Serikali yaanza kuwafilisi Wenye makontena waliokwepa kulipia kodi

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,694
2,000
Kwa vile wengine wanafanya haimaanishi na sisi tufanye hivyo. Let's do away with madalali! Hela nyingi zinapotea kupitia hawa watu. Hivyo hamna kitengo serikalini kinachoweza kufanya hiyo kazi?. Hebu gazeti la jamhuri lituchunguzie hayo makampuni ni ya nani.
Hicho kitengo kitakuwa ni kupoteza pesa in long run kwa sababu ya kulipa mishahara na uendeshaji.

Haya matukio ya kukwepa kodi ni one-off.

Kwenye uchumi huria mara nyingi inayodaiwa huwa ni serikali.

Ni mara chache sana serikali kudai kwa sababu sekta ya biashara kwa sasa iko mikononi mwa wananchi.

Serikali kwa sasa kwa kiwango kikubwa haifanyi biashara.
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
LAKINI KUKWEPA KODI SI KOSA LA JINAI? KWA NINI WASIFIKISWE MAHAKAMANI PIA?
Of course best practice ni kuwafikisha mahakamani. Lakini chukulia mfano wewe umewafundisha wanao kuwa kuiba kitu cha mtu ni halali na wakafanya hivyo maisha yao yote. Halafu ghafla unaanza kushika dini wakati watoto wako washakuwa majizi sugu, utawakamata na kuwapeleka polisi au utaanza kuwapa somo upya? Bora kuwapa somo upya maana wafanyabiashara wote Tanzania ni wakwepa kodi na hawana utamaduni wa kulipa kodi. Mimi ningeshauri waanze na kuhamasisha wafanyabiashara juu ya sheria za kodi halafu baada ya hapo ndio waanze kudai kodi. Kuna watu wamefungua biashara kwa vile tu wamepewa mchongo na Riziwani kuwa mzigo utapita bandarini bila ushuru
 
singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,395
2,000
Wadaiwa 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella alisema hayo Dar es Salaam jana.

Akizungumza na gazeti hili, Kevela alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kevela alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa kulipa.

Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni alitaja wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh 28,249,352.50, Strauss International (45,393,769.95), Farid Abdallah Salum (52,185, 614.97).

Wengine ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro (64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem Abdul (130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading Co.Ltd (448,690,271.90).

Pia wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff Tyres General Co Ltd, (7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan (68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah Salem Sh 75,334,871. 85.

Akizungumzia wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14 walizopewa na zikaisha juzi, alisema wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza kulipa madeni baada ya kampuni yake kuwafuatilia.

Kevela alisema hadi jana zaidi ya Sh milioni 200 zimelipwa na wadaiwa hao.

Wadaiwa hao 24 walishindwa kulipa kodi kwa wakati kama walivyotakiwa kufanya, ndipo TRA ilimpa dalali huyo kazi ya kuwafilisi. Kampuni hiyo ya udalali ilitoa siku 14, kuanzia Februari 10, mwaka huu wawe wamekamilisha; muda ambao umeisha juzi.

Kevela alisema katika siku hizo 14, kati waliojitokeza kulipa,wanne kati yao wamemaliza madeni na wengine wanne wamepunguza madeni na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki. Waliomaliza madeni yao Wadaiwa waliolipa madeni yao yote ni Issa Ali Salim aliyekuwa akidaiwa Sh 94,543,161.96, Libas Fashion (26,593,245.78), Omary Hussein Badawy (21,346,615.40) na Zulea Abas Ali (16,760577.24).

Waliopunguza madeni yao waliopunguza madeni yao ni Zuleha Abbas Alli aliyelipa Sh milioni 47 na kubakiwa na deni la Sh 28,508,551, awali alikuwa akidaiwa Sh 75,508,551.88, mwingine ni Ally Awes Hamdani aliyelipa Sh milioni 17.26 awali alikuwa akidaiwa Sh 55,485,904.07).

Wengine waliopunguza kidogo ni Tifo Global Trading Co Ltd waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 1,573,300,644.58, Lotai Steel Tanzania Ltd, waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 5,476,475,738.19.

“Tulikabidhiwa wadaiwa 24 na TRA, waliokwepa kodi kwa kutorosha kontena katika bandari kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa walipewa muda wa kulipa ila walikaidi, tukakabidhiwa tuwafilisi mali zao zote ili kulipia madeni na wamejitokeza hao na kuanza kulipa wengine wamemaliza”, alisema Kevela.

Awali wadaiwa 24, walikwepa kodi ya Sh bilioni 18.95 kwa kutorosha makontena 329 ya bidhaa zao kutoka Kampuni ya SSB ambayo ndiyo mmiliki wa bandari kavu ya (Azam ICD) na kampuni ya Regional Cargo Services.

Mapema Desemba mwaka jana aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA, Dk Philip Mpango alizungumza na waandishi wa habari na kusema kampuni 15 kati ya 43, zilizokwepa kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya Azam, wamelipa.

Dk Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa kodi hao 43, kulipa wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake. Kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na waliobaki hawakujitokeza kulipa.
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,610
2,000
Hivi haukuwekwa mwongozo ktk ulipaji huo kws maana inawezekana vipi mtu anadaiwa bilion moja na point kadhaa alaf anapunguza deni kwa kulipa milion mbili?huu ni mzaha,mtazamo wang kama mtu hajalipa angalau nusu ya kile anachodaiwa nae afilisiwe tu
 
samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,393
2,000
Kweli uchumi wa TZ umeshikwa na wageni. ( kwa mujibu wa hayo majina)
 
MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,642
2,000
Zipo kejeli nyingi kuwa ni nguvu ya soda, hata kama ni soda ukiweka gongo utalewa, kwa hio hii ni soda special-Rais Magufuli

Wanaolalamika wachache muwapuuze kwa sababu ni miongoni ya waliofaidi matunda ya wanyonge kwa miaka ya nyuma-Rais Magufuli
ngoma ya watoto haikeshi
 
wakimataifa.

