwajui na hawakutumwa kazi hiyo,ndio maana kama ulisoma Nyasa Times,wale jamaa waliokamatwa wanakataa katakata kutumwa na Tanzania.

Tunaweza kutofautiana ktk mambo ya sera,itikadii na namna ya kuendesha serikali zinazoongozwa na vyama vya siasa.Lakini ni lazima tufungamane ktk mambo yanayohusu Ulinzi na Usalama wa Taifa letu.

Wakati sisi tukishinda na kukutana humu tukiisema Serikali na wanasiasa wetu;kuna watu wapo ktk mipaka ya nchi,nchi jirani,nchi kavu na majini wakihakikisha nchi hii inaendelea kuwa shwari na mahali salama pa kuishi.

Tunapofungua makasha ya zawadi za msimu wa Xmass na mwaka mpya,kuna wenzetu ktk mahandaki na mapori ya mipakani mwa nchi zetu wanafungua chupa za maji yasiyo na ladha kupooza makoo yao sbb ya kuhangaika kutwa kucha kuhakikisha adui hapenyi ktk mipaka yetu.Hawa tunatakiwa tuwaheshimu,bila kujali hisia zetu na utofauti wetu wa itikadi za kisiasa...Huu ndio utaifa,na huu ndio Umoja wa kweli wa Kitaifa.

Hujui hao waliokamatwa;Walitaka kuokoa nini kikubwa kilicholenga kuliharibia Taifa letu....Ninayasema haya kwa dhati ya moyo na kwa uzoefu wa Mataifa mengine.Tuwape heshima walinzi wa amani na umoja wa nchi hii.Kuna watu hawafanyi kazi kwa ajili ya CCM au CHADEMA/CUF,bado tuna watu wanaofanya kazi kwa ajili ya TAIFA tu....Ukiwapa "mtihani" wa CCM na CHADEMA Wanapata "Zero"
 
joely

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
1,053
1,250

Wewe unafikiri nchi inaendeshwa kama shamba la mkonge
 
Kutwa

Senior Member
Aug 29, 2016
186
500
Yaana serikali hawajui kama kuna majasusi Malawi?.....

Walitumwa na nani hivi kwa nini usifanye uchunguzi kwanza ndio ukaja kutoa majibu?......

Hapa kilichotakiwa ni kujibu kuna majasusi au hakuna? .....

Serikali ilitakiwa kuja na jibu sio kuchunguza majasusi wake kama wapo uko.........

Haya mambo yanatokea Tanzania pekee bora angekaa kimya......
Hivi huko kwenye data center zenu za vyama huwa mnalipwa kwa post per day au ukubwa wa pumba mnazoandika.
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,582
2,000
Yaana serikali hawajui kama kuna majasusi Malawi?.....

Walitumwa na nani hivi kwa nini usifanye uchunguzi kwanza ndio ukaja kutoa majibu?......

Hapa kilichotakiwa ni kujibu kuna majasusi au hakuna? .....

Serikali ilitakiwa kuja na jibu sio kuchunguza majasusi wake kama wapo uko.........

Haya mambo yanatokea Tanzania pekee bora angekaa kimya......
Hata kama kweli tumetuma unategemea Mahiga aseme ndio tumetuma majasusi.
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
10,856
2,000
Yaana serikali hawajui kama kuna majasusi Malawi?.....

Walitumwa na nani hivi kwa nini usifanye uchunguzi kwanza ndio ukaja kutoa majibu?......

Hapa kilichotakiwa ni kujibu kuna majasusi au hakuna? .....

Serikali ilitakiwa kuja na jibu sio kuchunguza majasusi wake kama wapo uko.........

Haya mambo yanatokea Tanzania pekee bora angekaa kimya......
Mkuu technically, sina sababu ya kukushambulia lakini hebu soma vizuri ujumbe wa barafu kwako. Ukiangalia kwa undani hata sababu iliyotolewa kwamba majasusi wetu wamekwenda kuchunguza kama Malawi wanatengeneza nyuklia haina uzito. Malawi na silaha za nyuklia??? Bado sana. Habari kama hizi tunapozipata wanajamvi ni bora tukakaa kimya kusubiri ama kukombolewa kwa vijana wetu au matokeo ya majadiliano kama itagundulika kweli ni vijana wetu. Kama alivyosema barafu usalama wetu unapaswa kuwa mojawapo kati ya vitu vinavyotuunganisha kama taifa. Vitu vingine ni maafa, vita, michezo na vingine vya aina hiyo ambavyo havihusishi itikadi. Tuwakemee wote wanaoleta itikadi hata kwenye masuala yasiyohtaji itikadi hata kama ni Viongozi wetu. Kama taifa "USALAMA WETU KWANZA".
 
LEWANGANGUMU

JF-Expert Member
Feb 19, 2016
288
250
Hapana mkuu technically hapa natofautiana na wewe.

Mambo ya "Ujasusi" kati ya nchi na nchi siyo ya kuyajibu kichwa kichwa tena ktk media.Kama kweli hao ni "watu wetu" na tukisema tuna taarifa nao,basi ndio tunazidisha mgogoro.Kumbuka kuwa hao kama walitumwa,maanake ilikuwa waende bila kujulikana na warudi bila kujulikana...Kama wamekamatwa basi ujue "Mission not accomplished"

Tena kwa nchi nyingine mnawakana kabisa...Kwamba hawa hatuwajui na hawakutumwa kazi hiyo,ndio maana kama ulisoma Nyasa Times,wale jamaa waliokamatwa wanakataa katakata kutumwa na Tanzania.

Tunaweza kutofautiana ktk mambo ya sera,itikadii na namna ya kuendesha serikali zinazoongozwa na vyama vya siasa.Lakini ni lazima tufungamane ktk mambo yanayohusu Ulinzi na Usalama wa Taifa letu.

Wakati sisi tukishinda na kukutana humu tukiisema Serikali na wanasiasa wetu;kuna watu wapo ktk mipaka ya nchi,nchi jirani,nchi kavu na majini wakihakikisha nchi hii inaendelea kuwa shwari na mahali salama pa kuishi.

Tunapofungua makasha ya zawadi za msimu wa Xmass na mwaka mpya,kuna wenzetu ktk mahandaki na mapori ya mipakani mwa nchi zetu wanafungua chupa za maji yasiyo na ladha kupooza makoo yao sbb ya kuhangaika kutwa kucha kuhakikisha adui hapenyi ktk mipaka yetu.Hawa tunatakiwa tuwaheshimu,bila kujali hisia zetu na utofauti wetu wa itikadi za kisiasa...Huu ndio utaifa,na huu ndio Umoja wa kweli wa Kitaifa.

Hujui hao waliokamatwa;Walitaka kuokoa nini kikubwa kilicholenga kuliharibia Taifa letu....Ninayasema haya kwa dhati ya moyo na kwa uzoefu wa Mataifa mengine.Tuwape heshima walinzi wa amani na umoja wa nchi hii.Kuna watu hawafanyi kazi kwa ajili ya CCM au CHADEMA/CUF,bado tuna watu wanaofanya kazi kwa ajili ya TAIFA tu....Ukiwapa "mtihani" wa CCM na CHADEMA Wanapata "Zero"
nimependaa sana maoni yko na unaonekanaa unaonaa mbali sanaaaa
Wewe ni mtu mmoja lakin ni kama watu million mojaaa
 
Transcend

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
20,171
2,000
Yaana serikali hawajui kama kuna majasusi Malawi?.....

Walitumwa na nani hivi kwa nini usifanye uchunguzi kwanza ndio ukaja kutoa majibu?......

Hapa kilichotakiwa ni kujibu kuna majasusi au hakuna? .....

Serikali ilitakiwa kuja na jibu sio kuchunguza majasusi wake kama wapo uko.........

Haya mambo yanatokea Tanzania pekee bora angekaa kimya......
Mkuu hivi vitu havitaki mtu kukurupuka! Hata kama wanajua hawawezi kuweka open!

vitu vingine sio lazima viitiwe press!
 
Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,875
2,000

Serikali ya Tanzania imesema itafanya uchunguzi kuhusu habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Malawi vinavyodai majasusi wanane wa Tanzania wametiwa mbaroni wakifanya ujasusi katika mgodi mmoja wa urani katika nchi hiyo.Gazeti la kila siku la The Citizen la hapa nchini limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, taarifa za kutiwa mbaroni watu hao ziliripotiwa kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi na vyombo vya habari vya Malawi vikadai kuwa, majasusi wanane wametumwa na serikali ya Tanzania kwenda kuchunguza iwapo Malawi inaunda silaha za nyuklia kwa kutumia urani kwenye mgodi wa Kayerekera uliopo Wilayani Karonga ama la.

Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga ameliambia gazeti la The Citizen kuwa hana habari kuhusu ripoti hizo na kuahidi kufuatilia.“Ndio kwanza nasikia habari hii kutoka kwako. Haya ni madai mazito. Nitafuatilia jioni hii. Nitawasiliana na ubalozi wetu Malawi na maafisa wetu wa intelijensia kujua zaidi kuhusu madai hayo. Haya ni madai mazito sana,” amesema Dk. Mahiga.

Vyombo vya habari vya Malawi vimezinukuu duru za usalama bila ya kutaja majina zikisema kuwa, baadhi ya Watanzania hao wamekamatwa na vifaa vinavyotia wasiwasi zikiwemo kamera zenye uwezo mkubwa wa kupiga picha.

=======

Tanzania investigates Malawi ‘spies’ reports

Dar es Salaam. The government says it will investigate claims reported by the Malawian media yesterday that eight alleged spies from Tanzania were arrested while trying to illegally enter a uranium mine in the neighbouring country.

Reports of the arrests were first published last Thursday, and the Malawian media yesterday suggested that the eight were spies sent by the Tanzanian government to investigate if the country “is developing nuclear weapons from uranium at Kayerekera mine site in Karonga District”.

The group also allegedly entered Malawi without travel documents, according to reports posted on the nyasatimes.com, blantyrepost.com and maravipost.com websites.

The Minister of Foreign Affairs and East African and International Cooperation, Dr Augustine Mahiga, told The Citizen yesterday that he was unaware of the reports and promised to make a follow-up.

“I’m hearing this the first time from you. These are serious allegations. I will make a follow-up this evening. I will get in touch with our embassy there and our intelligence people to see if they know anything about this...these are very serious allegations,” said Dr Mahiga.

The Malawian media quoted anonymous security sources saying some of those arrested had “suspicious” devices, including a “heavy camera”.

“The question is why visit Kayerekera Uranium mine site out of different structures here in the district, and the other thing is that the group are failing to disclose the reason behind their coming. It seems the Tanzanian government thinks that Malawi is preparing something big and it is trying its best to be alert,” said one of the source.

The reports also suggested that “the Tanzanian government is frustrated with Malawi’s position of being unshaken with the issue of Lake Malawi border dispute between the two neighbouring countries.”

But Karonga deputy police spokesperson, Mr George Mlewa, dismissed the border link and uranium allegations allegation when contacted, saying they were treating the suspects as trespassers.

“While our investigation is underway on the matter, I can tell you that we don’t have such information so far...those are just mere rumours,” he said.

Police said villagers at Kayuni village were surprised to see the Tanzanians loitering around the mine.

“When they asked them what they wanted at the mine, they failed to give convincing answers,” said Mr Mlewa.

He said this is when the villagers’ suspicion grew and called the police, who swiftly came and arrested the eight foreigners.

Mr Mlewa said the eight would appear before in court soon to answer charges of criminal trespass, but said the case may change according to evidence that would be obtained through the investigation.

Meanwhile, the suspects were transferred from police custody to Mzuzu prison.

Recently, according to Malawian media reports, a group of university students from Tanzania under the Moravian Church were also blocked from visit the mine site, which is currently closed.

Chanzo: The Citizen
Hivi kwa kutumia akili za kawaida Malawi inaweza kutengeneza silaha ya nuklia hadi Tanzania iwe na wasiwasi?!

Kwa kuwa na mgodi wa uranium, Malawi wanadhani wanaweza kutengeneza hata generator la kuzalisha umeme!!

Mbona Wamalawi wanajidharaurisha kiasi hiki!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom