Serikali yafuta utaratibu wa kuagiza mbolea kwa zabuni, sasa Wafanyabiashara wote ruksa kuingiza mbolea nchini!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,598
141,413
Waziri wa kilimo Prof Mkenda amesema serikali imefuta utaratibu wa kuagiza mbilea kwa zabuni na kuanzia sasa wafanyabiashara wote wenye uwezo wanaruhusiwa kuingiza mbolea nchini.

Mkenda amesema utaratibu wa tenda ulipelekea bei ya mbilea kupanda sana hivyo wafanyabiashara wanaruhusiwa kuingiza mbolea na kuuza kulingana na bei ya soko ( soko huria(

Chanzo: ITV habari
 
Kwahiyo mbolea yoyote ile inaweza kuingizwa nchini kama zamani hata mbolea zilizoisha muda wake.

Vipi kuhusu viwanda vya mbolea kikiwemo kile cha kigeni kule Kagera?

Mbolea ni sehemu ya "Food Security" hakuna viongozi wanaozingatia hilo.

Wizara iweke utaratibu wa kudhibiti ubora wa mbolea na wapi zitoka.
 
Kwahiyo mbolea yoyote ile inaweza kuingizwa nchini kama zamani hata mbolea zilizoisha muda wake.

Vipi kuhusu viwanda vya mbolea kikiwemo kile cha kigeni kule Kagera?

Mbolea ni sehemu ya "Food Security" hakuna viongozi wanaozingatia hilo.
Hakuna wanachoweza zaidi ya kuharibu tupu
 
Wewe agiza mbolea mamlaka za kukagua ubora wa Mbolea zipo mbolea yako ikikdhi viwango itaingizwa sokoni....mbona hata kwenye sukari wale waliopewa vibali maalumu waliwahi kuleta sukari mbovu toka Brazil.
 
Hakuna wanachoweza zaidi ya kuharibu tupu
JPM aliwapa waturuki fulani hivi shamba kubwa sana kama hekari 33 au zaidi sehemu moja hivi ukielekea Morogoro.

Wale waturuki wanalima mapapai kwa ajili ya soko la nje.

Watanzania tupo tunapigana vikumbo Kariakoo na kuliunguza soko.

JPM aliwapa masharti waturuki wale waendeleze eneo lote la shamba na vijiji jirani.

Hadi leo wanavijiji wameajiriwa pale shambani na pana shule, zahanati na huduma zingine zote uzijuazo weye.

Pita nyakati za usiku utadhani wapita Ankara.

Wafahamu wale wananchi wanalipwa kiasi gani kwa mwezi? (labda waturuki wabadilike sasa hivi.

Tukipata wawekezaji tuzungumze nao na si kuanza kutanguliza bakuli la 10%
 
Wewe agiza mbolea mamlaka za kukagua ubora wa Mbolea zipo mbolea yako ikikdhi viwango itaingizwa sokoni....mbona hata kwenye sukari wale waliopewa vibali maalumu waliwahi kuleta sukari mbovu toka Brazil.
Watanzania tayari tumelishwa sukari mbovu, mafuta ya kula mabovu na kila aina ya takataka.

Madawa yanayoingizwa mengi ni expired na yanakuwa supplied ndani ya mfumo kwa kubadili details ndogo tu.

Ndo maana baadhi ya watanzania akili zao wazifahamu wenyewe.
 
Back
Top Bottom