Serikali yabadilisha gia angani; yaamua kuwakaribisha wachina kuwekeza kwenye Madini

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
kairuki..1-768x392.jpg
Serikali kupitia Wizara ya Madini, imewakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza kwenye miradi mbali mbali ya madini hapa nchini.

Wito huo ulitolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke na ujumbe alioambatana nao Wizarani hapo kutoka kwenye Ubalozi huo ili kujadiliana masuala mbalimbali ya madini ikiwemo fursa za uwekezaji.

Waziri Kairuki alisema kuwa, Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini na hivyo zipo fursa lukuki za uwekezaji ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za nchini China kwa manufaa ya pande zote mbili

“Rasilimali za madini ni nyingi na hivyo zipo fursa mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za China na wakati huo huo kuchangia katika uchumi na pato la Taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Kairuki.

Aidha alisema, yapo maeneo ambayo wawekezaji wanaweza kushirikiana na Serikali ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni uchimbaji wa madini kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), tafiti za utambuzi wa maeneo yenye madini kwa kushirikiana na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo cha Madini (MRI).

Aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha madini yanayochimbwa nchini yanaongezwa thamani kabla hayajasafirishwa ili kukuza uchumi wa Taifa na wakati huo huo, kuongeza mapato ya Serikali na kuzalisha ajira zaidi.

“Madini yakiongezwa thamani hapa nchini, faida zitakazopatikana ni nyingi na ni kubwa ikiwemo ajira lakini pia mapato nayo yataongezeka kwa kuelewa thamani halisi ya madini husika,” alisema Waziri Kairuki.

Kwa upande wake Balozi Ke alipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu na kwamba Serikali ya China itaendeleza ushirikiano wa karibu na wa dhati na Serikali ya Tanzania hususan kwenye Sekta ya Madini ili kuhakikisha sekta hiyo inaleta tija iliyokusudiwa kwa Taifa.

Alisema kampuni mahiri nyingi kutoka China tayari zimeonyesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini na ziko tayari kuja kuwekeza Nchini.

My take: Hawa wachina watakuwa waaminifu kuliko wawekezaji kutoka Ulaya? Maana wazungu tuliwaita wezi wa rasilimali
 
Wasisahau kuzingatia uzoefu wa Angola na wachina katika uwekezaji wa mafuta na madini tusije tukapotea zaidi
Serikali iingie ubia na kampuni za serikali za China kama itaonekana kampuni private za madini za China haziaminiki.China wana kampuni za serikali za madini zinazofanya vizuri waingie ubia Haya naachia wataalamu wa wizara
 
Serikali kupitia Wizara ya Madini, imewakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza kwenye miradi mbali mbali ya madini hapa nchini.

Wito huo ulitolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke na ujumbe alioambatana nao Wizarani hapo kutoka kwenye Ubalozi huo ili kujadiliana masuala mbalimbali ya madini ikiwemo fursa za uwekezaji.

Waziri Kairuki alisema kuwa, Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini na hivyo zipo fursa lukuki za uwekezaji ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za nchini China kwa manufaa ya pande zote mbili

“Rasilimali za madini ni nyingi na hivyo zipo fursa mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za China na wakati huo huo kuchangia katika uchumi na pato la Taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Kairuki.

Aidha alisema, yapo maeneo ambayo wawekezaji wanaweza kushirikiana na Serikali ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni uchimbaji wa madini kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), tafiti za utambuzi wa maeneo yenye madini kwa kushirikiana na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo cha Madini (MRI).

Aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha madini yanayochimbwa nchini yanaongezwa thamani kabla hayajasafirishwa ili kukuza uchumi wa Taifa na wakati huo huo, kuongeza mapato ya Serikali na kuzalisha ajira zaidi.

“Madini yakiongezwa thamani hapa nchini, faida zitakazopatikana ni nyingi na ni kubwa ikiwemo ajira lakini pia mapato nayo yataongezeka kwa kuelewa thamani halisi ya madini husika,” alisema Waziri Kairuki.

Kwa upande wake Balozi Ke alipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu na kwamba Serikali ya China itaendeleza ushirikiano wa karibu na wa dhati na Serikali ya Tanzania hususan kwenye Sekta ya Madini ili kuhakikisha sekta hiyo inaleta tija iliyokusudiwa kwa Taifa.

Alisema kampuni mahiri nyingi kutoka China tayari zimeonyesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini na ziko tayari kuja kuwekeza Nchini.

My take: Hawa wachina watakuwa waaminifu kuliko wawekezaji kutoka Ulaya? Maana wazungu tuliwaita wezi wa rasilimali
Sera zetu za kiuchumi na mambo ya nje ni Zing Zang.
 
Wawe waangalifu tusije kujutia baadae
Duniani kote hata Tanzania kuna matapeli na wezi cha muhimu ni kufanya due diligence sawa sawa Chinese wana watu wazuri sana ingawa wako wachache matapeli kama ilivyo Nigeria wako wazuri mfano dangote aliyowekeza sana Tanzania .Si kila mnigeria tapeli.Ni kazi pia ya balozi wa China kufanya vetting nchini kwake kuhakikisha wale wanaokuja kuwekeza Tanzania ni wawekezaji waaminifu sio matapeli watakaochafua sifa ya China. Kabla kupeleka proposal kwa waziri wetu au raisi ajiridhishe kuwa hao anaowaleta wamefanyiwa vetting na serikali ya China kuwa si matapeli wao na wafanyakazi wao watakaokuja Tanzania
 
Ushahidi please

Mkuu habari ndio hiyo, ww jikunyate ndani blanket la uzalendo academia maana siku hizi ni ngumu kutofautisha kati ya uzalendo na ujinga. Inaonekana kama mkulu anawaanini sana wachina kuliko wazungu. Lakini asikudanye mtu wazungu ni bora mara kulinganisha na wachina. Angalia ubora wa huduma za wazungu fananisha na wachina. Nenda kwenye ajira uangalie malipo ya mzungu na mchina, ukweli uko wazi. Ni kweli wazungu ni lakini wana utu kuliko wachina.
 
Ushahidi please

Mkuu habari ndio hiyo, ww jikunyate ndani blanket la uzalendo academia maana siku hizi ni ngumu kutofautisha kati ya uzalendo na ujinga. Inaonekana kama mkulu anawaanini sana wachina kuliko wazungu. Lakini asikudanye mtu wazungu ni bora mara kulinganisha na wachina. Angalia ubora wa huduma za wazungu fananisha na wachina. Nenda kwenye ajira uangalie malipo ya mzungu na mchina, ukweli uko wazi. Ni kweli wazungu ni lakini wana utu kuliko wachina.
 
Wasisahau kuzingatia uzoefu wa Angola na wachina katika uwekezaji wa mafuta na madini tusije tukapotea zaidi
.
Angala ilikua miongoni mwa nchi tajiri Afrika wakati wazungu wakiwa wawekezaji wao wakuu. Ila baada ya kuwakaribisha wachina wamekua wakirudi nyuma kwa kasi ya hatari. Wachina ni hatari ya afya ya makuzi ya chumi za nchi nyingi maana wanajifikiria wao tu.
Wakati mugabe anawafukuza wazungu China ilimwahidi kumsaidia kwa hali na mali ahadi ambayo kila uchwao ilionekana kutotekelezeka hadi Zimbabwe ilipo paralyze mazima kiuchumi na kijamii pia.
 
Mkuu habari ndio hiyo, ww jikunyate ndani blanket la uzalendo academia maana siku hizi ni ngumu kutofautisha kati ya uzalendo na ujinga. Inaonekana kama mkulu anawaanini sana wachina kuliko wazungu. Lakini asikudanye mtu wazungu ni bora mara kulinganisha na wachina. Angalia ubora wa huduma za wazungu fananisha na wachina. Nenda kwenye ajira uangalie malipo ya mzungu na mchina, ukweli uko wazi. Ni kweli wazungu ni lakini wana utu kuliko wachina.
Wazungu huwa ni walipaji wazuri kwenye mishahara ya watumishi wao na hakuna unyama unyanyasaji lakini wachina kwa watu weusi hufanywa unyama mwingi hata gereji za wachina zilizojazana Nchini kuna unyanyasaji kwa wazawa, wachina ni hatari sana kwenye viwanda vyao hakuna usawa kwa mtu mweusi ni hatari kwa uchumi kuliko wazungu.
 
Back
Top Bottom