Serikali yafufua mchakato ujenzi Bandari ya Bagamoyo

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
618
1659703546437.png

SERIKALI imeanza mchakato wa kutafuta mwekezaji mpya kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo baada ya mazungumzo na mwekezaji wa awali kutokufikiwa mwafaka na hatimaye kujitoa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, alisema hayo jana alipoulizwa swali na waandishi wa habari kuhusiana na hatua ambayo serikali imefikia katika mpango wake wa kuanza ujenzi wa bandari hiyo.

“Bandari ya Bangamoyo ni kweli muda mrefu tumeizungumza na tulikuwa tunaenda vizuri na baadhi ya watu lakini sasa hivi inaonekana yale mazungumzo hayakwenda vizuri. Mwenyewe ameamua hatoendelea kuwekeza huko,” alisema Prof. Mbarawa.

Pia alisema hata baada ya mazungumzo na mwekezaji wa awali kuvunjika, nia ya serikali ya kujenga bandari hiyo iko pale pale.

“Nia ya serikali iko pale pale kwa sababu tunajua bandari hii ya Dar es Salaam inaanza kufika mahali inashindwa uwezo wake na bandari itakayotuokoa ni hii ya Bagamoyo. Kwa hiyo hilo la serikali tunalijua na tutahakikisha tunalisimamia ili tuijenge haraka iwezekanavyo.

“Katika mpango huu, naamini tutapata wawekezaji wengine wazuri na wenye uwezo wa kujenga bandari hii ya Bagamoyo,” alisema Mbarawa.

Wakati wa Bunge la Bajeti lililomalizika Juni 30, mwaka huu, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka 2022/23, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, alisema katika kipindi cha mwaka 2021/22, serikali ilifufua majadiliano ya mradi wa Bandari na Kanda Maalum ya Bagamoyo (BSEZ) uliosimama tangu mwaka 2018.

Alisem wizara yake ndiyo ilikuwa inaratibu uendelezaji wa BSEZ unaolenga kuendana na ushindani wa biashara za usafiri wa majini pamoja na kuunganisha shughuli zingine za kiuchumi ikiwamo viwanda na utalii.

Dk. Kijaji alisema wizara hiyo ilifufua majadiliano na wawekezaji ambao ni Merchants Holdings (International) Co. Ltd (CMHI) ya China na Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman (OIA) ambayo awali ilikuwa inaitwa Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Oman (SGRF).

Kwa mujibu wa Kijaji, majadiliano hayo yalihusu eneo dogo la mradi wa BSEZ kwa kuendeleza eneo la hekta 3,087 kati ya hekta 9,887 ambapo unahusisha ujenzi wa bandari.

Pia alisema mpango huo ulihusisha ujenzi wa kituo cha usafirishaji kwenye eneo la hekta 887 na uendelezaji wa eneo maalum la viwanda kwenye eneo la hekta 2,200.

Chanzo: IPP MEDIA
 
Marekani na Ufaransa zilionesha Nia ya kuwekeza,komaeni na hao..

Kilichomtoa Mchina hapo itakuwa ni kubadilika kwa terms of contract sio kingine.
Marekani na Ufaransa walionesha interest kwenye kushauri

Ila baada ya hali kubadilika sana duniani ambapo Urusi na China wanaongeza ushawishi Afrika jambo hili limemfanya Marekani aanze kubadili sera zake hasa kiuchumi towards Afrika.

Hili linaweza kumfanya Mmarekani kuja kuwekeza Bandari ya Bagamoyo as kwa mchina haitawezekana tena maana alivoanza kuona danadana kwetu alienda kuwekeza bandari ya Lamu Kenya
 
Marekani nao ni hopeless, hawawezi kuwekeza hapo, unless kama mnawapa military base na uranium, they are equally wachenzi kama China
 
Mchina kajenga bandari ya Lamu Kenya. Nguvu nyingi anapeleka bandari ya Lamu Kenya.

Kuja kujenga tenda Bandari Bagamoyo wakati ameshajenga hapo Lamu tu kwake kibiashara haina afya
Ni wawekezaji wawili tofauti. Hata hivyo kilichokwamisha ni masharti ya mkataba kwa kuwa huo ujenzi wa lamu port haijaanza baada ya ya kwetu kushindikana. Umeanza kabla hata ya mazungumzo ya hii ya bagamoyo.

