Serikali yaanza kufanya tathmini ya kila kaya kubaini familia zenye njaa na kugawa chakula

Hivi kejeli zilipokuwa zikitamkwa zilikuwa zinamaanisha nini? Wamesema hakuna njaa sasa wanaenda kufanya nini huko? Au ndiyo kupima kina cha maji kilipofikia?

Viongozi waache kucheza na akili za watu
serikali ya ccm ni sikivu kauli yake ni faraja tofautisha kualu ya serikali na kauli ya bwana mmoja serikali si mtu
 
Lowassa kweli nimemkubali... Ni mwanasiasa anaetumia vema kichwa chake..jamaa wameona akigawa chakula tuu lazima itakula upande mmoja hiyo
 
Sijawahi kumuamini faru J kabisa, juzi tu kasema hatoi msosi hata iweje leo nani tena anaagiza tathmini hiyo?
 
Wakigawa mnalalamika wakikaa kimya mnalalamika mlitaka watu wafe ndo mje kuilaumu selikari kuwa tulisema kuwa njaa ipo
Mjifunze siku nyingine kubisha wakati hali halisi inaonekana.

Siku kadhaa nyuma maneno ya shombo yalitawala humu, azimio la kugawa chakula limekuja ndiyo tunakutana na komenti kama zako.
 
Siri-kali imenunua shamba?

Mkulu "alitania" kwa kusema serikali haitatoa chakula cha msaada(chakula cha bure).

Link Serikali haitagawa chakula cha msaada - Magufuli | East Africa Television

Kwa nini siri-kali imeamua sasa kubeba misalaba ya wananchi walioshindwa kujitetemesha, wapiga dili, wa-hapana kazi tu kujipatia chakula?

Au wanataka kuzuia mswada binafsi (Zitto) wa kura ya kutokuwa na imani ya mtumbua majipu.

Njaa imepinda nayo inyooshwe.

Link Rais Magufuli: Magazeti yanayoandika kuna njaa yamenunuliwa na wanasiasa na wafanyabiashara

Link tishio la njaa, vyakula vyapanda

Link BAA LA NJAA NCHINI: Wananchi Kwimba wamsimamishwa Mkuu wa Mkoa wakiwa na mabua yaliyokauka


Duhuu kwenye hiyo video pogba anarusha mikono na madole utafkiri anawaelekeza viziwi na vipofu.
 
Hapa mimi sielewi, kwa hiyo serikali haina uhakika na hizo tani 2.5m (I stand to be corrected on figures) zilipo na inazisaka majumbani mwa watu!?
Sijui hili zoezi litafanyikaje ...kutakuwa na kuchungulia vyumbani au uvunguni!? Mind you, wanakokwenda kufanya tathmini ni kwa wananchi ambao tayari muda mrefu wanalia upungufu na ukosefu wa chakula!
 
Nimesikia kwenye magazeti ya leo kuwa serikali imeanza kufanya tathimini ya familia zenye njaa na kuanza kugawa chakula nchi nzima .

Chanzo.magazeti ya leo
Hayo magazeti hawaachi tu habari za kichochezi mbona nimemsikiliza viruri pole pole pale Lumumba ameekataa kwa kichwa cha mbwa kwamba hakuna njaa watakuwa wemekosa habari za kuandika wana hamu ya kutumbuliwa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom