Serikali yafuta kodi ya pango la ardhi katika majengo yanayotoa huduma za jamii bila faida

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Serikali imefuta kodi ya pango la ardhi katika majengo na maeneo yote ya taasisi ambazo zinatoa huduma katika jamii bila kufanya biashara na kuzalishi faida

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na kufafanua kuwa majengo haya ni ya binafsi na Serikali

Akitolea mfano amesema ni Zahanati, Mashule, Kanisa, Misikiti na majengo mengine kama hayo. Viwanja vitapimwa lakini hawatalipia kodi hiyo

Aidha, ameongeza kuwa maeneo ya biashara kama 'Mlimani City' ambalo lipo ndani ya chuo litapimwa na eneo hilo litalipiwa kodi ila eneo la chuo halitalipiwa

====

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema serikali imefuta kodi ya pango la ardhi katika majengo na maeneo yote ya taasisi ambazo zinatoa huduma katika jamii bila kufanya biashara na kuzalishi faida.

Waziri Lukuvi amesema hayo wakati alipofanya ziara ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ya wakazi wa jiji la arusha ambapo ametoa agizo kwa maafisa wote wanaohusika na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi kuziondoa katika orodha ya madeni taasisi binafsi, za dini, za serikali na mashirika yote ambayo hayazalishi faida.

Hata hivyo waziri Lukuvi amesema kwamba sheria hiyo imeanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 julai 2018 ambapo Serikali kupitia Bunge imeridhia kuondolewa kodi ya pango la ardhi taasisi za elimu, shule za msingi, sekondari, vyuo, vituo vya afya, hospitali, taasisi za umma na taasisi za dini kama misikiti na makanisa ambayo yalikuwa yanalipa kodi hiyo.

Pamoja na msamaha huo wa kodi Waziri Lukuvi amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri kote nchini kupima maneo yanayotoa huduma kwa jamii ili kuitambua mipaka ya shule, zahanati na maeneo mengine na kuzipatia hati miliki za ardhi zitakazo wawezesha kutambua mipaka ya maeneo hayo lakini taasisi hizo hazitalipa kodi tena.

“Yale maeneo ambayo yana hati ya pamoja wakati sehemu ya eneo inatumika kuzalisha faida basi maafisa ardhi watakokotoa eneo linalozalisha faida na wataliondoa lile eneo linalozalisha faida na kulitoza kodi, mfano eneo la Mlimani City ambalo linazaliosha faida katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam” amsema Lukuvi.

Aidha, katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amesema kwamba kuanzia sasa vibali vya ujenzi vitakuwa vinatolewa kila wiki na vitakuwa vinatolewa na maafisa wa serikali waliopo wilayani ambao ni maafisa mipango miji, maafisa ardhi, wapimaji na wathamini ambao ni wataalamu.

“Kulikuwa na ucheleweshaji wa utoaji vibali vya ujenzi Mheshimiwa Rais ameshatoa maelekezo kwamba vibali vya ujenzi havitatolewa tena na kamati za madiwani kwasababu ilikuwa inachukua muda na walikuwa lazima walipwe posho, kwahiyo vibali vya ujenzi vitakuwa vinatoka kila wiki na vitatolewa na wataalamu wa serikali waliopo wilayani” amsema Mheshimiwa Lukuvi.

Amesema kwamba Serikali imeamua kubadili utaratibu huo ili kuwawezesha wananchi ambao walikuwa wana fedha ya kujenga maeneo yao lakini vibali vya ujenzi vilikuwa havitolewi kwa wakati, na kuna watu ambao walikuwa wanakaa mwaka mzima wakisubiri vibali vya ujenzi kitendo amabacho kilichangia ujenzi holela katika miji.

Mheshimiwa Lukuvi amesema serikali imeamua kuchukua hatua hizo ili kuondoa kero kwa wananchi ambao walikuwa wanapata tabu ya urasimu uliokuwepo hapo awali, kitu ambacho kilikuwa ni kikwazo katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesikiliza kero za migogoro ya ardhi ya wananchi zaidi ya 200 wa jiji la Arusha ambao walihudhuria katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Azimio la Arusha jijini hapo.
 
Bado sijaelewa, kuna maeneo ya kanisa na kanisa lenyewe. Eneo la kanisa au msikiti linaweza kuwa na shule, maduka, hostels na kumbi za starehe; bustani, mashamba na mifugo mbalimbali, vyote hivyo viendeshwe bila faida? Au kuanzia sasa faida ktk miradi ya misikiti na makanisa itajulikana kama zaka, efd-free zone!
 
Soma uelewe wamesema yasiyo ya biashara na yanayotoa huduma bila kuzalisha faida
 
Asante, ila usifikiri kuwa sijaelewa, bali hata nyumba unayoishi mwenyewe unalipia kodi (property tax). Kama ni hivyo
a. Hiyo kodi ilipiwe chumba au upande uliopangishwa
b. Umempangisha mtu fremu ya duka au kinyozi mbele ya nyumba yako, kosa! Yani kodi ya jengo lako itazidi, wakati huo mwenye duka nae analipa kodi kwa vat au efd!
c. Ardhi ni mali yetu sote Watanzania kwahiyo basi, kama kanisa au msikiti hautozwi kodi ya ardhi na nyumba unayoishi (au sehemu unayokaa) isitozwe kodi. Inazalisha faida gani?

Lakini kwa sasa haijalishi wewe ni mstaafu huna kazi au biashara, na hiyo nyumba umetumia vihela vya mshahara au pension yako kiduchu ukajenga uzeeni. Watakufata mpaka kaburini!

