Serikali yaelezea kusononeka kwa kuzomewa na wananchi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Posted Date::10/11/2007
Serikali yaelezea kusononeka kwa kuzomewa na wananchi
Beatrice Charles
Mwananchi

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru, amesema tabia ya wananchi kuwazomea viongozi wa serikali kutokana na tuhuma za ufisadi sio haki.

Akizungumza na viongozi wa serikali za mitaa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke juzi, Ngombale-Mwiru alisema wananchi wanatakiwa kusubiri uamuzi wa vyombo vinavyoshughulikia tuhuma hizo.

Ngombale-Mwiru alisema, mtu au kiongozi anayetuhumiwa kwa rushwa atashugulikiwa na taasisi husika na iwapo atabainika kuwa kuhusika na ufisadi, sheria itachukua mkondo wake.

Kinachotakiwa kufanywa ni uchunguzi wa kina, kama mtu atabainika kupokea au kutoa rushwa, vyombo vya sheria vitashughulikia,? alisema.

Alisema mawaziri wanaofanya ziara mikoani, wamekwenda kwa ajili ya kutekeleza ilani ya CCM ya kuboresha elimu, miundombinu, kilimo, afya na maji sio kuwatangaza mafisadi.

Waziri Kingunge alisema, wapinzani wamepotea kwa kutilia shaka viongozi wa serikali kwamba wamekula rushwa bila kuwa na ushahidi.

Jitihada ambazo wanazifanya wapinzani ni kulaumu viongozi na kukichafua chama tawala na serikali yake kwa wananchi bila ya kufanya uchunguzi,aliongeza.
 
Taratibu....

serikali imeanza kutoka kwenye mikataba mibovu, ubadhirifu BOT na matumizi yasiyoeleweka ya ikulu na sasa wanataka issue ya rushwa peke yake ndiyo ijadiliwe.......

hii propaganda itamshinda Kingunge na I cant wait siku akipata stroke or something like that (haya ni maoni yangu binafsi)...
 
Na bado, wataendelea kuzomewa, tena ni bora kama angekaa kimya huyo mzee wa watu anafikiria bado tuko kwenye enzi za chama kimeshika hatam.

Wananchi nawapongeza sana kwa sababu hiyo ndio njia itakayowafahamisha kuwa makosa yao hayawezi vumiliwa tena,
 
Kuzomewa tu haitoshi....wafukuzwe kazi (kwa kutowapigia tena kura) kabisa!!! Sisi si ndio waajiri wao...sasa kama haturidhishwi na utendaji wao wa kazi miaka nenda miaka rudi sijui kwa nini tunawaendekeza?
 
Taratibu....

serikali imeanza kutoka kwenye mikataba mibovu, ubadhirifu BOT na matumizi yasiyoeleweka ya ikulu na sasa wanataka issue ya rushwa peke yake ndiyo ijadiliwe.......

hii propaganda itamshinda Kingunge na I cant wait siku akipata stroke or something like that (haya ni maoni yangu binafsi)...

mzee wa watu alisomea analogy halafu anadhani digital itaaply yenyewe. zamani wazee wetu walikuwa wanajenga ujamaa walihitaji jamii ya ngombare ila kizazi chetu sisi hakihitaji propaganda maana tunajua kutumia macho na akili zetu vyema.

Je mnakumbuka maneno ya nyerere alisema kuwa mtu mbabe akiwa anafanya mambo ya ovyo, dawa yake ni kumzomea. nadhani watanzania wanamuenzi baba wa taifa kuliko serikali
 
watanzania tumepata silaha kwa hawa viongozi vibaka kuwazomea tu, na napendekeza neno fisadi liongezwe wakati wa kuzomea ili wafahamu kwamba sisi walipa kodi ambao tunawafanya waishi maisha ya kifahari haturidhiki na yale wanayoyafanya.

Si mnaona jinsi wanavyoweweseka.
 
Kwa nini Mzee wewe umeng'ang'ania kusema Rushwa wakati hoja yenyewe ni UFISADI.

Rushwa na UFISADI ni mambo mawili Tofauti kabisa, Ufisadi ni Uoza wa juu kabisa wa viongozi wa kitaifa.

