Serikali yadang’anya walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yadang’anya walimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 28, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,210
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Serikali yadang'anya walimu

  na Mwandishi wetu
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kuanza kulipa madeni ya walimu kuanzia Desemba mwaka huu kama ilivyoahidi, Tanzania Daima Jumatano imebaini.
  Endapo serikali itashindwa kulipa madeni hayo hadi Desemba 31, mwaka huu, walimu wametishia kuitisha mgomo nchi nzima hadi walipwe madai yao.

  Hadi sasa walimu wanaidai serikali zaidi ya sh bilioni 48 ambazo iliahidi kuanza kuzilipa kwa awamu, na kwa kuanzia, mwezi huu iliahidi kulipa sh bilioni 20.
  Ahadi hiyo imekuwa ikitolewa kwa nyakati tofauti na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo na hivi karibuni aliifafanua tena wakati wa mahafali ya 47 ya Chuo cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), ambapo wahitimu wengi ni walimu.

  Katika mahafali hayo, Waziri Mulugo alisisitiza kuwa kuanzia Desemba, serikali itakuwa imelipa sh bilioni 20 kati ya 48, sawa na asilimia 44, inazodaiwa na walimu na sh bilioni 28 sawa na asilimia 56, zitalipwa mapema mwakani.

  Kwa mujibu wa naibu waziri huyo, malipo hayo yangeingizwa kwenye mishahara wa walimu hao Desemba mwaka huu.

  Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa ahadi hiyo ni sawa na changa la macho kwani hakuna mwalimu aliyeanza kulipwa kama ilivyoahidiwa na serikali.

  Baadhi ya walimu waliozungumza na gazeti hili, walisema hawakuona nyongeza yoyote ya fedha kwenye akaunti zao kama walivyoahidiwa.

  "Nilimsikia naibu waziri akikaririwa mara mbili kwamba madeni ya walimu yanaanza kulipwa mwezi huu. Hadi sasa hakuna aliyelipwa," alisema mwalimu mmoja wa jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu jana, Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT), Gratian Mukoba, alisema serikali imeamua kuwachezea walimu mithili ya watoto wadogo.
  "Alisema kila wakati imekuwa ikiahidi inalipa, lakini hailipi. Kwa mfano walituambia wataanza kutulipa Novemba, ilipofika wakahamisha deni hadi Desemba, nayo hakuna kitu. Kwanini watuchezee wakati hizo ni hela zetu?" alihoji Mukoba.

  Kwa mujibu wa Mukoba ambaye hakupenda kutoa msimamo wa CWT, alisema kuwa siku chache zijazo, watatoa msimamo mzito dhidi ya Serikali kwani hawaoni sababu za kudang'anywa kama watoto.

  "Kwanza hela tunazodai ni zetu, zilitokana na makosa yao wakati wa kulipa mishahara maana kama ulitakiwa kulipwa sh 10,000 wao walikuwa wanalipa sh 1,000. Sawa wamehakiki, wameona walikosea, wanachopaswa kufanya ni kuturudishia fedha zetu na si kuhamisha deni kila wakati," alisema Mukoba.

  Vyanzo vyetu vya habari kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi, vilirejea kauli ya mara kwa mara ya hivi karibuni kuwa serikali haina fedha kiasi cha kushindwa kulipa mishahara kwa wakati.

  Habari zaidi zinasema kuwa serikali haina fedha kwani hadi sasa imeshindwa hata kulipa ruzuku ya vyama, kikiwamo Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuvifanya vishindwe kuendesha shughuli zao.
  Kabla ya Waziri Mulugo kutangaza tarehe ya kuanza kulipa madeni ya walimu, CWT ilikutana na serikali na kukubaliana kuanza kulipa madeni hayo wakati wowote.

  Wakati walimu wakicharuka walipwe madeni yao, kwa upande wake serikali iko taabani kifedha kwani haina uwezo wa kuajiri watumishi wapya wala kupandisha vyeo wale waliopo.

  Kutokana na ukata huo, tayari imeagiza ajira zote serikalini katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 zipunguzwe kwa asilimia 50. Vilevile upandishaji vyeo upunguzwe kwa kiwango kilekile.

  Kwa hatua hii, serikali inabadilisha maamuzi ya Bunge lililoidhinisha mapato na matumizi yake Juni mwaka huu.

  Serikali imekiri kutokuwa na uwezo wa kutekeleza bajeti iliyopitishwa na Bunge, kuwa na vipaumbele tofauti na mashaka na vyanzo vyake vya mapato.
  Utekelezaji wa hatua hiyo ya serikali ulianza rasmi Novemba mwezi uliopita.

