Serikali yafukuza kazi W/viti wa Vitongoji, waliochaguliwa na wananchi

wapo na wataendelea na kazi ya kuwaongoza makarani wa sensa kama kawaida na wameahidi kufanyakazi hiyo kufa na kupona kuhakikisha mambo yanakwenda kwa ufanisi wilayani hai

Sasa nini kimetokea? Vyombo vya Habari vimemnukuu RC vibaya au wewe umekaidi amri ya RC?
 
Hao wenyeviti mnawalipa za nini? Mbona huku Dodoma hawalipwi, km wanagoma waacheni wajiunge na MaDr na Walimu Watu watahesabiwa tu
 
wapo na wataendelea na kazi ya kuwaongoza makarani wa sensa kama kawaida na wameahidi kufanyakazi hiyo kufa na kupona kuhakikisha mambo yanakwenda kwa ufanisi wilayani hai
Kama kazi hii itafanywa baada ya vitisho, unadhani itakuwa na ufanisi???? Kwani malipo yao ni fedha nyingi??????
 
Sasa nini kimetokea? Vyombo vya Habari vimemnukuu RC vibaya au wewe umekaidi amri ya RC?

hii ilikuwa katika gazeti la mwananchi

WENYEVITI wa vitongoji 116 katika wilaya ya Hai,wametishia kutoshiriki zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia Agosti 26 nchini kote kwa madai wanaidai halmashauri hiyo kiasi cha Sh Mil 280.8 ikiwa ni fedha zao za posho kuanzia mwaka 2009 hadi sasa.
Mkuu wa mkoa huo,Leonidas Gama, aliyasema hayo katika mkutano wake na wanahabari akizungumzia maandalizi ya zoezi hilo ambalo alisema limekamilika kwa asilimia kubwa .
Pamoja na kuwepo kwa tishio hilo,mkuu wa mkoa alisema wenyeviti hao wamepewa muda wa siku moja kufafanua msimamo wao iwapo wanataka kuendelea kufanya kazi za serikali ama la kutokana na kwamba madai yaohayahusiani na shughuli ya sensa.
“Kwa sasa tunachangamoto mbili kubwa, hii ya kikundi cha waislamu na hawa wenyeviti wa vitongoji wilayani Hai….nimeongea na viongozi wa wilaya yao nikawataka kama msimamo wao ni kutoshiriki zoezi hili, basiwaandike barua ya kujiondoa katika nafasi zao za uenyekiti”alisema Gama..
Aidha Gama amesema kwa mujibu uongozi wa halmashauri ya wilaya, madai ya wenyeviti hao hayakulipwa mapema kutokana na kukosekana kwa fedha katika bajeti lakini kwa mwaka huu ni miongoni mwa madai yatakayopewakipaumbele katika malipo.
Kuhusu kikundi cha waislamu wanaopinga zoezi hilo kilichopo katika wilaya za Same,Mwanga,Moshi mjini na Hai ,Gama alisema tayari jitihada zimefanyika kuwashirikisha viongozi wa madhehebu ya dini ili kuwaelimisha waumini wao kushiriki zoezi hilo.
Alisema mkoa una makarani wa sensa 4937 ambao wamegawanyika katika makundi mawili moja likiwa na makarani 2156 kwa ajili ya kujaza dodoso refu na 2279 kwa ajili ya Dodoso fupi huku makarani wa akiba wakiwa 153 na wasimamizi 349.
Akizungumzia vituo kwa ajili ya zoezi hilo alisema kuna vituo 3357 vilivyogawanywa katika makundi mawili ya Dodoso fupi vilivyopo 2279 na dodoso refu vipo 1078 na kwamba Agosti 23 imetengwa kwa ajili ya kutambua maeneo ya kazi ambapo wataongozwa na wenyeji wao ambao ni wenyeviti wa vitongoji,vijiji na mitaa.
Mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kutunza kumbukumbu za taarifa za watu watakaolala katika nyumba zao kwa usiku wa kuamkia Agosti 26 na kwamba zoezi hilo litafanywa kwa siku saba na wasihofu iwapo makaranihawatafika tarehe 26 bali wasubiri hadi watakapofika kwa takribani siku saba
Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook
 
...Madai ya tangia mwaka 2009 hayakuweza kulipwa kutokana na 'kukosekana kwa fedha katika bajeti' lakini 'mwaka huu ni miongoni mwa madai yatakayopewa kipaumbele katika malipo'.

..Majibu mepesiii kwa maswali magumu.
 
labda kukufafanulia tu suala siyo deni hilo la nyuma bali taratibu kufuatwa,suala la fedha za vitongoji lipo kisheria kwa maana ni asilimia ishirini ya mapato ya halmashauri lazima ielekezwe vijijini hivyo kwa mwaka huu mwelekeo ni kuhakikisha kwamba fedha utaratibu unasimamiwa siyo suala la majibu rahisi ama magumu ndugu yangu
 
...Mkuu, Asante kwa ufafanuzi lakini nahisi kama hukuielewa vyema Hoja yangu ambayo ni kwamba:
Hawa Viongozi wanasemekana kutimuliwa kutokana na kutaka walipwe posho zao wanazodai tokea mwaka 2009 hadi leo, kwa maana ya kwamba Miaka MINNE.
Je kauli ya kwamba 'mwaka huu madai yao yamepewa kipaumbele' ina tofauti gani na ambayo bila shaka wamekuwa wakipewa kwa miaka MINNE iliyopita?
Kwa maana hiyo, kwako ni sawa kwa mtu kucheleweshewa Haki yake kwa Miaka MINNE kwa sababu tu ya Taratibu kufuatwa??
Huoni kama iwapo Taratibu zinakandamiza haki ya mtu Kulipwa chake kwa kazi aliyofanya kwa muda muafaka basi hazifai na zinapaswa kufutwa haraka iwezekanavyo??
Kwa nini hili suala la 'kufuata taratibu' linakuja pale tu linapohusu kulipa walalahoi haki zao??

Hudhani kwamba Kauli nyepesi kama hiyo ni sawa na kuwapa Waathirika hao wa Posho Zilizochelewa majibu mepesi kwa maswali magumu??
 
wananchi wa kikjiji cha cheka wanamkataa mwenyekiti wa kijiji hicho cha chemka kutokana na ubadhirifu wa kiasi cha tsh. 16 milioni na kutowasomea mapato na matumizi tangu aliposhika uongozi. sasa swala hili sisi kama wadau wa kijiji hiki hatujui ukweli wake tunasubiria wahusika ambao nipamoja na mkuu wa wilaya watufahamishe ukweli ulivo.
KAZA BUTI NOVAT KAZI UNAYO.
 
hapo ndipo ndugu zangu muelewe umuhimu wa kuwepo kwa nafasi ya mkuu wa wilaya,kukujibu,moja wao ndiyo wamesema kuwa wanadai kiasi hicho cha fedha lakini lakini lazima tupate upande wa pili wa halmashauri-kimsingi tatizo lipo lakini bado wenyeviti hao hata majukumu yao hawayafahamu walieleza wazi siku niliyokutana nao je unadhani wanaweza hata kufahamu kitu kujenga msingi wa kitu wanachodai ? kuna kanuni,sheria na taratibu za stahili hizo lakini kwa kumalizia ni kwamba taarifa hiyo haijakaa vizuri nimeingia hapa Mei ya nyuma nitayaangalia nimewaahidi wenyeviti hao kuingia katika meza ya uchambuzi nao wameomba na waheshimiwa madiwani wawepo nimewaambia hakuna kipingamizi,nilifanya hivyo hata kwa walimu,lakini kwa ufupi ni kwamba matatizo kama hayo mbele nitajitahida tatizo lisitokee.
 
mpaka taarifa ya ukaguzi ninayo kaka nipo vizuri kama mwananchi wa kijiji hicho vuta subira nimeingia hai kuna mambo kibao afadhali lenu kuna maeneo watu wanamenga maeneo ya shule na kuuza,kuna uvamizi wa vyanzo vya maji na migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na mashamba ya wawekezaji,chemka nakuja
 
Naona tabu kuamini ujumbe huu. Hivi kweli huyu mkuu wa mkoa anaweza kuwa so ignorant? Tanzania tumefika pabaya kutokana na ombwe la uongozi katika serikali. Pamoja na semina elekezi zote utendaji ndio huu? Huyu RC ni kituko. Oh God what is this???? "Mungu tusaidie tuione 2015 na utujaze hekima tuwachague viongozi wenye kukuogopa na wenye uchungu na watanzania. Amen"
 
huyo RC ni jazba alizoleta.wenye mamlaka ya kuwafuta kazi wenyeviti wa vitongoji ni wananchi waliowachagua.

jamani labda haikueleweka ingawa hapo juu niliweka kipande cha habari ya gazeti la mwananchi,RC alichosema ni kwamba kama kuna mwenyekiti anaona kwamba hawezi kushiriki katika sensa basi aandike barua
 
