Serikali yafungua milango ya majadiliano kwa magazeti yaliyofungiwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kutaka vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa, linahusu televisheni za mtandaoni pekee.

Hata hivyo, Bashungwa ameeleza leo Jumatano, Aprili 7 2021 kuwa Serikali inafungua milango yake kwa vyombo vingine vya habari vilivyofungiwa kuangalia namna gani vinaweza kufunguliwa kwa mujibu wa sheria.

Kauli ya Bashungwa inatokana na madai ya wadau wa habari nchini, kutaka vyombo vya habari yakiwemo magazeti yaliyofungiwa kufunguliwa kupitia agizo hilo la Rais Samia.

Juzi, wakati akiwaapisha makatibu na manaibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, Rais Samia aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilifungiwa na kwamba, vipewe uhuru katika kutekeleza majukumu yake bila kuvunja sheria.

“Nasikia kuna vyombo vya habari mlifungia, vifungulieni na vifuate sheria, tusiwape mdomo wa kusema kwamba tanaminya uhuru wa kuzungumza.

“Tusifungie kibabe, wafungulieni na kuhakikisha wanafuata sheria na miongozo ya Serikali. Hakikisheni kila mliyempa ruhusa ye kuendesha chombo cha habari afuate sheria.

Kanuni ziwe wazi kuwa kosa hili adhabu yake ni hii na mnakwenda kulingana na adhabu mlizoziweka kwenye kanuni, tusifungie kibabe, viacheni vifanye kazi,” alisema Rais Samia.

Baada ya kauli hiyo, wadau wa habari walipongeza uamuzi huo wa Rais Samia huku wakiomba agizo hilo lifanyiwe kazi mara moja na mamlaka husika.

Hata hivyo, mjadala mkali uliibuka baada ya Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi kuhojiwa na kituo cha luninga cha Wasafi, akieleza kuwa uamuzi huo utahusu televisheni za mtandaoni pekee.

Baadhi ya wadau wa habari walitegemea kuona vyombo vyote vilivyofungiwa yakiwemo magazeti yakifunguliwa. Hata hivyo, kauli ya Bashungwa kuwa vyombo vingine nje ya televisheni za mtandaoni vinaweza kukaa mezani na wizara hiyo kila kimoja kulingana na kesi yake iliyosababisha kufungiwa.

Mwananchi
 
Very stupid approach

Ufafanuzi wa msigwa× stupid approach karma itamfuata bora angekaa kimya

Ufafanuzi wa Dr abbas x very stupid as well bora anangekaa kimya wakahandle hii issue internally

Hii ni first approach kwa Mh Rais kuwa hasimamii maneno yake na HUKO TWENDO NI KUBAYA

THIS MADAM ATAKUWA WORSE PRESIDENT EVER IN THIS PLANET
 
N mm cjamwelewa mama samia au hao wachini aliowapa maagizo ndio hawajamwelewa mama maana kila mmoja anasema lakee
 
Waziri wa habari mh Bashungwa amesema msamaha wa Rais Samia unahusu Online tv zaidi ya 460 zilizofungiwa pekee na siyo magazeti au kitu kingine chochote.

Bashungwa amesema atashughulikia magazeti yaliyofungiwa case by case hivyo wamiliki wa magazeti hayo wafike ofisini kwake kwa mazungumzo ya kutatua tatizo lililopo

Source BBC Dira ya Dunia

Ukinizingua Nitakuzingua!
 
Kwa hiyo mama alikosea?
IMG-20210406-WA0003.jpg
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kutaka vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa, linahusu televisheni za mtandaoni pekee...
Jaribio la hawa wateule wa rais likishinda basi ni mwanzo wa kuelewa kuwa mh rais yeye sii kauli ya mwisho katika nchi na ni dalili za kiti cha rais kutoheshimiwa.

Pili watu wale wale waliofungia hivyo vyombo vya habari ni vigumu sana kuwatumia hao hao kuvifungulia. Rais atakuwa amefanya kosa kubwa kurithi wateule wenye viapo kwa mtu mwingine.
 
Very stupid approach

Ufafanuzi wa msigwa× stupid approach karma itamfuata bora angekaa kimya...
Tangu lini Chadema wakaitakia mema ccm hadi wajipe kazi ya kumsifia rais Samia?.

Kazi ya kumsifia rais Samia ni ya MATAGA siyo ya chadema
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kutaka vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa, linahusu televisheni za mtandaoni pekee.

Hata hivyo, Bashungwa ameeleza leo Jumatano, Aprili 7 2021 kuwa Serikali inafungua milango yake kwa vyombo vingine vya habari vilivyofungiwa kuangalia namna gani vinaweza kufunguliwa kwa mujibu wa sheria.

Kauli ya Bashungwa inatokana na madai ya wadau wa habari nchini, kutaka vyombo vya habari yakiwemo magazeti yaliyofungiwa kufunguliwa kupitia agizo hilo la Rais Samia.

Juzi, wakati akiwaapisha makatibu na manaibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, Rais Samia aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilifungiwa na kwamba, vipewe uhuru katika kutekeleza majukumu yake bila kuvunja sheria.

“Nasikia kuna vyombo vya habari mlifungia, vifungulieni na vifuate sheria, tusiwape mdomo wa kusema kwamba tanaminya uhuru wa kuzungumza.

“Tusifungie kibabe, wafungulieni na kuhakikisha wanafuata sheria na miongozo ya Serikali. Hakikisheni kila mliyempa ruhusa ye kuendesha chombo cha habari afuate sheria.

Kanuni ziwe wazi kuwa kosa hili adhabu yake ni hii na mnakwenda kulingana na adhabu mlizoziweka kwenye kanuni, tusifungie kibabe, viacheni vifanye kazi,” alisema Rais Samia.

Baada ya kauli hiyo, wadau wa habari walipongeza uamuzi huo wa Rais Samia huku wakiomba agizo hilo lifanyiwe kazi mara moja na mamlaka husika.

Hata hivyo, mjadala mkali uliibuka baada ya Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi kuhojiwa na kituo cha luninga cha Wasafi, akieleza kuwa uamuzi huo utahusu televisheni za mtandaoni pekee.

Baadhi ya wadau wa habari walitegemea kuona vyombo vyote vilivyofungiwa yakiwemo magazeti yakifunguliwa. Hata hivyo, kauli ya Bashungwa kuwa vyombo vingine nje ya televisheni za mtandaoni vinaweza kukaa mezani na wizara hiyo kila kimoja kulingana na kesi yake iliyosababisha kufungiwa.

Mwananchi
The hallmarks of bad governance:

1. Ambiguity
2. Arbitrariness
3. Capriciousness
 
Waitike mazungumzo.
HUYU MWANAMKE SSH ASITU CHEZEE WANAUME......!

Abas na Baahungwa KAZENI, ONESHENI KUWA NINYI NI WANAUME.

Otherwise vyombo vya habari, VITA WADHARAU.
MLIFUNGA KWA SHERIA FUNGUENI KWA SHERIA.

Mwanamke ni mwanamke tu, hata AWE NANI.
 
Sasa hiyo sentensi ya chini ya nini.
Yaonekana roho yataka kukutoka kisa tu rais kawa wakike.
Vumilia tu ndio ishakuwa subiri awamu yake ipite uchague wanaume wenzio.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom