Serikali yaanza kuwafilisi Wenye makontena waliokwepa kulipia kodi

Hata katika nchi zilizoendelea kazi ya kufuatilia madeni hufanywa na madalali!

Hakuna jambo la ajabu kwa madalali kufanya kazo hiyo!
Kwa vile wengine wanafanya haimaanishi na sisi tufanye hivyo. Let's do away with madalali! Hela nyingi zinapotea kupitia hawa watu. Hivyo hamna kitengo serikalini kinachoweza kufanya hiyo kazi?. Hebu gazeti la jamhuri lituchunguzie hayo makampuni ni ya nani.
 
simon wa uda mbona hayupo,..
hii danganya toto haikubaliki....
mkwepa kodi anabembelezwa hivi aisee,..muhujumu uchumi
tunawabembeleza na kuwanyenyekea hivi..,..
hivi viloja vipo TZ tu...............
 
Hawa madalali wanaingiaje humu, kwani TRA wanashindwa kufuatilia madeni wenyewe? Hawa Yona wanachukua 10% sio? Hizi Auction Marts zinamilikiwa na nani?
Registered as Debt Collectors/ Court Brokers na wanalipia kodi za license zao as such. Halafu wewe una hoji upuuzi. Wake up Tanzania.
 
Ni aheri ungeandika kwa Kiswahili. Kama unakipenda sana kiingereza, weka juhudi zaidi katika kujifunza ili uweze kuimudu lugha hiyo.

poorly/
MTU anadaiwa 1 bil, analipa 2mil, mnamu Assume amepunguza HOW THIS SHITS!!
NI BORA MKAWAINGIZA KATIKA MFUMO MAALUM WADAIWA WOTE WALIPE KWA AWAMU KWA LAZIMA!
ITS A JOKES!,N NONSENSE!!
*************
hapana pata kitu hapa besa yote IPO Dubai,kama tafilisi tafilisi Mali ya million 20/30 pekee!
ingine kwisha ficha mbali bana.
 
Nakumbuka kuna kiongozi wa awamu ya nne aliwahi kusema kuwaingilia wafanya biashara wakubwa kunaweza kukaiyumbisha nchi akimaanisha waachwe wafanye wapendavyo,ndio huu mchezo ninaiuona hapa!
 
Unatakiwa kufahamu kuwa wafanyabiashara wengi Tanzania ni Waarabu, Wahindi na Wapemba ambao kiasili ni waislam lakini pia kuna ukweli ambao haujafanyiwa utafiti, wafanyabiashara wengi ni waislam. Kuna sababu nyingi lakini mojawapo inasadikika kuwa waislam wengi kutokana na historia, hawakuwa kwenye ajira, wakajibidisha kwenye biashara kama ndiyo option pekee iliyokuwepo, na kwa kufanya hivyo miongoni mwao baadhi wakafanikiwa mpaka kuwa wafanyabiashara wakubwa.

Walliofanikiwa, wengine wakawarithisha watoto wao, watoto walirithi kwa kuona kilichokuwa kikifanywa na wazazi wao.

Mbona wote nimajina ya kiislamu container zilikuwa ni za Bakwata??
 
Hatua nzuri, mwanzo mzuri. Athari zake ni kuwa licha ya kuipatia serikali kilicho chake lakini pia itaweka heshima ya kodi na kuwafanya wafanyabiashara wajue kuwa lazima walipe kodi. Ukwepaji kodi sio tena competitive advantage. Mfano sasa hivi bei ya matairi ya gari imepanda, ina maana wale wafanyabiashara waliokuwa wanawazidi wenzao kisa tu wao wamekwepa kodi kwa memo za Riziwani Kikwete sasa watacheza katika uwanja sawa na mzalendo mlipa kodi, level play ground. Hongera kwa hili rais wangu JPM
Wakwepa kodi wanashirikiana na watendaji wa serikali.
TPA hakuna auto system iliyo imara, watu wameichakachua na wanajipigia tu.
What about memos from the 'then' white house? Home Shopping Center uaikumbuka?
 
Wengine waliopunguza kidogo ni Tifo Global Trading Co Ltd waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 1,573,300,644.58, Lotai Steel Tanzania Ltd, waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 5,476,475,738.19.

Kuna watu wanautani... yani milion mbili kwenye hela zote hizo!!! bora angeacha tu kulipa...
 
WADAIWA 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella alisema hayo Dar es Salaam jana.

Akizungumza na gazeti hili, Kevela alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kevela alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa kulipa.

Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni Alitaja wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh 28,249,352.50, Strauss International (45,393,769.95), Farid Abdallah Salum (52,185, 614.97). Wengine ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro (64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem Abdul (130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading Co.Ltd (448,690,271.90).