UFISADI ni mithili ya ukuta katika nyumba.Rushwa ni kama Tofari katika ukuta. Ukuta haujengwi kwa tofari pekee yake kuna Mortar, Kuna Lipu, kuna Nilu, kuna rangi au waweza kuwa na vikorombwezo vingine kutoka na aina ya ukuta.

Toka lini Ukuta ukaitwa Tofari? Rushwa na ufisadi havina maana moja.

Kwa taarifa yako mzee kingunnge kupotosha maana kwa makusudi kwa nia ya kudhoofisha hoja kwa kutumia wadhifa wako kama waziri ndani ya serikali ili kulinda Maslahi ya watuhumiwa wa UFISADI na chama cha SISIEMU nao pia ni UFISADI.

Mzee Kingunge iko siku sisi wajukuu zako tutakulazimisha kumeza maneno yako.
 
kingunge atakuja chini kwenye historia kama kiongozi MSALITI..amesaliti FIKRA na MISIMAMO ya KIJAMAA ya mwalimu NYERERE ..kama mwalimu angeamka leo akamkuta kingunge angekufa mara ya pili kwa mshtuko..hakumjua kingunge bepari..alimjua kama kijana machachari mjamaa na mfuasi wake wa kweli ...aliyeona na kumuamuru mkapa amfanye mshauri wake mkuu...akiamini atamshauri vema kwenye misingi ya UTU ya kijamaa..lakinio mwe ..kingunge huyu huyu...

hakuishia hapo kingunge alipoona mkapa muda unaisha na bado ana tamaa ya kubakia IKULU akaamua kumsaliti tena MKAPA ..na taratibu akaaza kudandia project ya BOYZ 11 MEN TWO:....mkapa kushtuka too late mshauri wake mkuu kumbe ndie alikua kinara wa kumleta kikwete..akabaki hana muhimili...ikabidi kiulaini akubali nchi apewe kikwete tena kwa expense ya kuwachafua kina salim ....lakini mkapa kakabaki na majozi makubwa moyoni ya kusalityiwa na mshauri wake...kumbe hata mipango waliyokuwa wakishauiriana ilikuwa ikitumika na wanamtandao...

sasa tumuite nani huyu KINGUNGE NGOMBALE MWIRU ..jina linalomfaa ni MSALITI!!!!
 
Kuna mtu kule juu kasema hawezi kusubiri siku Kingunge atakapo "chabangwa" na stroke......mie naongezea kwamba labda hiyo ndio itakuwa tiketi yake kwenda kwa retirement, Kingunge tumekuchoka nenda kajiunge na wazee wenzako huko kwenye Retirement center au Nursing homes za kibongo.....utafia kwenye ofisi, huna jipya kwani ubongo wako umechoka. Kwa kizazi hiki wewe ni no match, we're BIGGER than hizo rhetoric zako za kizamani, hata huko China ulipojifunzia hawazitumii tena!!!!!!!!!. Unajiahibisha bure kizee wewe,achana na serikali...GO HOME!!!!
 
kingunge atakuja chini kwenye historia kama kiongozi MSALITI..amesaliti FIKRA na MISIMAMO ya KIJAMAA ya mwalimu NYERERE ..kama mwalimu angeamka leo akamkuta kingunge angekufa mara ya pili kwa mshtuko..hakumjua kingunge bepari..alimjua kama kijana machachari mjamaa na mfuasi wake wa kweli ...aliyeona na kumuamuru mkapa amfanye mshauri wake mkuu...akiamini atamshauri vema kwenye misingi ya UTU ya kijamaa..lakinio mwe ..kingunge huyu huyu...

hakuishia hapo kingunge alipoona mkapa muda unaisha na bado ana tamaa ya kubakia IKULU akaamua kumsaliti tena MKAPA ..na taratibu akaaza kudandia project ya BOYZ 11 MEN TWO:....mkapa kushtuka too late mshauri wake mkuu kumbe ndie alikua kinara wa kumleta kikwete..akabaki hana muhimili...ikabidi kiulaini akubali nchi apewe kikwete tena kwa expense ya kuwachafua kina salim ....lakini mkapa kakabaki na majozi makubwa moyoni ya kusalityiwa na mshauri wake...kumbe hata mipango waliyokuwa wakishauiriana ilikuwa ikitumika na wanamtandao...

