Serikali yabadili muundo wa vyeti vya kuzaliwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yabadili muundo wa vyeti vya kuzaliwa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Jun 23, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Na Felix Mwagara


  WAKALA wa Serikali wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), katika kupambana na udanganyifu wa vyeti vya kuzaliwa nchini umeanza kutoa vyeti vipya vya kuzaliwa vyenye alama maalum za usalama.


  Vyeti hivyo vinavyotengenezwa kwa kutumia kompyuta, vimeanza kutolewa wiki iliyopita katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.


  Akizungumza a mwandishi wa habari hii jana, Afisa Usajili Msaidizi wa Rita, Joseph Mwakatobe alisema kumekuwa na udanganyifu mkubwa sana wakati wanakuwa wanavihakiki vyeti vingi katika ofisi zao ndio maana wameamua kuvifanyia mabadiliko katika utaalum maalum ili mtu yoyote asiweze kufanya udanganyifu wa vyeti hivyo.


  “Tumeanza kufanya mabadiliko kwenye vyeti vya kuzaliwa na kwa kuanzia tuliona vema kuanza kutoa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na sambamba na ofisi ya Makao Makuu ambayo nayo imeanza kutoa”, alisema Mwakatobe.


  Alisema vyeti vipya vina mvuto wa pekee kutokana na karatasi iliyotumika kuwa nzuri na tofauti kabisa na ile ya zamani na kwamba pia vina alama za kiusalama ambayo inawasaidia kutambua kama cheti ni sahihi ama siyo na kwamba vinatengenezwa kwa kompyuta tofauti na vile vya zamani ambavyo vilikuwa vinatengenezwa kwa kuchapa kwenye mashine.


  Mwakatobe alisema pamoja na kuanza kuvitoa katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ofisi yake bado haijaanza katika mikoa mingine, ingawa inatarajia kuendelkea katika mikoa ya Pwani na Tanga.


  Alipoulizwa kuhusu wenye vyeti vya zamani kutambulika kwao, Mwakatobe alisema vyeti vya zamani vitaendelea kutumika na itakapohitajika kila mtu awe na cheti kipya basi serikali itatangaza.


  “Kwasasa vile vyeti vya zamani vitaendelea kutumika kama kawaida, itakapofikia muda wa kila Mwananchi awe na cheti kipya na kile cha zamani kisitumike , wananchi watajulishwa” alisema Mwakatobe.


  Aidha, Yusufu Bakari mkazi wa Gongolamboto aliyekuwa anatembelea mabanda mbalimbali uwanjani hapo alipohojiwa kuhusu hatua ya Rita kubadilisha vyeti alisema serikali imefanya jambo la msingi kwa kufanya mabadiliko hayo kwani hapo mwanzo hata yeye mwenyewe alipewa cheti feki mtaani kwao.

  “Kwa hatua hiyo napenda kuipongeza serikali kwani hata mimi nilishapewa cheti feki lakini kwasasa inabidi nikitafuta hicho kipya, hii tabia ya cheti feki imezagaa mtaani hasa hapa Dar es Salaam” alisema Bakari.
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  jambo la maana kamua hivyo sema hata hivyo watu watapata dili tu hakuna kisichowezekana bongo.
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Mie pia naona kama wakubwa wanachongeana dili la tenda ya kuvitengeneza tu!
  Kama ni ufeki hata dola za kimarekani zipo feki!
  Iwe ni kweli kwa wema, siyo inatafutwa pesa ya uchaguzi!
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wangeanza na udhibiti wa vyeti vya shule na vyuo; hasa katika kuhakiki.
   
 5. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Wazo zuri japo naona ni kama kuruka majivu na kukanyaga moto!..
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwa usanii wa Watanzania wa ofisi za briefcase, sijui ni kitu gani ambacho hawawezi kughushi!!!!!?? Yaani kuna kona na chemba za ajabu na mambo ya ajabu yanafanyika huko, ni mitandao mipana!!! Anyway, let them try their luck!!! Wanaweza kuthibiti kughushi!!!! I doubt!!
   
Loading...