Serikali yagoma kuwalipa mishahara waajiriwa wapya wa mahakama ya Tanzania

mzee wa giningi

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
519
336
Serikali iliwaajiri watumishi wapya wa mahakama mwaka jana baada ya mda iliwasimamisha kazi wamekaa mwaka mmoja nyumbani wamekuja kuitwa mwezi wa saba mwaka huu kurudi kazini cha lush an chakushangaza serikali imegoma kuwapa pesa za kujikimu na mshahara leo hii wana miezi miwili wapo vituo vya kazi lakini hawana mshahara wala pesa ya kujikimu na kazi wanafanya serikali acheni mateso ya namna hii kama hamtaki kuajiri semeni tu.

Inauma sana aiseee kuwa omba omba huku unafanya kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwe na huruma ww acha siasa kwenye life ya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio dharau huo ni ushauri positive. Unafikiri kupayuka hapa ndio hela itakuja?

Sisi wengine mbona tulikaa miezi 4 bila pesa ila badae tukapewa? Watulie wachape kazi ili umuhimu wao uonekane....pia mbona hawatwambii kama wameishafikisha malalamiko yao kwa wakubwa wao wa Mahakama?
 
Serikali iliwaajiri watumishi wapya wa mahakama mwaka jana baada ya mda iliwasimamisha kazi wamekaa mwaka mmoja nyumbani wamekuja kuitwa mwezi wa saba mwaka huu kurudi kazini cha lush an chakushangaza serikali imegoma kuwapa pesa za kujikimu na mshahara leo hii wana miezi miwili wapo vituo vya kazi lakini hawana mshahara wala pesa ya kujikimu na kazi wanafanya serikali acheni mateso ya namna hii kama hamtaki kuajiri semeni tu.

inauma sana aiseee kuwa omba omba huku unafanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko Tanzania hakuna serikali sasa hivi. Kuna ujambazi uliohalalishwa unaitwa serikali tu.
 
Sio dharau huo ni ushauri positive. Unafikiri kupayuka hapa ndio hela itakuja?

Sisi wengine mbona tulikaa miezi 4 bila pesa ila badae tukapewa? Watulie wachape kazi ili umuhimu wao uonekane....pia mbona hawatwamnii kama wameishafikisha malalamiko yao kwa wakubwa wao wa Mahakama?
Majibu yako ya kisiasa sana political oriented

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu, katika ajira za serikali ikiwa ni ajira ya kwanza ni kawaida kukaa miezi mitatu hadi minne bila kulipwa mshahara. Kuingiza watumishi kwenye pay roll ni hadi mchakato maalumu ufanyike. hata hivyo kuna haki ya kupewa posho au pesa ya kujikimu katika kipindi hicho cha mpito.

Hizi ajira za mahakama zilizositishwa na kurudishwa zimekaa kimaslahi flani. Ajira hizi zilitoka wakati ambao kuna baadhi ya mamlaka hazikuwa tayari au kuridhia kuajiri ajira mpya. Kwa maneno mengine Ajira hizi zilizua mtafaruku kati ya tume ya utumishi wa mahakama na idara zingine.

Kwa ushauri tafuteni haki yenu ya kupewa pesa ya kujikimu, mshahara utaingia tu baada ya kumaliza miezi yenu mitatu. Ukibidi tafuteni wawakilishi na mkaonene ma mtendaji mkuu wa mahakama.
 
Hili lizeee linaharibu nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu kuna watu wanamsifia sana,hawa huwa wanajua anavyoharibu ila wanapata manufaa fulani kumshabikia au niujinga wa kukosa elimu ya msingi ya uraia tu?
Nchi inakuwa kama haina kiongozi ovyo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Raisi hata hahusiki kabisa na suala hili. Hili ni suala linahusu Tume ya utumishi wa mahakama na ofisi ya Mtendaji mkuu wa mahakama. Hata katika awamu zilizopita za serikali hii kitu ilikuwepo.
Mahakama ya Tanzania imejaa ukiritimba na rushwa sana. Watumishi hawapendani na wanafanyana hila wao kwa wao. Kuna makundi na ubaguzi ndani ya mahakama ya tanzania, kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya juu kabisa ni makundi hasimu tu. Poleni zenu mnaoingia huko.
 
Ndugu, katika ajira za serikali ikiwa ni ajira ya kwanza ni kawaida kukaa miezi mitatu hadi minne bila kulipwa mshahara. Kuingiza watumishi kwenye pay roll ni hadi mchakato maalumu ufanyike. hata hivyo kuna haki ya kupewa posho au pesa ya kujikimu katika kipindi hicho cha mpito.

Hizi ajira za mahakama zilizositishwa na kurudishwa zimekaa kimaslahi flani. Ajira hizi zilitoka wakati ambao kuna baadhi ya mamlaka hazikuwa tayari au kuridhia kuajiri ajira mpya. Kwa maneno mengine Ajira hizi zilizua mtafaruku kati ya tume ya utumishi wa mahakama na idara zingine.

Kwa ushauri tafuteni haki yenu ya kupewa pesa ya kujikimu, mshahara utaingia tu baada ya kumaliza miezi yenu mitatu. Ukibidi tafuteni wawakilishi na mkaonene ma mtendaji mkuu wa mahakama.
Ni kawaida sababu ya ujinga. Maendeleo yote haya ya technology why utese watu muda wote huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raisi hata hahusiki kabisa na suala hili. Hili ni suala linahusu Tume ya utumishi wa mahakama na ofisi ya Mtendaji mkuu wa mahakama. Hata katika awamu zilizopita za serikali hii kitu ilikuwepo.
Mahakama ya Tanzania imejaa ukiritimba na rushwa sana. Watumishi hawapendani na wanafanyana hila wao kwa wao. Kuna makundi na ubaguzi ndani ya mahakama ya tanzania, kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya juu kabisa ni makundi hasimu tu. Poleni zenu mnaoingia huko.

Rais anahusika na kila kitu kinachotokea katika serikali ya Tanzania.

Hiyo Tume ya Utumishi mkubwa wake anateuliwa na nani?

Jaji Mkuu anateuliwa na nani?

Waziri wa Sheria anateuliwa na nani?

Bajeti ya Mahakama inatoka wapi?

Ulisikiliza hotuba ya Magufuli alivyohutubia mahakama?

Hayo madudu ya Mahakama za Tanzania Magufuli ana mpango gani kufanya yaishe? Yeye ndiye mkuu wa nchi, Mahakama zikifulia huwezi kusema hahusiki.

Sent from my Kimulimuli
 
Jibu lako limejikita katika siasa zaidi, sio kitaaluma.
 
Back
Top Bottom