Serikali yafunguka utata wa kampuni ya kununua korosho

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,445
2,000
Baada ya kusambaa kwa taarifa za kampuni ya Indo Power ya Kenya kutokuwa na uwezo wa kununua tani 100,000 za korosho nchini, Serikali imejibu na kusema haiangalii mambo mengine, bali uwezo wake wa kutekeleza masharti ya mkataba.

Januari 30, Serikali ilitangaza kumpata mteja atakayenunua tani 100,000 za korosho kwa Dola 180,000 za Marekani (zaidi ya Sh418 bilioni) na wiki mbili tangu kutolewa kwa taarifa hiyo, gazeti la kila wiki la The East African limechapisha habari kuwa kampuni hiyo iliyosajiliwa mwaka 2016 haina historia ya kufanya miamala mikubwa kiasi hicho.

“Kampuni hii iliyojikita kwenye biashara ya kimataifa haina tovuti. Hata hivyo, taarifa zake za usajili zinaonyesha haina akaunti za benki, wanasheria wala katibu wa kampuni na haina wakaguzi wa hesabu,” limesema gazeti hilo.

Kwenye miamala iliyofanya tangu ianzishwe, The East African linasema Indo Power haijawahi kuwa na mkataba japo wa Dola 10 milioni na kwa maelezo ya kampuni husika, fedha za kufanikisha mkataba wake na Tanzania utafanikishwa na mkopo kutoka benki ya nje ya Kenya.

Hata hivyo, katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa Joseph Buchweishaija aliiambia Mwananchi jana kuwa historia sio hoja ya msingi waliyoipa kipaumbele.

“Inayouza korosho ni Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko, jukumu letu lilikuwa kufanikisha biashara tu. Unachoangalia ni uwezo wa mnunuzi kulipa bei anayoitaka muuzaji yanayobaki wanaelewana wao,” alisema katibu mkuu huyo.

Nyaraka za usajili wa kampuni hiyo, The East African linasema zinaonyesha ina makao makuu yake katika Mji wa Thika, nje kidogo ya Jiji la Nairobi katika jengo la Indo House ambalo lilipotafutwa halikupatikana.

Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Indo Power, Brian Mutembei ameliambia gazeti hilo kuwa wamejikita kwenye biashara ya mazao ikijihusisha zaidi na kahawa, kuku, uingizaji wa pombe uuzaji jumla wa bidhaa za mafuta na haijawahi kufanya biashara ya korosho.

Profesa Buchweishaija alisema “inawezekana ikawa haijawahi kufanya biashara hii lakini imeona fursa ikaamua kuitumia. Sote tunafahamu hata matajiri wakubwa hawana fedha, huzitoa benki. Hawa nao wamechukua mkopo benki. Watanzania nasi tunatakiwa kuzitumia fursa zinazojitokeza kila inapobidi.”

Kutokana na uchanga wake kufanikisha mkataba huo, Mutembei ameliambia The East African kuwa hati ya muamana (letter of credit) ya mkataba wa Indo Power na bodi ya mazao mchanganyiko imetolewa na benki ya nje ya Kenya.

“Tumeshapeleka hati ya malipo ya fedha zote zinazohitajika kwa Serikali ya Tanzania. Imetolewa na benki ya nje ambayo siwezi kuitaja kutokana na sababu za kibiashara,” amenukuliwa Mutembei na gazeti hilo.

Kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mauzo ya korosho uliofanywa kati ya mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Dk Hussein Mansour na Mutembei, walikuwapo pia Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda, Joseph Kakunda na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga.

Pamoja na hao, alikuwepo Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu ambaye aliliambia gazeti hilo kuwa ni wajibu wake kufanikisha biashara kati ya kampuni za Kenya zinazotaka kuwekeza au kufanya biashara na Tanzania.

Bila kujali uwezo wa kampuni hiyo, malipo ya mkataba uliosainiwa, taarifa zinasema yanatarajiwa kufanywa kwenye akaunti iliyopo BoT ndani ya wiki moja baada ya kuafikiwa kwa makubaliano hayo.

Hata hivyo, alipotafutwa Gavana Luoga kujua kama malipo hayo yamefanyika na kupata taarifa za ziada alisema bodi ya nafaka itakuwa inafahamu zaidi kuliko yeye.

“Wasiliana nao,” alisema kwa kifupi kupitia kwa msaidizi wake.

Alipoulizwa Dk Mansoor hakutaka kuzungumzia suala hilo akisema, “kuna mambo yanaendelea hivyo siwezi kusema lolote kwa sasa mpaka yatakapokamilika, naomba uwe na subira.”

Alipoulizwa kama mambo yote muhimu yalizingatiwa kabla ya kuingia mkataba na kampuni hiyo, alisema: “Wizara ya Viwanda ndio iliyoufanikisha. Wao ndio wataalamu, hata kama sisi tunasaini wao wanatuwezesha.”

