Serikali yaanzisha ujenzi wa vituo vya malezi ya watoto ili kukabiliana na ukatili dhidi yao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Shirika la Brac Tanzania imeanza kuratibu uanzishwaji wa Vituo vya Malezi kwa watoto wadogo vitakavyomilikiwa na kuendeshwa na Jamii ya eneo husika.
Hayo yamesemwa jijini Dar E s Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Mwajuma Magwiza wakati akikagua Maendeleo ya uanzishwaji wa vituo hivyo kwa Halmashauri za Wilaya ya Temeke na Kigamboni
vinavyojengwa kwa ushirikiano wa Wananchi, Serikali na Shirika la
Brac.

Bi. Mwajuma amesema lengo la uanzishwaji wa Vituo vya Malezi kwa
watoto katika kijamii ni kuhakikisha watoto wanapata sehemu sahihi ya
kukaa na kulelewa wakati wazazi na walezi wanapokuwa katika majukumu ya kutafuta riziki.

Ameongeza kuwa vituo hivyo vya Malezi pia vitasaidia kuondokana na
vitendo vya Ukatili kwa watoto wadogo ikizingatiwa kuwa watoto hao hufanyiwa vitendo vya Ukatili katika jamii zetu.

" Vituo hivi vitakuwa chini ya jamii husika na vitasaidia malezi kwa
watoto pale wazazi na walezi wanapokuwa katika majukumu ya utafutaji wa kipato." alisema.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbagala Kuu Fabian Chilumba amesema kuwa wameupokea mradi huo kwa dhati na atahakikisha anahamasisha wananchi waendelee kuchangia nguvu zao kuhakikisha mradi inaisha kwa wakati na kuanza kutumika.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Somangila na Naibu Meya Manispaa ya Kigamboni Mhe. Steven Warioba amesema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa vituo hivyo katika Mitaa kwani kuna watoto wengi wanahitaji huduma ya uangalizi wakati wazazi hawapo nyumbani.

Naye Diwani Kata ya Kimbiji Muhidini Budaya amesema atashirikiana na
viongozi wa Manispaa ya Kigamboni kuhamasisha wananchi kushiriki
katika ujenzi wa vituo hivyo ili kuhakikisha watoto wao wanapata
sehemu sahihi ya kulelewa wakati wakiwa katika majukumu ya kutafuta
riziki.

Aidha Meneja Mradi kutoka Shirika la Brac, Novatus Tarimo amesema
Shirika lao linashirikiana na wananchi katika kuhakikisha mradi wa
ujenzi wa Vituo hivyo vya Malezi kea Watoto kwa ngazi ya Jamii
inakamilika na inaaza kutumiwa na Watoto wa Jamii husika.

Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Brac na wananchi kuchangian nguvu zao inaendesha zoezi la ujenzi wa mradi wa Vituo vya Malezi kwa
Watoto wadogo kwenye ngazi ya Jamii katika mikoa ya Dodoma na Dar Es Salaam ambapo, jumla ya Vituo 30 vinajengwa katika Mitaa ya
Halmashauri mbalimbali za mikoa hiyo.
 
Kwenye industry ya huduma za jamii, hakuna mradi unaoendeshwa na serikali ukafanikiwa. Angalia shule za serikali na Hospitali.
Naamin hata vituo hivyo havitakuwa na jipya.
 
Back
Top Bottom