Naona tabu kuamini ujumbe huu. Hivi kweli huyu mkuu wa mkoa anaweza kuwa so ignorant? Tanzania tumefika pabaya kutokana na ombwe la uongozi katika serikali. Pamoja na semina elekezi zote utendaji ndio huu? Huyu RC ni kituko. Oh God what is this???? "Mungu tusaidie tuione 2015 na utujaze hekima tuwachague viongozi wenye kukuogopa na wenye uchungu na watanzania. Amen"

jamani labda haikueleweka ingawa hapo juu niliweka kipande cha habari ya gazeti la mwananchi,RC alichosema ni kwamba kama kuna mwenyekiti anaona kwamba hawezi kushiriki katika sensa basi aandike barua
 
huyo RC ni jazba alizoleta.wenye mamlaka ya kuwafuta kazi wenyeviti wa vitongoji ni wananchi waliowachagua.

jamani labda haikueleweka ingawa hapo juu niliweka kipande cha habari ya gazeti la mwananchi,RC alichosema ni kwamba kama kuna mwenyekiti anaona kwamba hawezi kushiriki katika sensa basi aandike barua
 
hapo ndipo ndugu zangu muelewe umuhimu wa kuwepo kwa nafasi ya mkuu wa wilaya,kukujibu,moja wao ndiyo wamesema kuwa wanadai kiasi hicho cha fedha lakini lakini lazima tupate upande wa pili wa halmashauri-kimsingi tatizo lipo lakini bado wenyeviti hao hata majukumu yao hawayafahamu walieleza wazi siku niliyokutana nao je unadhani wanaweza hata kufahamu kitu kujenga msingi wa kitu wanachodai ? kuna kanuni,sheria na taratibu za stahili hizo lakini kwa kumalizia ni kwamba taarifa hiyo haijakaa vizuri nimeingia hapa Mei ya nyuma nitayaangalia nimewaahidi wenyeviti hao kuingia katika meza ya uchambuzi nao wameomba na waheshimiwa madiwani wawepo nimewaambia hakuna kipingamizi,nilifanya hivyo hata kwa walimu,lakini kwa ufupi ni kwamba matatizo kama hayo mbele nitajitahida tatizo lisitokee.

Mkuu, Tunakushukuru kwa maelezo mema. Ni matumaini yetu kwamba maelezo haya yatakwenda sambamba na VITENDO kutokana na ukweli kwamba hii sio mara ya kwanza kusikia na kushuhudia Viongozi wanaoingia madarakani kwa nia njema kabisa ya kushughulikia matatizo mbalimbali yaliyo kwenye mifumo yetu lakini mwisho wa siku wakajikuta wanalazimika kujiunnga na mfumo wa wanasiasa wa 'Bora Liende'.
Ningependa kujipa matumaini kwamba kwako itakuwa tofauti kwa vile una uzoevu wa kuziona kasoro hizo na kuziandika/kuzitangaza na sasa umeingia 'jikoni' na utaweza kuzifanyia kazi.
Wasiwasi wangu hata hivyo, ni je Mwisho wa Siku utaweza kucheza Ngoma tofauti na ile aliyolipia Mpiga Zumari ??

labda kukufafanulia tu suala siyo deni hilo la nyuma bali taratibu kufuatwa,suala la fedha za vitongoji lipo kisheria kwa maana ni asilimia ishirini ya mapato ya halmashauri lazima ielekezwe vijijini hivyo kwa mwaka huu mwelekeo ni kuhakikisha kwamba fedha utaratibu unasimamiwa siyo suala la majibu rahisi ama magumu ndugu yangu

Ufafanuzi hafifu kwa hoja nzito!
 
wapo na wataendelea na kazi ya kuwaongoza makarani wa sensa kama kawaida na wameahidi kufanyakazi hiyo kufa na kupona kuhakikisha mambo yanakwenda kwa ufanisi wilayani hai

Tutoke nje ya mada,
Hii style ya kila anaetuhumiwa au kuhusishwa na jambo flani kulijibu directly hapahapa JF inatia moyo sana, na kuonyesha jinsi huyo mtu alivyo erevuka.

Yaani kuliko kuacha jambo likajadiliwa tu bila kua na conclusion yoyote, basi muhusika analijibu na kuondoa utata uliopo na kuweka mambo Sawa.

Ushauri wangu kwa mods, wale watajwa ambao mnaweza juwasiliana nao ni vyema mkawa mnawafahamisha kuhusu topic inayowagusa kisha mkawasaidia kufungua ID ili wajibu direct.

Nova we ni gamba, but nimefurahishwa na kujitokeza kwako hapa, big up DC!!
 
Back
Top Bottom