Chanzo: Mwananchi
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,905
2,000
Kwa ufupi

Baada ya kuwapo habari kwamba kampuni ya Indo Power haina historia ya kufanya miamala mikubwa na haitoweza kununua tani 100,000 za korosho ambazo bei yake ni zaidi ya Sh418 bilioni, Serikali imesema kampuni hiyo imechangamkia fursa na inaweza kuchukua mkopo benki.

Kuona vituko Zaidi bofya hapa: Serikali yafunguka utata wa kampuni ya kununua korosho

Sent using Jamii Forums mobile app
Coarterm nielimishe, hivi kuna nini kimejificha huko nyuma kutafuta kampuni kama hii. kuna mbia ndania wateule au Magu mwenywe? Kwanini itafutwe kampuni mavi hivi?
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,947
2,000
Kama ni hivi basi Serikali ya Tanzania inaweza kufanya mkataba hata na wahuni tu wa barabarani..

Maana hawa INDO hata kama ni watakatishaji fedha au drug dealers serikali ni ngumu kugundua kwa style hii ya kufanya biashara..

Kuna mahala nimeona kwamba huyu MD wa INDO ni mshirika wa karibu wa Vice President wa Kenya (Ruto) na huku tena kuna tuhuma kutoka kwa Zitto kwamba hizi pesa zakulipia hizi korosho zimekwapuliwa kutoka BOT kwenye akaunti ya Mashirika ya umma na hawa INDO ni danganya toto tu..

Awamu hii bhana.
 
kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
210
1,000
Ifike mahali tuseme na tuwaambie viongozi wasitoe ufafanuzi wa kila Jambo kwenye vyombo vya habari, sikutegemea kama hawa tunaowahita makatibu wakuu wanaweza kuwa na majibu ya namna hii.

Wanaifanya nchi ionekane kama haina Sheria bali ni utashi tu mtu flani. Serikali siku zote inapaswa kufanya biashara safi na ndiyo maana Sheria zipo. Leo unasema hoja siyo kumjua mnunuzi bali unataka fedha ziingie BOT, kwa hiyo hata fedha chafu nazo zinaruhusiwa kuingia BOT?

Kama ni fedha tu kuingia BOT je wale waliokuwa mtwara Tena watanzania wenzetu mbona hatukuwapa hii condition?

Nchi inaitaji wanamikakati hasa majasusi wa kiuchumi...tumejaza waalimu wa vyuo serikali Sasa hata Siri za utendaji wa serikali zinavuja bila wenyewe kutambua kwamba siri wanazivujisha.

Mnawapa credit wapinzani wapate hoja daily kwa kushindwa kufungana speed gavana.......jaribuni kuiba mawazo kwa wazee waliotangulia au toeni semina elekezi kudhibiti uzungumzaji wa viongozi wakubwa kwenye media.

Hapo wanahojiwa watu wawili ndani ya serikali wanajikanyaga wakati wote Hawa walikuwepo kwenye kusaini mkataba Arusha, means hawakujua chanzo Cha mkataba na hawakujua malengo ya mkataba ndio maana wanajibu vitu visivyoeleweka.

Due diligence it's so important kwenye business za serikali na kampuni binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,331
2,000
Eti...hatuangalii yaliyopita ilimradi tunataka mnunuzi"...!What a puke of talking!
-Unapinga ufisadi
-Unapinga utakatishaji fedha
-Unapinga wizi
-Unapinga upiga deals
Unajinadi kwa maneno mengi uonekane u mwema.Halafu unaambiwa huyu unayefanya naye biashara ana mambo yasiyoeleweka vema kitaalamu,kibiashara na kiuweledi.Weye unatoa majibu ya kipuuzi kama kibaka ana alosto ya heroin?
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
23,375
2,000
Tutapambana Na Rushwa Na Wizi Serikalini Bila Kigugumizi Chochote, Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua
 
kisepi

JF-Expert Member
Jun 9, 2015
1,885
2,000
Eti...hatuangalii yaliyopita ilimradi tunataka mnunuzi"...!What a puke of talking!
-Unapinga ufisadi
-Unapinga utakatishaji fedha
-Unapinga wizi
-Unapinga upiga deals
Unajinadi kwa maneno mengi uonekane u mwema.Halafu unaambiwa huyu unayefanya naye biashara ana mambo yasiyoeleweka vema kitaalamu,kibiashara na kiuweledi.Weye unatoa majibu ya kipuuzi kama kibaka ana alosto ya heroin?
Tulishawapa nchi.tuaikilizie tu bloo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,746
2,000
Kama Magufuli hajajuwa Mungu anampiga mapigo kumi kama ya Farao basi atajuwa ha ha kangomba pedeshee la kenya limekuja kumchezesha ngoma ya sindima nilidhani ni muweza
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,544
2,000
Baada ya kusambaa kwa taarifa za kampuni ya Indo Power ya Kenya kutokuwa na uwezo wa kununua tani 100,000 za korosho nchini, Serikali imejibu na kusema haiangalii mambo mengine, bali uwezo wake wa kutekeleza masharti ya mkataba.

Januari 30, Serikali ilitangaza kumpata mteja atakayenunua tani 100,000 za korosho kwa Dola 180,000 za Marekani (zaidi ya Sh418 bilioni) na wiki mbili tangu kutolewa kwa taarifa hiyo, gazeti la kila wiki la The East African limechapisha habari kuwa kampuni hiyo iliyosajiliwa mwaka 2016 haina historia ya kufanya miamala mikubwa kiasi hicho.

“Kampuni hii iliyojikita kwenye biashara ya kimataifa haina tovuti. Hata hivyo, taarifa zake za usajili zinaonyesha haina akaunti za benki, wanasheria wala katibu wa kampuni na haina wakaguzi wa hesabu,” limesema gazeti hilo.

Kwenye miamala iliyofanya tangu ianzishwe, The East African linasema Indo Power haijawahi kuwa na mkataba japo wa Dola 10 milioni na kwa maelezo ya kampuni husika, fedha za kufanikisha mkataba wake na Tanzania utafanikishwa na mkopo kutoka benki ya nje ya Kenya.

Hata hivyo, katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa Joseph Buchweishaija aliiambia Mwananchi jana kuwa historia sio hoja ya msingi waliyoipa kipaumbele.

“Inayouza korosho ni Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko, jukumu letu lilikuwa kufanikisha biashara tu. Unachoangalia ni uwezo wa mnunuzi kulipa bei anayoitaka muuzaji yanayobaki wanaelewana wao,” alisema katibu mkuu huyo.

Nyaraka za usajili wa kampuni hiyo, The East African linasema zinaonyesha ina makao makuu yake katika Mji wa Thika, nje kidogo ya Jiji la Nairobi katika jengo la Indo House ambalo lilipotafutwa halikupatikana.

Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Indo Power, Brian Mutembei ameliambia gazeti hilo kuwa wamejikita kwenye biashara ya mazao ikijihusisha zaidi na kahawa, kuku, uingizaji wa pombe uuzaji jumla wa bidhaa za mafuta na haijawahi kufanya biashara ya korosho.

Profesa Buchweishaija alisema “inawezekana ikawa haijawahi kufanya biashara hii lakini imeona fursa ikaamua kuitumia. Sote tunafahamu hata matajiri wakubwa hawana fedha, huzitoa benki. Hawa nao wamechukua mkopo benki. Watanzania nasi tunatakiwa kuzitumia fursa zinazojitokeza kila inapobidi.”

Kutokana na uchanga wake kufanikisha mkataba huo, Mutembei ameliambia The East African kuwa hati ya muamana (letter of credit) ya mkataba wa Indo Power na bodi ya mazao mchanganyiko imetolewa na benki ya nje ya Kenya.

“Tumeshapeleka hati ya malipo ya fedha zote zinazohitajika kwa Serikali ya Tanzania. Imetolewa na benki ya nje ambayo siwezi kuitaja kutokana na sababu za kibiashara,” amenukuliwa Mutembei na gazeti hilo.

Kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mauzo ya korosho uliofanywa kati ya mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Dk Hussein Mansour na Mutembei, walikuwapo pia Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda, Joseph Kakunda na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga.

Pamoja na hao, alikuwepo Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu ambaye aliliambia gazeti hilo kuwa ni wajibu wake kufanikisha biashara kati ya kampuni za Kenya zinazotaka kuwekeza au kufanya biashara na Tanzania.

Bila kujali uwezo wa kampuni hiyo, malipo ya mkataba uliosainiwa, taarifa zinasema yanatarajiwa kufanywa kwenye akaunti iliyopo BoT ndani ya wiki moja baada ya kuafikiwa kwa makubaliano hayo.

Hata hivyo, alipotafutwa Gavana Luoga kujua kama malipo hayo yamefanyika na kupata taarifa za ziada alisema bodi ya nafaka itakuwa inafahamu zaidi kuliko yeye.

“Wasiliana nao,” alisema kwa kifupi kupitia kwa msaidizi wake.

Alipoulizwa Dk Mansoor hakutaka kuzungumzia suala hilo akisema, “kuna mambo yanaendelea hivyo siwezi kusema lolote kwa sasa mpaka yatakapokamilika, naomba uwe na subira.”

Alipoulizwa kama mambo yote muhimu yalizingatiwa kabla ya kuingia mkataba na kampuni hiyo, alisema: “Wizara ya Viwanda ndio iliyoufanikisha. Wao ndio wataalamu, hata kama sisi tunasaini wao wanatuwezesha.”

Chanzo: Mwananchi
Hivi nani seaji wa hiyo kampuni (INDO) ? Jinsi Serikali ilivoongea kwenye hii habari, ni kama SERIKALI YETU NDO MSEMAJI WA INDO
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,303
2,000
Halafu huyu jamaa eti naye ni profesa

Hivi maprofesa wa bongo wamesomea Ujinga?

Yaani serikali haioni haja ya kuichunguza kampuni, ina maana hata wakiingiza pesa zinazotokana na Human Trafficking hiyo ni sawa tu hata kama ni pesa chafu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom