tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,818
- 18,241
Wakati akihojiwa na Radio One katika kipindi cha Kumepambazuka, waziri wa kazi, Bi Gaudencia Kabaka alisema kwamba serikali imeanzisha mfuko wa fidia kwa wafanyakazi, ambao wafanyakazi na waajiri watalazimishwa kuchangia mfuko huo. Lengo la mfuko ni kutunisha fedha kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi wanaopata ulemavu au kufa wakiwa kazini.
Naona sasa serikali imewachoka wafanyakazi. Tumekuwa tukishuhudia wafanyakazi wakikatwa makato mbalimbali yasiyokuwa na tija kila kukicha. Walimu wanaidai serikali madeni yanayofikia Tsh bilioni 61. Pamoja na manyanyaso yote haya, bado serikali imeona haitoshi imeamua kubuni KERO mpya kwa wafanyakazi! Yaani eti badala ya kutatua kero za watumishi wao wanaongeza kero nyingine mpya!
Ni busara kama fidia hizi zingekuwa zinachangiwa na wajiri peke yao. Wao ndio wanaoshindwa kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kusababisha kuumia/kufa kwa wafanyakazi, badala ya kuwabebesha mzigo huu wafanyakazi.
Wabunge wasikubali kupitisha sheria hii inayolenga kuwakandamiza wafanyakazi.