Serikali yafyata kwa Dowans

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
24
Serikali yafyata kwa Dowans
• Yajiandaa kula matapishi yake

na Sauli Giliard

BAADA kuikwepa mitambo ya kufua umeme ya Dowans kwa takriban mwaka mmoja, hatimaye serikali iko katika mipango kabambe kuhakikisha inainunua mitambo hiyo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100, Tanzania Daima Jumapili imebaini.

Miongoni mwa mikakati ya kuijengea mazingira mazuri ya kuihalalisha mitambo ya Dowans ni kufutwa kwa zabuni zilizotangazwa na serikali za kununua mitambo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 kwa kituo cha Dar es salaam na megawati 60 kwa kituo cha Mwanza.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata kutoka katika chanzo kimoja kilichoko serikalini ni kwamba mitambo hiyo inaweza kununuliwa katika kipindi cha miezi miwili kutoka hivi sasa.

Chanzo hicho kimebainisha kuwa pamoja na utayari huo wa serikali kutaka kuinunua mitambo hiyo, bado kumekuwapo na kusitasita kulitekeleza jambo hilo kwa hofu ya kushambuliwa kisiasa kama ilivyowahi kutokea huko nyuma.

Mjadala wa kuinunua mitambo hiyo ambayo ilirithi mkataba kutoka katika kampuni ya Richmond, uliwagawa wananchi katika makundi mawili ambapo moja likiunga mkono huku jingine likipinga kwa madai ni kuhalalisha ufisadi.

Rais Jakaya Kikwete naye aliingia katika mjadala huo kwa kuhitimisha kuwa isinunuliwe baada ya kuona upepo wa wale waliokuwa wakipinga ununuaji wake kuwa mkali zaidi.

Badala yake taifa lilipokuwa likikabiliwa na uhaba wa umeme mwaka jana rais aliziagiza Wizara za Nishati na Madini, Katiba na Sheria na ile ya Fedha na Uchumi kuketi pamoja ili kuiwezesha mitambo ya kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kuwashwa pasi na kujali gharama au kesi iliyo mahakamani.

Hata hivyo ilikuja kubainika kuwa gharama za kuihudumia IPTL ni kubwa zaidi kuliko ile ya kuinunua mitambo ya Dowans ambayo mpaka sasa inaendelea kukaa katika eneo linalomilikiwa na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) eneo la Ubungo, jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, ripoti ya Kamati ya Bunge inayoshughulikia Fedha na Uchumi ilitoa mchanganuo wake wa mzigo unaobebwa na serikali kutokana na mitambo ya IPTL kwamba unaweza kuongezeka na kufikia sh bilioni 60 kwa mwezi kiasi ambacho ni mara kumi zaidi iwapo ingetumika ile ya Dowans.

Dalili za kuitumia tena mitambo ya Dowans zilianza kuonekana mwishoni mwa mwaka jana pale ilipotokea mgao mkubwa wa umeme na Kamati ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo (CCM), pamoja serikali kukubali Dowans iuze umeme TANESCO lakini si kununuliwa.

Wazo kama hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Adam Malima, aliyeweka wazi kuwa endapo mtu atainunua mitambo hiyo serikali iko radhi kununua umeme huo na si mitambo.

Hata hivyo Tanzania Daima Jumapili, imebaini kuwa serikali inaendelea kupata wakati mgumu wa kuwa na umeme wa uhakika kwani tangu kauli hizo kutolewa, hakuna aliye tayari kununua mitambo hiyo.

Vilevile mchakato wa kuipata mitambo mipya ya megawati 100 kwa kituo cha Dar es Salaam na megawati 60 kwa ajili ya Mwanza imeonekana kusuasua, jambo linaloipa nafasi mitambo ya Dowans kununuliwa na serikali.

Hivi karibuni TANESCO ilitangaza kufuta zabuni hizo zilizokuwa zimetangazwa kwa namba PA/001/09/HQ/W/016 kwa ajili ya kununua mtambo wa kutumia gesi kwa ajili ya kituo cha kuzalisha umeme cha Ubungo, jijini Dar es Salaam ile ya Mwanza ilitangazwa kwa namba PA/001/09/HQ/W/018.

Tangazo hilo lilifafanua kwamba zabuni hiyo itatangazwa tena kwa wale walioshiriki kuzingatia kifungu cha 54(5) cha Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004.

Tanzania Daima Jumapili, ilipomtafuta Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha, kuelezea sababu ya uamuzi huo wa kufuta zabuni hizo mbili alisema kwamba wizara haihusiki na suala hilo.

Meneja Mawasiliano wa TANESCO, Badra Masoud, alipoulizwa sababu za shirika hilo kuchukua uamuzi wa kufuta zabuni hiyo bila ya kutaja sababu, alisema zilishawahi kutajwa siku za nyuma.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa na uchumi wanaiona hatua hiyo ya kufuta zabuni za kununua mitambo mipya kama ilivyokubaliwa hapo awali ni njia ya kujenga mazingira ya kutaka Dowans ikubalike kwa wananchi na wanasiasa.

Wachambuzi hao wanaeleza kuwa bila ya kuwepo kwa mbinu hizo serikali za kutangaza na kufuta zabuni hizo watu hawatakubali mitambo hiyo inunuliwe kwa kuwa ilirithi mkataba kutoka kwa kampuni hewa ya Richmond.

Wanabainisha kuwa kwa hali ilivyo wananchi wanaaminishwa kuwa kuipata mitambo mipya ni mchakato mrefu zaidi na huenda nchi ikaingia katika mgawo wa umeme kama ilivyotekea miaka ya nyuma.

Tanzania Daima Jumapili ilizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah, kufahamu hatua ambayo imefikiwa na serikali tangu ipokee mapendekezo ya kununua mitambo ya Dowans na kuachana na IPTL.

