Serikali yaanza kufanyia kazi kwa haraka malalamiko yaliyoletwa JamiiForums kuhusu hospitali ya Dar Group

bwashee2020

Member
Dec 8, 2020
43
59
Tunarudi tena jukwaani wana JF kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kutupatia kiongozi bora wana Temeke; Ndg. Godwin Gondwe ambaye siku ya jana(tar 24/12/2020) alifanya ziara katika hospitali ya Dar Group akiambatana na mganga mkuu wa wilaya, DAS, OCD, mwenyekiti wa Serikali ya mtaa , afsa rasilimali watu na ma-afsa usalama, na kuwapa nafasi wafanyakazi kuelezea kero zao.

Baada ya kuwasikiliza wafanyakazi , muheshimiwa mkuu wa wilaya pia aliwapa management nafasi ya kuongea na kuleta usuluhishi kati ya wafanyakazi na management ya hospitali hiyo inayohudumia zaidi ya wateja 400 kwa siku na zaidi ya wateja 11,000 kwa mwezi.

Aidha muheshimiwa mkuu wa wilaya alitoa maagizo yafuatayo:

1. Kuheshimu taaluma za wafanya kazi na kuacha kunyanyasa wafanyakazi mara moja.

2. Wafanyakazi kutimiza wajibu wao wa kuhudumia wagonjwa na kufata taratibu za kazi.

3. Mikataba kupitiwa upya na kumpa mfanyakazi taarifa ya siku 28 kabla ya mkataba wake kuisha na unapoisha apewe stahiki zake.

4. Kuacha mara moja kutuma mtu kuchuguza vyumba vya madaktari na kuingia bila taarifa kwani tiba ni siri kati ya mgonjwa na tabibu.

5.Kuacha mara moja kuwashinikiza madaktari kuongeza vipimo visivyo na tija kwa wagonjwa ili kuongeza kipato kwani kufanya hivyo ni kuwaumiza wagonjwa na kuhujumu mifuko ya bima za afya na kuhujumu uchumi wa nchi.

6. Watumishi waende likizo kwa wakati na wapewe malipo yao ya likizo.

7. Kuacha mara moja tabia ya kuwasumbua wafanyakazi mara wapatapo ujauzito kazini, ikiwemo kuwafukuza kazi sababu ya ujauzito, kwani ujauzito ni zawadi kutoka kwa Mungu.

8. Kurudishwa mara moja kazini kwa daktari daraja la pili ambaye ilithibitika alisimamishwa kwa uoenevu.

9. Pia mkuu wa wilaya amesema ataunda tume maalumu itakayoichunguza kwa kina hospital ya Dar group, tume hiyo itaanza kazi tarehe 26 December na ameomba wafanya kazi waipe ushirikiano tume hiyo bila kuogopa vitisho.

SHUKRANI


Ahsante Mheshimiwa Rais kwa kutupatia Godwin Gondwe wana Temeke, viongozi wengine vijana wajifunze kwa mkuu huyu wa wilaya ya Temeke.

Tunaishukuru wizara ya Afya chini ya Dr Gwajima kwa kuendelea kuisimamia vyema sekta ya Afya.

Tunaushukuru uongozi mzima wa wilaya ya Temeke na DMO wa Temeke kwa kulipa jambo hili uzito unaostahili na kulishughulikia ipasavyo.

Tunashukuru bodi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi wa JamiiForums kwa kutusaidia kupaza sauti zetu. Mungu aendekee kuwalinda na awabariki.

Shukrani ziende pia kwa wahudumu wote wa Afya nchini kwa kuendelea kufanya kazi zao kwa weledi licha ya changamoto wanazozipitia.

WITO
Viongozi wakumbuke vyeo ni dhamana wajitahidi kuongoza kwa kuzingatia haki na usawa bila kuweka makundi baina ya wanaowaongoza na wajitahidi kuwa VIONGOZI kuliko kuwa WATAWALA.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.