  Waraka wa serikali umesainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, Habu Mkwizu na kupelekwa kwa makatibu wakuu wote wa wizara, wakuu wa idara na taasisi zake nyingine.

  Matokeo ya uamuzi huu, waraka unaeleza: "Ni kwamba kila mwajiri sasa atalazimika kuandaa upya mahitaji yake ya ikama (taratibu za ajira na malipo) kwa kuzingatia ukomo uliorekebishwa wa bajeti uliotolewa na wizara ya fedha kwa mwaka 2011/12."

  Kila mwajiri amepelekewa jedwali la viwango vya ajira mpya, mishahara na nyongeza; na kutakiwa kufuata mkondo huo wakati wa kuwasilisha maombi mapya ya vibali vya ajira mpya kwa mwaka huu wa fedha.

  Waraka unaagiza waajiri kuweka kipaumbele katika kutenga "nafasi za kutosha kwa ajili ya wataalamu wa sekta za Elimu, Afya, Kilimo na Mifugo."

  Aidha, upungufu huo wa kifedha, umeibua hofu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo na ahadi nyingine zilizotolewa na Rais Kikwete wakati wa kampeni za urais muhula wa pili, zikiwamo ahadi za ujenzi wa barabara za ghorofa, ununuzi wa meli, viwanja vya ndege, bandari na reli.

  [​IMG]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sasa kwanini walimwamini hata mtu nwenye degree faki aisee
   
 3. n

  nyangasese Senior Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wangekua ni wabunge wangeshalipwa zamani.wabunge wetu ni wanafiki wakubwa wanatetea maslahi yao binafsi, si ya wapiga kura wao.Nadhani serikali imeshindwa kuongoza nchi inatengeneza mgogoro ambao hautaisha hata wakilipa hayo mabilioni kwani maelfu ya walimu wamepanda madaraja na bado hawajarekebishiwa mishahara yao zaidi ya mwaka sasa na Mwanza ndio inaongoza.Hii ni ajabu kwani rais wa nchi alikwisha tamka kua hataki tena kuona malimbikizo ya madai kwa watumishi wa umma.Je,hii ni dharau kwa kiongozi wa nchi au serikali imefilisika?
   
 4. W

  Welu JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Jamani kuweni na huruma na Serikali, juzi pesa imetumika kwenye sherehe za miaka 50 ya Tanganyika. Nasikia Richmond wamelipwa. Pia maisha kwa wabunge yamepanda. Na sasa wamepata kisingizio mafuriko! LABDA hivi waziri akisema uongo kama alivyosema Mlugo kuna hatua yoyote apasayo kuchukuliwa? Au kwa wakubwa kutamka chochote ni ruksa? Mlugo jitokeze tena kuongopa maana walimu mwawaona ni wa kuwaongopea tu. Mmeweza kwa uongo, na songeni mbele kwa utapeli. Hakika mmethubutu.
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  poleni sana walimu na CWT yenu
   
 6. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Polen.endeleen hivyo hivyo kukaa kimya mtalipwa
   
 7. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Duu!Ni maumivu tu mwaka huu,hadi tuzinduke na kuyatimua haya magamba!Mwaka 2015 mbali sana,watakuwa wameshamaliza nchi hawa!
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hivi gazeti la mbowe litaandika usahihi wa taarifa mbalimbali kuhusu serikali kweli? ni kulishana makasa tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu mpaka basi
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  zile 64 za miaka 50 zingetosha kulipa walimu na chenji ingebaki
   
 10. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yangu macho na masikio,WE WANT THE HANDSOME PRESDENT,they said
   
 11. cpt

  cpt JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  jaman c mbona hta hko ka mshahara chenyewe cha mwezi huu hatujalipwa!?
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  msipate tabu walimu, mtalipwa karibu na uchaguzi wa 2015v ili mkasimamie tena upigajin kura vizuri
   
 13. m

  mintolo jingi Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh, tatizo ni sourse au uhalali na uhalisia wa habari? jaribu kuwauliza walimu wakuthibitishie kama wamilipwa au hawajalipwa ndipo upost masaburi yako hapa.
   
 14. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  MTM unafikiri shida ni degree feki? Shida kwa upande wangu ni ufisadi ambao unitafuna serikali kama mchwa vile!!
   
 15. m

  mintolo jingi Member

  #15
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asalaleeeeee!!!!!!!!! cheap labours na wakati mwingi wananegotiate while they are hungry and serikali inakuwa imeiona future yao zaidi ya wao wanavyoiona. poooooooooooooor teachers riiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiich mps
   
 16. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hapo kuna ka-ukweli.....too bad!
   
Loading...