Pia wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff Tyres General Co Ltd, 7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan (68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah Salem Sh 75,334,871. 85.

Akizungumzia wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14 walizopewa na zikaisha juzi, alisema wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza kulipa madeni baada ya kampuni yake kuwafuatilia. Kevela alisema hadi jana zaidi ya Sh milioni 200 zimelipwa na wadaiwa hao.

Wadaiwa hao 24 walishindwa kulipa kodi kwa wakati kama walivyotakiwa kufanya, ndipo TRA ilimpa dalali huyo kazi ya kuwafilisi. Kampuni hiyo ya udalali ilitoa siku 14, kuanzia Februari 10, mwaka huu wawe wamekamilisha; muda ambao umeisha juzi.

Kevela alisema katika siku hizo 14, kati waliojitokeza kulipa,wanne kati yao wamemaliza madeni na wengine wane wamepunguza madeni na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki. Waliomaliza madeni yao Wadaiwa waliolipa madeni yao yote ni Issa Ali Salim aliyekuwa akidaiwa Sh 94,543,161.96, Libas Fashion (26,593,245.78), Omary Hussein Badawy (21,346,615.40) na Zulea Abas Ali (16,760577.24).

Waliopunguza madeni yao Waliopunguza madeni yao ni Zuleha Abbas Alli aliyelipa Sh milioni 47 na kubakiwa na deni la Sh 28,508,551, awali alikuwa akidaiwa Sh 75,508,551.88, mwingine ni Ally Awes Hamdani aliyelipa Sh milioni 17.26 awali alikuwa akidaiwa Sh 55,485,904.07). Wengine waliopunguza kidogo ni Tifo Global Trading Co Ltd waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 1,573,300,644.58, Lotai Steel Tanzania Ltd, waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 5,476,475,738.19.

“Tulikabidhiwa wadaiwa 24 na TRA, waliokwepa kodi kwa kutorosha kontena katika bandari kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa walipewa muda wa kulipa ila walikaidi, tukakabidhiwa tuwafilisi mali zao zote ili kulipia madeni na wamejitokeza hao na kuanza kulipa wengine wamemaliza”, alisema Kevela.

Awali wadaiwa 24, walikwepa kodi ya Sh bilioni 18.95 kwa kutorosha makontena 329 ya bidhaa zao kutoka Kampuni ya SSB ambayo ndiyo mmiliki wa bandari kavu ya (Azam ICD) na kampuni ya Regional Cargo Services.

Mapema Desemba mwaka jana aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA, Dk Philip Mpango alizungumza na waandishi wa habari na kusema kampuni 15 kati ya 43, zilizokwepa kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya Azam, wamelipa.

Dk Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa kodi hao 43, kulipa wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake. Kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na waliobaki hawakujitokeza kulipa.
Chanzo:Habarileo

SORRY JAMANI, MBONA HAWA WATU WENGI KAMA SIO WOTE NI WAISLAM NA WACHAGA WACHACHE AMA NI MAJINA TU!!!
 
Hatua nzuri, mwanzo mzuri. Athari zake ni kuwa licha ya kuipatia serikali kilicho chake lakini pia itaweka heshima ya kodi na kuwafanya wafanyabiashara wajue kuwa lazima walipe kodi. Ukwepaji kodi sio tena competitive advantage. Mfano sasa hivi bei ya matairi ya gari imepanda, ina maana wale wafanyabiashara waliokuwa wanawazidi wenzao kisa tu wao wamekwepa kodi kwa memo za Riziwani Kikwete sasa watacheza katika uwanja sawa na mzalendo mlipa kodi, level play ground. Hongera kwa hili rais wangu JPM

LAKINI KUKWEPA KODI SI KOSA LA JINAI? KWA NINI WASIFIKISWE MAHAKAMANI PIA?
 
Huyo dalali nae ni mpumbavu tu, mtu anadaiwa mabilioni ,analipa milioni mbili halafu unakuja kumweka katika fungu la walio punguza deni. Msitake kutufanya wajinga bana. Hao ndio walitakiwa wafilisiwe kwanza maana wanaleta utani.
mkuu mi nimerudia mara 4 kusoma kile kipande, nimeshangaa kweli unasemaje mtu anadaiwa bilioni 5 halafu useme kapunguza deni kwa mil 2? dhihaka ilioje!
 
Hao watu wangeandaliwa mfumo wa kunipa. Taratibu za nchi zetu mali za watu wengi hazifahamiki zilipo. Hapo hasa inatakiwa ukishindwa kulipa unakuwa declared bankrupt. Hakuna kufanya biashara kwa miaka Milano, unafilisiwa na mahakama ifanye kazi yake.
 
Back
Top Bottom