Khijjah, alikiri ya kwamba mapema mwaka huu kabla ya kikao cha 18 hakijaanza mjini Dodoma, wizara yake ilipeleka ripoti kwa Kamati ya Fedha na Uchumi ikiainisha mzigo wa gharama unaobebwa na serikali kwa kuendelea kuitumia mitambo ya IPTL.

"Ile ripoti ilikuwa ni ushauri kwa wizara na sisi tulikuja kuiwasilisha mbele ya kamati. Imeainisha kila kitu ndiyo maana serikali inaharakisha ununuzi wa mitambo kwa ajili ya vituo vya Dar es Salaam na Mwanza," Kijjah aliliambia gazeti hili.

Alipoulizwa hatua iliyofikiwa na serikali katika utekelezaji wa ripoti hiyo, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa Dowans, Kijjah alisema uamuzi huo haujachukuliwa kutokana na hali ya utata uliojitokeza juu ya umiliki wake.

"Hatujafikia hatua hiyo baada ya kutokea malumbano ya hapa na pale. Majadiliano bado yanaendelea," alisema.

Ripoti hiyo, ambayo katibu mkuu alisema kuwa imeainisha kwa mapana gharama hizo, imebainisha kuwa serikali inaweza kutumia sh bilioni 6.4 pekee iwapo itanunua mitambo ya Dowans kuliko gharama inazoingia sasa kuiendesha IPTL.

IPTL iliyoingia nchini mwaka 1997 wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, inaligharimu taifa kiasi cha sh bilioni 20 kila mwezi, zikiwa ni gharama za kununulia mafuta lita 14,125 za mafuta mazito pamoja na kuwalipa wafanyakazi.

Ripoti hiyo imetoa mchanganuo wa gharama hizo unaoonyesha kila mwezi serikali inalazimika kununua kiasi hicho cha mafuta kwa gharama ya sh bilioni 13.6 kila mwezi, kununua mafuta mengine kwa sh milioni 996 na sh bilioni 2 kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi.

Chapuo kwa ajili ya mitambo ya Dowans imekuja kwani ripoti hiyo imekwishabainisha wazi kuwa iwapo itatumika, kiasi kisichopungua sh bilioni 13 kitaokolewa kila mwezi na kukielekeza katika huduma nyingine za kijamii ambazo zinalegalega.

Katika kile kinachoonekana kuitiisha serikali na kuona hakuna mbadala mwingine zaidi ya Dowans, ni kuwa iwapo mitambo ya IPTL haitatumika, taifa litagharamika mara sita zaidi ya kiasi kilichopo kwa sasa.

Ripoti hiyo imeweka bayana kuwa pamoja na Dowans kuonekana kuwa ahueni kuliko IPTL, kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha umeme wa uhakika wa megawati 105 kwa gharama ya sh bilioni 6.4 kwa mwezi badala ya takriban sh bilioni 20 zinazolipwa kila mwezi kwa IPTL inayozalisha megawati 100.

Kupanuka kwa shughuli za kiuchumi huku idadi kubwa ya watu ikiingia katika kundi la watu wenye kipato cha kati, taifa lina upungufu wa megawati 225 huku takwimu zikionyesha ni asilimia 14 tu ya Wanzania takriban milioni 40 ndiyo wanaotumia umeme majumbani mwao.

Source: Tanzania Daima - Sauti ya Watu
 
Who is the government and who is Dowans?! Kwa nini wanaogopa kushambuliwa kama wanafanya jambo la maana! something fishy here! Hii mitambo si tuliikataa! Hiyo nguvu ya kutaka ku-lazimisha mitambo inunuliwae inatoka kwa nani hasa! Why Dowans anyway!
Hatutaki kununua mali za wizi sisi! Hiyo mitambo waichukue wakawashe umeme majumbani kwao!
 
Who is the government and who is Dowans?! Kwa nini wanaogopa kushambuliwa kama wanafanya jambo la maana! something fishy here! Hii mitambo si tuliikataa! Hiyo nguvu ya kutaka ku-lazimisha mitambo inunuliwae inatoka kwa nani hasa! Why Dowans anyway!
Hatutaki kununua mali za wizi sisi! Hiyo mitambo waichukue wakawashe umeme majumbani kwao!
Tulishasema hapa JF kitambo sana kwamba mitambo hiyo kwa njia moja au nyingine
itanunuliwa tu. Nani atakubali Rostum ale hasara? Halafu kumbuka huu ni mwaka wa uchaguzi. CCM wataenda wapi kuchota EPA nyingine?
 
Pesa ya kampeni hiyo,

lakini nini jipya hapa? mlitegemea kitu tafauti?

Mkuu i knew it, tulianza na kesi ya Ditopile tulisema ameua bila kukusidia, that was it. "justice" was done. Tukaja na EPA tukasema tutawafikisha mahakamani, na tukazuga kwa kuwaweka kina Mramba na Yona rumande na kesi nyingine zimeiva hivi karibuni tutawafikisha mahakamani....that was it, tukaanza kuhalalisha ujinga wetu wa IPTL na kuanza kununua umeme wao....tukathibitisha ya Julius a.k.a Nyani Ngabu (ndivyo tulivyo), tukafunga mjadala wa Richmond kimya kimya kama vile haupo na kama vile hatukuibiwa pesa...., na sasa tuko Dowans....come October 2010, kila kitu kitakuwa kimefunikwa na tutakuwa tunapita. Who will be the loser?? Tanzania, Tanzanians and that will go on and on.
 
Halafu sijui huo mradi wa 132KV kutoka Ubungo hadi Makumbusho wataunganisha na mitambo hiyo au itakuwaje?
 
Back
Top Bottom