Serikali yaandaa mwongozo wa msamaha wa matibabu kwa makundi tofauti yasiyokuwa na uwezo

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019


Kupitia wizara afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imeandaa mwongozo wa msamaha kwa makundi tofauti yasiyokuwa na uwezo ikiwa ni pamoja kundi la watu wagonjwa sugu ikiwa ni pamoja na selimundu

Hayo yamesemwa Juni 10 ,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii ,jinsia,wazee na Watoto,Dokta Faustine Ndugulile,wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Taska Mbogo aliyehoji mpango wa Serikali wa kuwasaidia wagonjwa wa Selimundu[Sickle cell] juu ya kupata matibabu bure.

Katika Majibu yake,Mhe,Ndugulile amesema wagonjwa wa Selimundu wanahitaji matibabu mfululizo kwani huwa wanapata maumivu na madhara ya ugonjwa huo mara kwa mara hivyo ,serikali imeandaa mwongozo wa kutoa msamaha kwa makundi tofauti yasiyo na uwezo ikiwa ni pamoja na kundi la wagonjwa wa Selimundu na kinachotakiwa ni kuhakikiwa na kupatiwa kibali cha huduma bila malipo.

Aidha,Dokta. Ndugulile amesema Serikali imeanzisha mpango wa Taifa wa Udhibiti wa Magonjwa yasiyoambukizwa ambapo ugonjwa wa Selimundu [sickle Cell] utakuwa ni moja ya magonjwa yatakayokuwa yanaratibiwa kitaifa.
 
Back
Top Bottom