 
Kama kweli ina macho ya kuona hili iangalie na malalamiko ya mfuko wa bima ya afya sababu ya kuzorota kwa huduma zitolewazo na mfuko huu, kila kukicha baadhi ya huduma zinapunguzwa. Je hii nayo ikoje? Mfuko ni NHIF.
 
Kama kweli ina macho ya kuona hili iangalie na malalamiko ya mfuko wa bima ya afya sababu ya kuzorota kwa huduma zitolewazo na mfuko huu ,kila kukicha baadhi ya huduma zinapunguzwa . Je hii nayo ikoje?
Kweli kabisa hata kipimo Cha elfu tano naambiwa nilipie wakati bima nachangia kila mwezi. Bima nalo janga lingine la taifa.

Mtoto akitibiwa kwa bima dawa hakuna au unaambiwa hana ugonjwa. Ukitoa keshi ugonjwa utaonekana na dawa utanunua.

Kwa kweli ni mateso Sana.
 
Kwa hili nampongeza DC na Serikali kwa ujumla. Unyanyasaji kwa watu wanyonge sio jambo zuri. Hongera na wewe 'Whistleblower' jitahidi kucover identity yako usiongee sana kama vile si unaona malalamiko yetu yamefika maea hili mara lile, watakutafutia sababu halali kama binadamu unaweza kuteleza.
 
Kwa hili nampongeza DC na Serikali kwa ujumla. Unyanyasaji kwa watu wanyonge sio jambo zuri. Hongera na wewe 'Whistleblower' jitahidi kucover identity yako usiongee sana kama vile si unaona malalamiko yetu yamefika maea hili mara lile, watakutafutia sababu halali kama binadamu unaweza kuteleza.
Ahsante kwa ushauri kiongozi. Mungu ni mwema.
 
Sawa toeni huduma nzuri kwa wateja msiturudishe kule mama mzazi anajifungua wauguzi wanapiga stori.
Ikiwa hivyo hata wewe utakuwa wa kwanza kuingia kwenye lawama kwani wakati wengine wanaona uelekeo wa kupotea wewe na ukoo wako kusifia tu hata uovu.
 
Kama ni kweli hilo lililoandikwa ndilo lililofanyika,namuombea GG kwa Bwana Mungu Mwenyezi azidi kumpa afya njema ya mwili, akili, roho na moyo ili awatumikie Watanzania vile kiongozi anavyopaswa kutumika.

GG piga kazi kwa maslahi mapana ya Taifa na kwa kumuogopa Mungu wako.
 
Kama ni kweli hilo lililoandikwa ndilo lililofanyika,namuombea GG kwa Bwana Mungu Mwenyezi azidi kumpa afya njema ya mwili,akili,roho na moyo ili awatumikie Watanzania vile kiongozi anavyopaswa kutumika.
GG piga kazi kwa maslahi mapana ya Taifa na kwa kumuogopa Mungu wako.
Ila tu ni kama anafanya hayo kwa dhati na sii kwa unafiki na maslahi binafsi.ikiwa hivyo atakuwa analitendea haki taifa letu.
 
Ikiwa hivyo hata wewe utakuwa wa kwanza kuingia kwenye lawama kwani wakati wengine wanaona uelekeo wa kupotea wewe na ukoo wako kusifia tu hata uovu.
Duh;
Hapana mkuu huwa nina hulka ya kutwanga pale inapotakiwa kutwanga, fuatilia vyema post zangu, usihesabu tu zile ambazo hazifurahishi nafsi yako.
 
Tofauti za kimalezi uchangia pia.
Huwezi linganisha mtu aliyekulia mjini na aliyeleta ng'ombe mjini na akakosa nauli ya kurudi kijijini akabebwabebwa we Hadi akawa mtu kwa msaada wa ndumba akawa mtu hata kiutendaji ni lzm wawe tofauti
 
Back
Top Bottom