Serikali yaanza mchakato wa ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Umeme Mto Ruhudji Njombe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Timu ya Watalaamu wa Serikali imefika na kufanya ukaguzi wa kwanza katika maporomoko ya mto Ruhudji katika kijiji cha Itipula mkoani Njombe ambao unatarajiwa kujengwa mradi mkubwa wa umeme utakaozalisha megawats 358 za umeme.

Mradi huo ambao utajengwa katika kipindi cha miezi 36 unaotarajiwa kuanza mwezi juni au julai mwaka huu ulifanyiwa utafiti kwa mara ya kwanza 1998 na kisha kusimama kwa muda mrefu jambo ambalo lilisababisha wananchi kupoteza matumaini na kuanza kurudi kwenye maeneo waliotakiwa kupisha.

Naibu katibu mkuu wizara ya nishati mhandisi Leonard Masanja akizungumza mbele ya timu ya watalaamu kutoka wizara ya nishati, TANESCO na wakazi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mradi amesema katika mradi huo uliosubiriwa kwa zaidi ya 22 kutajengwa mabwawa 2,Intake moja pamoja miuondombinu ya umeme na barabara.

Tito Muinuka ambaye ni mkurugenzi wa shirika la umeme TANESCO nchini anasema kitendo cha kufika hapo ni mwanzo wa kuanza utekelezaji wa mradi huo na kwamba kukamilika kwake kutaongeza kiwango cha hazina ya megawats nchini huku Wangwe Elieza Mjiolojia wa TANESCO akisema kutajengwa Zanziber DAM ,Storage Dam na Intake moja

Kwa upande wao wakazi wa kijiji cha Itupula na vijiji jirani akiwemo Eleteus Mkolwe,Josphat Mwenda ambao ni miongoni mwa waliosimama kufanya shughuli za mendeleo ya kudumu katika la mradi kwa zaidi ya miaka 22 wanasema wamefurahishwa na uamuzi huo wa serikali na kwamba wana amini wanakwenda kupata ajira kwa vijana kupitia mradi huo.

1610515003752.png
 
MW358, huu ni umeme ni mwingi sana. So far kwa vyanzo vyote hivi tena vya umeme wa maji, tuwe na imani tutapata umeme wa uhakika na gharama za uzalishaji zitashuka. Hivyo, tuamini pia na bei za bidhaa zitashuka kwa kiwango fulani. Hongera sana kwa Govt na wa-TZ wote..!!
 
Back
Top Bottom