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
1,603
1,500
Ukifungwa na [HASHTAG]#magufuli[/HASHTAG] hakuna [HASHTAG]#suluhu[/HASHTAG] kutoka [HASHTAG]#majaliwa[/HASHTAG]
 
kakayake

Member
Dec 23, 2015
12
45
Hivi hao ni wadaiwa au wakwepa kodi nchi zingine walitakiwa kuwa ndani wananyea debe

Afadhali ipi sasa? jiongeze mwenyewe
 
afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
It is easier to say you will do something than to actually do it!

Talk is cheap!

Kukaa nyuma ya keyboard/keypad na kuweza kuandika comments au kutoa ushauri kimaandishi ni kazi rahisi sana ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza!

Kwa hiyo ulitaka kusema nini?
 
afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Hivi hao ni wadaiwa au wakwepa kodi nchi zingine walitakiwa kuwa ndani wananyea debe

Afadhali ipi sasa? jiongeze mwenyewe

Nadhani watashitakiwa baada ya kulipa hiyo hela. Kukimbilia kuwashitaki na hatimaye kuwafunga kabla hawajalipa hakutaisaidia nchi.
 
Jipu-bishi

Senior Member
Feb 16, 2016
107
225
Wadaiwa 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella alisema hayo Dar es Salaam jana.

Akizungumza na gazeti hili, Kevela alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kevela alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa kulipa.

Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni alitaja wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh 28,249,352.50, Strauss International (45,393,769.95), Farid Abdallah Salum (52,185, 614.97).

Wengine ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro (64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem Abdul (130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading Co.Ltd (448,690,271.90).

Pia wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff Tyres General Co Ltd, (7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan (68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah Salem Sh 75,334,871. 85.

Akizungumzia wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14 walizopewa na zikaisha juzi, alisema wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza kulipa madeni baada ya kampuni yake kuwafuatilia.

Kevela alisema hadi jana zaidi ya Sh milioni 200 zimelipwa na wadaiwa hao.

Wadaiwa hao 24 walishindwa kulipa kodi kwa wakati kama walivyotakiwa kufanya, ndipo TRA ilimpa dalali huyo kazi ya kuwafilisi. Kampuni hiyo ya udalali ilitoa siku 14, kuanzia Februari 10, mwaka huu wawe wamekamilisha; muda ambao umeisha juzi.

Kevela alisema katika siku hizo 14, kati waliojitokeza kulipa,wanne kati yao wamemaliza madeni na wengine wanne wamepunguza madeni na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki. Waliomaliza madeni yao Wadaiwa waliolipa madeni yao yote ni Issa Ali Salim aliyekuwa akidaiwa Sh 94,543,161.96, Libas Fashion (26,593,245.78), Omary Hussein Badawy (21,346,615.40) na Zulea Abas Ali (16,760577.24).

Waliopunguza madeni yao waliopunguza madeni yao ni Zuleha Abbas Alli aliyelipa Sh milioni 47 na kubakiwa na deni la Sh 28,508,551, awali alikuwa akidaiwa Sh 75,508,551.88, mwingine ni Ally Awes Hamdani aliyelipa Sh milioni 17.26 awali alikuwa akidaiwa Sh 55,485,904.07).

Wengine waliopunguza kidogo ni Tifo Global Trading Co Ltd waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 1,573,300,644.58, Lotai Steel Tanzania Ltd, waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 5,476,475,738.19.

“Tulikabidhiwa wadaiwa 24 na TRA, waliokwepa kodi kwa kutorosha kontena katika bandari kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa walipewa muda wa kulipa ila walikaidi, tukakabidhiwa tuwafilisi mali zao zote ili kulipia madeni na wamejitokeza hao na kuanza kulipa wengine wamemaliza”, alisema Kevela.

Awali wadaiwa 24, walikwepa kodi ya Sh bilioni 18.95 kwa kutorosha makontena 329 ya bidhaa zao kutoka Kampuni ya SSB ambayo ndiyo mmiliki wa bandari kavu ya (Azam ICD) na kampuni ya Regional Cargo Services.

Mapema Desemba mwaka jana aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA, Dk Philip Mpango alizungumza na waandishi wa habari na kusema kampuni 15 kati ya 43, zilizokwepa kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya Azam, wamelipa.

Dk Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa kodi hao 43, kulipa wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake. Kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na waliobaki hawakujitokeza kulipa.
Nimesikitishwa, kwa majina kuonekana ya aina moja Bali, TRA kutoa mamlaka kwa kampuni kufanya kazi waliyopewa kisheria ambayo haijawapa mamalaka kishare hayo mamlaka na chombo chochote ya kukusanya mapato. Hakukuwa na haja ya kuwataja hawa watu kwenye vyombo vya habari na kuwadhalilisha namna hii pamoja na yote wana haki ya Ufaraga(Privacy) na TRA wangewafikia hawa watu na kuwapata hizi taarifa na wala sisi(public) hatukutakiwa kupewa majina. Sijui hawa kampuni ya Ufilisi wamefanya kwa niaba ya Mamlaka, au Wizara lakini pia sijui sheria imewapata wanazotumia imewapa mamlaka ya kutoa amri ambavyo wanafanya
Thinking aloud...hii ni bongo sheria sio lazima ifuatwe....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom