Serikali yaanzisha kero mpya kwa wafanyakazi

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,759
18,177
Wakati akihojiwa na Radio One katika kipindi cha Kumepambazuka, waziri wa kazi, Bi Gaudencia Kabaka alisema kwamba serikali imeanzisha mfuko wa fidia kwa wafanyakazi, ambao wafanyakazi na waajiri watalazimishwa kuchangia mfuko huo. Lengo la mfuko ni kutunisha fedha kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi wanaopata ulemavu au kufa wakiwa kazini.

Naona sasa serikali imewachoka wafanyakazi. Tumekuwa tukishuhudia wafanyakazi wakikatwa makato mbalimbali yasiyokuwa na tija kila kukicha. Walimu wanaidai serikali madeni yanayofikia Tsh bilioni 61. Pamoja na manyanyaso yote haya, bado serikali imeona haitoshi imeamua kubuni KERO mpya kwa wafanyakazi! Yaani eti badala ya kutatua kero za watumishi wao wanaongeza kero nyingine mpya!

Ni busara kama fidia hizi zingekuwa zinachangiwa na wajiri peke yao. Wao ndio wanaoshindwa kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kusababisha kuumia/kufa kwa wafanyakazi, badala ya kuwabebesha mzigo huu wafanyakazi.

Wabunge wasikubali kupitisha sheria hii inayolenga kuwakandamiza wafanyakazi.
 
Wacha wafanyakazi wateseke maana hii sirikali ya baba rizi ndio best choice yao!
 
Hivi huu utaratibu unatumika nchi gani? Bila hata kuwa mtaalamu wa mambo ya kazi na ajira, mimi ningemshauri Mama Mhe Kabaka badala ya kuanzisha huo mfuko, basi atunge sharia inayowalazimisha WAAJIRI WOTE kuwawekea wafanyakazi wao BIMA YA AJARI KAZINI. Mimi nilishawahi kufanya kwa contract kwenye shirika moja la Kimarekani hapa nchini. Kwa mda wote wa contract wafanyakazi tuliwekewa BIMA YA AJARI KAZINI. Dreva mmojawapo alipata ajari kazini na alilipwa fidia na BIMA. Simple and straight forward!
 
Sera ya CHADEMA si kuwawezesha wananchi kuchangia kwenye mifuko ya maendeleo. Hivyo sishangai maliberali kushabikia uzi huu
 
serikali iliyofilisika kimapato utaijua tu,hivyo vitu tokea zamani vinafidiwa na serikali lakini mtalii wa dunia kaikausha hazina sasa anageukia hela ya fidia ya wafanyakazi waumiapo au wakifa kazini,..chezea m.kwere wewe!!!
 
10301511_525226750915035_6060418289805338542_n.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario
 
Wafanyakazi nao wamezidi mno kukishabikia Chama Cha Mafisadi, ngoja waonjeshwe joto ya jiwe, labda akili zao zitazibuka na kukikataa Chama cha Shemeji yao!!!!!!!!
 
Sera ya CHADEMA si kuwawezesha wananchi kuchangia kwenye mifuko ya maendeleo. Hivyo sishangai maliberali kushabikia uzi huu

we acha ujinga mimi si chadema lkn kwa serikali kuintroduce hii shombo ni upumbavu, if thats tje case walitaliwa wa include kwa kuboresha kwa kuongeza makato kwenye related funds kama Bima ya Afya.

Kuanza ku establish mfuko mwingine ni matumizi mabaya ya pesa ya walipa kodi hasa kwa sababu watataka wawe na premises badala na a lot of resources ambazo nyingi zitakuwa hazina tija kwa wananchi.

acha utoto Lizaboni waonee huruma wakulima wa tumbaku wanaotaabika ruvuma kwa kuuza tumbaku kwa mkopo usiolipika kisa serikali haina pesa kimbe pesa zipo ila wana misuse kwa matumizi ka hayo ya ujinga ujinga.
 
Last edited by a moderator:
Watumishi wamekuwa walalamishi wa kila aina juu ya uonevu wanaofanyiwa na waajiri wao ikiwemo serikali. Lakini cha kushangaza wao ndio wamekuwa wakinunuliwa nyakati za chaguzi na kuwapa madaraka haohao wanaowalalamikia. Sasa kwa kuwa hili ni la kujitakia namshauri Gaudensia akate hata 20% ya payee zao mpaka pale watakapojitambua. "Haiwezekani uwe msimamizi wa uchaguzi unahongwa pesa ya kula wiki moja halafu upande wa pili unamlalamikia aliyekuhonga kuwa uongozi wake haufai"
 
10301511_525226750915035_6060418289805338542_n.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario

Ajabu na kweli! Kwa wenzetu, majoho haya ni ishara ya uwezo wa kuondoa kero kwa wananchi, kwetu, Majoho haya ndiyo yanaongeza kero!!!!!!
 
Wakati akihojiwa na Radio One katika kipindi cha Kumepambazuka, waziri wa kazi, Bi Gaudencia Kabaka alisema kwamba serikali imeanzisha mfuko wa fidia kwa wafanyakazi, ambao wafanyakazi na waajiri watalazimishwa kuchangia mfuko huo. Lengo la mfuko ni kutunisha fedha kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi wanaopata ulemavu au kufa wakiwa kazini.

Naona sasa serikali imewachoka wafanyakazi. Tumekuwa tukishuhudia wafanyakazi wakikatwa makato mbalimbali yasiyokuwa na tija kila kukicha. Walimu wanaidai serikali madeni yanayofikia Tsh bilioni 61. Pamoja na manyanyaso yote haya, bado serikali imeona haitoshi imeamua kubuni KERO mpya kwa wafanyakazi! Yaani eti badala ya kutatua kero za watumishi wao wanaongeza kero nyingine mpya!

Ni busara kama fidia hizi zingekuwa zinachangiwa na wajiri peke yao. Wao ndio wanaoshindwa kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kusababisha kuumia/kufa kwa wafanyakazi, badala ya kuwabebesha mzigo huu wafanyakazi.

Wabunge wasikubali kupitisha sheria hii inayolenga kuwakandamiza wafanyakazi.

mbona mifuko ya kijamii inatoa hayo mafao?
Mafao ya Kuumia Kazini
Mafao ya Msaada wa Mazishi
http://www.pspf-tz.org/?od=death
Local Authorities Pension Fund (LAPF)
http://www.ppftz.org/home/index.php/en/disability
http://www.ppftz.org/home/index.php/en/death
 
kwa hiyo tutakuwa tunajifidia wenyewe!

Ndio maana yake. Na ukitembelea kwenye viwanda vingi unakuta wafanyakazi hawavai protective gears na serikali haichukui hatua kwa kuchelea kuwaudhi wawekezaji.
 
moto utawaka muda c mrefu nyie subirini, maana sasa naona ccm wanazidi kupeleka mkono mahali pasipohusika. A QUIET SNAKE IS THE MOST VENOMOUS ONE.
 
Duh! Kweli sasa CCM imetuchoka wafanyakazi. Kwahiyo na yenyewe tutakatwa asilimia ngapi tena?
 
Sera ya CHADEMA si kuwawezesha wananchi kuchangia kwenye mifuko ya maendeleo. Hivyo sishangai maliberali kushabikia uzi huu

wacha siasa. all employees must be in at most one social security scheme (sheria inataka hivyo). na hizo social security schemes tayari zinatoa hayo mafao. ni haja gani ya kuchangia tena?
 
Back
Top Bottom