Kwa masharti yale mama Samia asingeweza kukubali. Ni kitanzi kile
 
Marekani na Ufaransa walionesha interest kwenye kushauri

Ila baada ya hali kubadilika sana duniani ambapo Urusi na China wanaongeza ushawishi Afrika jambo hili limemfanya Marekani aanze kubadili sera zake hasa kiuchumi towards Afrika.

Hili linaweza kumfanya Mmarekani kuja kuwekeza Bandari ya Bagamoyo as kwa mchina haitawezekana tena maana alivoanza kuona danadana kwetu alienda kuwekeza bandari ya Lamu Kenya
Uache uongo, Marekani hawezi kuwekeza bandari ya bagamoyo na hiyo nia haipo.

Sana sana hapo ni kuwabembeleza hao wa- OMAN
 
Marekani nao ni hopeless, hawawezi kuwekeza hapo, unless kama mnawapa military base na uranium, they are equally wachenzi kama China
Marekani hawezi kuwekeza kwenye bandari tena hasa ya hivyo, never. Na hajawahi kufanya hivyo, kipo special kimfanye awekeze Bagamoyo? Watu humu hawajui chochote ni waropokaji.

Hapo ni kurudi tu mezani na wa-oman
 
Ni Rasmi Mkataba Huo ni Kichaa pekee angekubali masharti yale .

Kufufuliwa kwa mazungumzo yale Vijana wengi ambao hata Mkataba awajawahi kuuona walidai JPM alikataa mradi kwa roho mbaya

Leo Hii Vichwa Chini Yuko wapi Yule Ngoswe Wa Kigoma Mchumba wa Serikali ya Kule Zenji na Kiongozi Mkuu wa zambarau?? alidai Tumejikosesha uchumi wakati hata mkataba ajawahi utia machoni
 
Marekani hawezi kuwekeza kwenye bandari tena hasa ya hivyo, never. Na hajawahi kufanya hivyo, kipo special kimfanye awekeze Bagamoyo? Watu humu hawajui chochote ni waropokaji.

Hapo ni kurudi tu mezani na wa-oman

Hata Oman sidhani…

Kumbuka Beira kuna Ujezi , Lamu same…

Niamini hii bandari yapasa kuiweka Pending Tupambane kwanza na Sgr , Mchuchuma

Tuongeze Nguvu Mtwara , Dar , Tanga Lindi

Hii Bandari ya Bagamoyo ilikua inaenda kutuuza mazima tumshukuru Mungu kwa kila jambo.
 
Biden kaandaa kikao na viongozi wa Afrika. Nadhani kitafanyika siku si nyingi sana.

Tuombe uzima tusikie jinsi Marekani atakavyotangaza mabadiliko ya Sera yake kwa Afrika. Wabashiri wanadai sasa Marekani ataanza uwekezaji mkubwa Afrika kama anavyofanya China. Tusubiri tuone
 
Hata Oman sidhani…

Kumbuka Beira kuna Ujezi , Lamu same…

Niamini hii bandari yapasa kuiweka Pending Tupambane kwanza na Sgr , Mchuchuma

Tuongeze Nguvu Mtwara , Dar , Tanga Lindi

Hii Bandari ya Bagamoyo ilikua inaenda kutuuza mazima tumshukuru Mungu kwa kila jambo.
Jarida la The African Report lilishaandika haya na kuelezea jinsi itakavyokuwa vigumu kwa Tanzania kuwashawishi tena Wachina kujenga Bandari Bagamoyo wakati China tayari amesha invest heavily kwenye Bandari ya Lamu hapo Kenya na Beira Msumbiji

Vyovyote vile ilikuwa ngumu sana China kufanya commitments kwenye Bandari zote hizo as kiuchumi lazima ingemletea hasara

Sasa tunachotakiwa kufanya Tanzania ni kupata mwekezaji ambaye sio mchina atakaye compete na mchina kwenye kanda hii
 
Back
Top Bottom