sasa tumuite nani huyu KINGUNGE NGOMBALE MWIRU ..jina linalomfaa ni MSALITI!!!!
jina safi kingunge ni mchawi kikwete alali bila kuongea au kumuona au kutaja jina la kingunge ng'ombaaari weruuuu
 
Haka kazee kananitia sana kichefuchefu,eti tunatekeleza ilani ya ccm,huu ni upumbavu tu,i really hate this shi.t called ilani ya chama.Mbona awali walisema hawazomewi,au ndo kupingana kwa kauli.
Wito wangu,Pambana na Kingunge,pambana na EL,pambana na JK,pambana na RA,pambana na CCM,pambana na mafisadi,tukishinda hii vita,Tanzania will have a new history.
 
Ama kweli silaha ya mnyonge ni kuzomea. Sasa wananchi wameshajua hili la kuzomea linawakosesha raha, basi itakuwa kama kazi mpaka wabadili mwelekeo kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania na sio kuendekeza usanii ambao unaliacha nyuma taifa letu.
 
Posted Date::10/11/2007
Serikali yaelezea kusononeka kwa kuzomewa na wananchi
Beatrice Charles
Mwananchi

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru, amesema tabia ya wananchi kuwazomea viongozi wa serikali kutokana na tuhuma za ufisadi sio haki.

Akizungumza na viongozi wa serikali za mitaa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke juzi, Ngombale-Mwiru alisema wananchi wanatakiwa kusubiri uamuzi wa vyombo vinavyoshughulikia tuhuma hizo.

Ngombale-Mwiru alisema, mtu au kiongozi anayetuhumiwa kwa rushwa atashugulikiwa na taasisi husika na iwapo atabainika kuwa kuhusika na ufisadi, sheria itachukua mkondo wake.

Kinachotakiwa kufanywa ni uchunguzi wa kina, kama mtu atabainika kupokea au kutoa rushwa, vyombo vya sheria vitashughulikia,? alisema.

Alisema mawaziri wanaofanya ziara mikoani, wamekwenda kwa ajili ya kutekeleza ilani ya CCM ya kuboresha elimu, miundombinu, kilimo, afya na maji sio kuwatangaza mafisadi.

Waziri Kingunge alisema, wapinzani wamepotea kwa kutilia shaka viongozi wa serikali kwamba wamekula rushwa bila kuwa na ushahidi.

Jitihada ambazo wanazifanya wapinzani ni kulaumu viongozi na kukichafua chama tawala na serikali yake kwa wananchi bila ya kufanya uchunguzi,aliongeza.

Wmeenda kutimiza ilani ya ccm kwa gharama ya nani? hiyo miundombinu na elimu na bla bla zinatekelezwa kwa wao kuzurura nchi nzima wakila kodi zetu? Nonsense kingunge huna jipya
 
Dawa kumbe ni kuwazomea tu viongozi wote wabovu, waizi, mafisadi, na wasiokuwa na uwezo wa uongozi,

Kwenye hilo ninaungana na wanaowazomea viongozi wapuuzi!
 
No! Dawa ni kutowachagua tena na tena na tena.

Nani atawachagua tena hawa mafisadi wala rushwa! watatumia vyombo vya dola kuwashinikiza wananchi na hatimaye kuiba kura na kurudi tena madarakani
 
Je mnakumbuka maneno ya nyerere alisema kuwa mtu mbabe akiwa anafanya mambo ya ovyo, dawa yake ni kumzomea. nadhani watanzania wanamuenzi baba wa taifa kuliko serikali

..ukizomewa lazima ujiulize, umefanya nini?

..tena inabidi utafute faragha halafu uchemshe bongo!

..unaweza kuta umejinyea !

..inahitaji busara!
 
Nani atawachagua tena hawa mafisadi wala rushwa! watatumia vyombo vya dola kuwashinikiza wananchi na hatimaye kuiba kura na kurudi tena madarakani

..wananchi huwa hawashinikizwi mkuu!

..wanawachagua kwa kupenda wenyewe!sasa,ujiulize wanakuwa wamelogwa?

..it's a phenomena in itself!
 
Back
Top Bottom