Serikali yadanganya kuhusu mradi wa maji korogwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yadanganya kuhusu mradi wa maji korogwe

Discussion in 'Jamii Photos' started by dalbega, Jun 25, 2012.

 1. d

  dalbega Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Aidha kwa bahati mbaya au kwa makusudi, Waziri wa Tamisemi ndugu Aggrey Mwanri aliliambia bunge kuhusu mradi wa maji wa Sakare- Bungu umeendelea kutengewa hela na serikali (Gazeti la Mwananchi tarehe 21/6/2012).

  Hizi habari sio za kweli. Toka ulipoanza mpaka sasa mradi huu umekuwa ukifadhiliwa na Shirika la World Vision kwa fedha kutoka kwa wafadhili wa Hong Kong. Hata wahandisi wa serikali wanapofanya kazi za ufuatiliaji na usimamizi wa huu mradi wamekuwa wakilipwa posho na shirika la World Vision. Hizi habari za serikali kutenga shilingi milioni 229 ni za uongo kabisa. Serikali haijawahi kutoa senti tano kwa ajili ya utekelezaji wa huu mradi. Kama hizi pesa ziliwahi kutolewa na serikali kuu ufuatiliaji ufanyike.

  Ninadhani ni vizuri kujenga tabia ya kufanya kazi na kusema ukweli. Tunazidi kurudi nyuma kimaendeleo kwa ajili ya uongo. INAKERA KWA KWELI!!!
   
 2. conveter

  conveter Senior Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  where are the photos? :noidea:
   
 3. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  peleka kule habari na hoja,
   
 4. d

  dalbega Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Sorry people. Nimefanya misposting. How can I move it to Habari na hoja? Bado mgeni kwenye JF
   
Loading...