Serikali yabadilisha gia angani; yaamua kuwakaribisha wachina kuwekeza kwenye Madini

Wachina wachache sana wanaongea kingereza wengi ni ali baba

Kwa hiyo ndio maana wanaajiri sana wachina wenzao sababu supervision lazima ifanywe na wachina wenzao na haohao wachina wenzao napo hawajui kiingereza kwa hiyo inawalazimu sasa nao waajiri wachina zaidi kwa sababu ya Language barrier.

Ila ukirudi kwa wazungu wengi wao wanajua kiingerza licha ya kutokutokea katika nchi zisizo za kiingereza kwa hiyo inakuwa rahisi sana kuwaajiri watanzania wengi sababu hakuna language barrier tena
 
Serikali iingie ubia na kampuni za serikali za China kama itaonekana kampuni private za madini za China haziaminiki.China wana kampuni za serikali za madini zinazofanya vizuri waingie ubia Haya naachia wataalamu wa wizara
kwani hiyo mikataba mibovu iliyopita walioingia ubia walikuwa wananchi wa kawaida au ni hao hao mnaowaita wataalamu wa wizara
 
Unajua kuna mtazamo kwamba wachina ni wazuri kuliko wazungu! Huu mtazamo ni kosa kubwa mno. Wachina wana njaa ya mali kuliko hata wazungu. Wachina wapo 1/3 ya idadi watu duniani. Kuwalisha watu takribani bilioni 2+ siyo kazi ndogo. Twendeni tukajifunze Zambia jinsi wachina wanavyowafanya wazambia vibaya kwenye copper.

Kama tukiwaruhusu wawekeze kwenye madini, ni vyema twende na mtazamo kama wa Botswana, na mtazamo wa kutowachukulia wachina kama wazuri kuliko wazungu. Lazima sheria na mikataba yetu iwe imara na inayoweka maslahi ya nchi mbele. La sivyo, wajukuu zetu watakojolea makaburi yetu.
Hii hofu juu ya wajukuu zetu kila mtu angekuwa nayo, leo tusingekuwa hapa. Kama tutaacha ubinafsi wa kujali leo yetu tu, hakika tutapiga hatua.

Tumeshazikwa hai tayari, dhambi yetu kubwa itakuwa kutowapa tumaini wale wajao la kutopitia yale yetu leo.

Laa! Mito ya damu itawamwagika wakikojolea makaburi yetu na kulaani.

Anaita sasa!
 
Wasikieni Wachina tu. Ni wezi wakubwa. Wengi wanajifanya hawajui Kiswahili kumbe ni janja ya kukwepa kuhojiwa.
 
Huyu Waziri anawafahamu Wachina?
1) China ina teknolojia ya chini sana kwenye sekta ya uchimbaji madini
2) China ina teknolojia duni sana na kwa ujumla hawajui kufanya utafiti wa madini ( walijaribu kule Tanga wakasema kuna dhahabu 7m ounces, alipoletwa mtafiti wa kujitegemea anayetambulika, ikadhihirika kuna 0.75m ounces)
3) Migodi yote yenye uzalishaji mkubwa wa dhahabu nchini China ni ile inayomilikiwa kwa ubia na makampuni ya Canada, Australia na USA
4) Migodi inayomilikiwa na Wachina pekee yao nchini China ndiyo inayoongoza kwa ajali Duniani, na uzalishaji mdogo
5) Kwa ujumla, kwa Dunia nzima, makampuni ya China ukilinganisha na ya Ulaya, America na Australia, ndiyo yananyoongoza kufanya kazi bila kuzingatia sheria (ukwepaji kodi, utendaji kazi usiozingatia ubora wa viwango au huduma, mistreatment ya wafanyakazi, ukosefu wa usalama kazini, mishahara duni, n.k.).

Kwa ujumla uwezo wa kitaalam katika utafiti na uchimbaji madinj kati ya wataalam Wachina na Watanzania, watanzania wapo mbali maradufu ya Wachina.

We are not better by chasing away Americans and Australians, and inviting Chinese. We are moving for the worst.
 
Hawa si ndio wamemaliza pembe ndovu wetu..?? Na tena tukanisikia zilisepa ndani ya air force ya kichina
 
Ni heri tupate mkoloni Mpya mzungu tumemchoka amekaaa na sisi miaka hatujaendelea wacha tumpe nafasi mkoloni mchina naye tuone.mzungu tumekaa naye toka 1884 wakati wa mkutano wa ukoloni wa kugawana Africa Berlin hadi leo we are nowhere .Chinese you are warmly welcome
Unajua Nyumba za wakuu wa mikoa yote Tanzania zimejengwa na wakina nani, ??

Primary road network ya Tanzania imejengwa na wakina nani ?

Reli ya kati imejengwa na wakina nani ???...


Ikulu ya Raisi imejengwa na wachina ??!


Hivi unajua miradi mingi ya afya ( ukimwi ) ni ya wazungu ?????


Hivi unajua taasisi nyingi za mambo ya kijamii kusaidia Watoto,wanawake na masikini ni ya wazungu ????? Kwa mfano IRC, PLAN international, Norwegian Church, We Care For Africa , Jhpiego, Save the children, I-Cap n.k


Unajua Hata ARVs mnapewa na wazungu ????


Unajua hata ruling system yA Tanzania tumeiga kwa wazungu na sio wachina ??? You know why ???



Unalijua shirika moja linaitwa DFID????? Ni la waingereza .... Kawaulize watanzania wanaofanya kazi shirika hili ndio utaacha kumlinganisha mzungu na vitu vya hovyo (wachina)
 
Kairuki kanenepa ile wizara imezidi kumpendeza baada ya unene huo kuanza kipindi yupo ikulu

"Kanenepa sasa kandiii....shime chakula changuu"
Hongera Magu kwa kumpa Kairuki shavu naona kakolea kwelikweli! Hakika kaula!
 
Back
Top Bottom