BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,889
Posted Date::10/11/2007
Serikali yaelezea kusononeka kwa kuzomewa na wananchi
Beatrice Charles
Mwananchi
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru, amesema tabia ya wananchi kuwazomea viongozi wa serikali kutokana na tuhuma za ufisadi sio haki.
Akizungumza na viongozi wa serikali za mitaa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke juzi, Ngombale-Mwiru alisema wananchi wanatakiwa kusubiri uamuzi wa vyombo vinavyoshughulikia tuhuma hizo.
Ngombale-Mwiru alisema, mtu au kiongozi anayetuhumiwa kwa rushwa atashugulikiwa na taasisi husika na iwapo atabainika kuwa kuhusika na ufisadi, sheria itachukua mkondo wake.
Kinachotakiwa kufanywa ni uchunguzi wa kina, kama mtu atabainika kupokea au kutoa rushwa, vyombo vya sheria vitashughulikia,? alisema.
Alisema mawaziri wanaofanya ziara mikoani, wamekwenda kwa ajili ya kutekeleza ilani ya CCM ya kuboresha elimu, miundombinu, kilimo, afya na maji sio kuwatangaza mafisadi.
Waziri Kingunge alisema, wapinzani wamepotea kwa kutilia shaka viongozi wa serikali kwamba wamekula rushwa bila kuwa na ushahidi.
Jitihada ambazo wanazifanya wapinzani ni kulaumu viongozi na kukichafua chama tawala na serikali yake kwa wananchi bila ya kufanya uchunguzi,aliongeza.