Mwisho, busara iliyotumika kwa uamuzi uliofanywa na Bunge, itumike kuhusu pia kodi za ardhi na majengo kwa wananchi bila kujali hali ya jengo, ilimradi linatumika kwa makazi binafsi au familia ya mtu kwa kuzingatia niliyosema hapa juu.
 
1_19_o.jpg

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema serikali imefuta kodi ya pango la ardhi katika majengo na maeneo yote ya taasisi ambazo zinatoa huduma katika jamii bila kufanya biashara na kuzalishi faida.

Waziri Lukuvi amesema hayo wakati alipofanya ziara ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ya wakazi wa jiji la arusha ambapo ametoa agizo kwa maafisa wote wanaohusika na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi kuziondoa katika orodha ya madeni taasisi binafsi, za dini, za serikali na mashirika yote ambayo hayazalishi faida.

Hata hivyo waziri Lukuvi amesema kwamba sheria hiyo imeanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 julai 2018 ambapo Serikali kupitia Bunge imeridhia kuondolewa kodi ya pango la ardhi taasisi za elimu, shule za msingi, sekondari, vyuo, vituo vya afya, hospitali, taasisi za umma na taasisi za dini kama misikiti na makanisa ambayo yalikuwa yanalipa kodi hiyo.

Pamoja na msamaha huo wa kodi Waziri Lukuvi amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri kote nchini kupima maneo yanayotoa huduma kwa jamii ili kuitambua mipaka ya shule, zahanati na maeneo mengine na kuzipatia hati miliki za ardhi zitakazo wawezesha kutambua mipaka ya maeneo hayo lakini taasisi hizo hazitalipa kodi tena.

“Yale maeneo ambayo yana hati ya pamoja wakati sehemu ya eneo inatumika kuzalisha faida basi maafisa ardhi watakokotoa eneo linalozalisha faida na wataliondoa lile eneo linalozalisha faida na kulitoza kodi, mfano eneo la Mlimani City ambalo linazaliosha faida katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam” amsema Lukuvi.

Aidha, katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amesema kwamba kuanzia sasa vibali vya ujenzi vitakuwa vinatolewa kila wiki na vitakuwa vinatolewa na maafisa wa serikali waliopo wilayani ambao ni maafisa mipango miji, maafisa ardhi, wapimaji na wathamini ambao ni wataalamu.

“Kulikuwa na ucheleweshaji wa utoaji vibali vya ujenzi Mheshimiwa Rais ameshatoa maelekezo kwamba vibali vya ujenzi havitatolewa tena na kamati za madiwani kwasababu ilikuwa inachukua muda na walikuwa lazima walipwe posho, kwahiyo vibali vya ujenzi vitakuwa vinatoka kila wiki na vitatolewa na wataalamu wa serikali waliopo wilayani” amsema Mheshimiwa Lukuvi.

Amesema kwamba Serikali imeamua kubadili utaratibu huo ili kuwawezesha wananchi ambao walikuwa wana fedha ya kujenga maeneo yao lakini vibali vya ujenzi vilikuwa havitolewi kwa wakati, na kuna watu ambao walikuwa wanakaa mwaka mzima wakisubiri vibali vya ujenzi kitendo amabacho kilichangia ujenzi holela katika miji.

Mheshimiwa Lukuvi amesema serikali imeamua kuchukua hatua hizo ili kuondoa kero kwa wananchi ambao walikuwa wanapata tabu ya urasimu uliokuwepo hapo awali, kitu ambacho kilikuwa ni kikwazo katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesikiliza kero za migogoro ya ardhi ya wananchi zaidi ya 200 wa jiji la Arusha ambao walihudhuria katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Azimio la Arusha jijini hapo.
 
Taasisi za elimu walitakiwa walipe kama ada tuna lipa ila kama hatulipii vijana wetu basi nao wapate hiyo nafuu ya kuto kulipa
 
images (6).jpg

WAZIRI Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewataka maofisa wote wanaohusika na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi, kuziondoa katika orodha ya madeni taasisi binafsi, taasisi za dini, taasisi za serikali na mashirika yote ambayo hayazalishi faida.
Amesema agizo hilo linatokana na serikali kufuta kodi ya pango la ardhi katika majengo na maeneo yote ya taasisi zinazotoa huduma katika jamii bila kufanya biashara na kuzalisha faida.
Lukuvi amesema hayo wakati alipofanya ziara ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ya wakazi wa Jiji la Arusha.
Amesema sheria hiyo imeanza kutekelezwa kuanzia Julai mwaka huu, ambapo serikali kupitia Bunge imeridhia kuondolewa kodi ya pango la ardhi taasisi za elimu, shule za msingi, sekondari, vyuo, vituo vya afya, hospitali, taasisi za umma na taasisi za dini kama misikiti na makanisa, ambayo yalikuwa yanalipa kodi hiyo.
Pamoja na msamaha huo wa kodi, Waziri Lukuvi aliwaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri kote nchini kupima maneo yanayotoa huduma kwa jamii ili kuitambua mipaka ya shule, zahanati na maeneo mengine na kuzipatia hati miliki za ardhi, zitakazo wawezesha kutambua mipaka ya maeneo hayo lakini taasisi hizo hazitalipa kodi tena.
"Yale maeneo ambayo yana hati ya pamoja wakati sehemu ya eneo inatumika kuzalisha faida basi maofisa ardhi watakokotoa eneo linalozalisha faida na wataliondoa lile eneo linalozalisha faida na kulitoza kodi, mfano eneo la Mlimani City Lukuvi alisikiliza kero za migogoro ya ardhi ya wananchi zaidi ya 200 wa Jiji la Arusha, ambao walihudhuria katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Azimio la Arusha jijini hapo.
 
Back
Top Bottom