Serikali yaelezea kusononeka kwa kuzomewa na wananchi

Inawezekana pia wanashinikizwa na propaganda za serikali kwa kuwatishia kutokuwaletea maendeleo. Tuna mifano mingi tu ambayo maeneo yaliyo na viongozi wengi kutoka kambi zinazotofautiana na CCM (wabunge/madiwani), wananchi wake huwa wananyanyapaliwa na serikali kwa kauli kama 'waambie wapinzani wawaletee maendelea.'

Na kuna kama ile kampeni ya muungwana -2005,'mafiga matatu', ile ilikuwa inashinikiza kiaina, kwamba ukichagua ni lazima uchague wote watau (raisi, mbunge na diwani), pamoja na kuwa maeneo mengine wabunge waliopendekezwa na CCM (Rita mlaki, Jackson Makweta, Mzindaka et el)wanachi hawakuwataka, JK aliwapigania ili wakubalike kwa wananchi.Sina uhakika mchango wao ukoje kwa hao wananchi, au labda bado wanaendekeza 'bifu'.

Cha muhimu pia ni kuwaambia wananchi ile dhana kuwa serikali italeta maendeleo wakati wao wamekaa wanapiga porojo ni kiini macho, watakapo anza kujitafutia maendeleo wao wenyewe hapo kutakuwa na mabadiliko ya kweli.
 
Nafikiri maneno mawili tu yanaweza kusaidia viongozi wabovu kurudisha heshima ya nchi nayo ni

1. FISADI
2. Kasungura


Haya maneno mawili yakitumika vizuri katika kuwazomea tutaweza kujenga tanzania yenye neema.
 
Kwa nini Mzee wewe umeng'ang'ania kusema Rushwa wakati hoja yenyewe ni UFISADI.

Rushwa na UFISADI ni mambo mawili Tofauti kabisa, Ufisadi ni Uoza wa juu kabisa wa viongozi wa kitaifa.

UFISADI ni mithili ya ukuta katika nyumba.Rushwa ni kama Tofari katika ukuta. Ukuta haujengwi kwa tofari pekee yake kuna Mortar, Kuna Lipu, kuna Nilu, kuna rangi au waweza kuwa na vikorombwezo vingine kutoka na aina ya ukuta.

Toka lini Ukuta ukaitwa Tofari? Rushwa na ufisadi havina maana moja.

Kwa taarifa yako mzee kingunnge kupotosha maana kwa makusudi kwa nia ya kudhoofisha hoja kwa kutumia wadhifa wako kama waziri ndani ya serikali ili kulinda Maslahi ya watuhumiwa wa UFISADI na chama cha SISIEMU nao pia ni UFISADI.

Mzee Kingunge iko siku sisi wajukuu zako tutakulazimisha kumeza maneno yako.
Anayameza now
 
Back
Top Bottom