Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imetangaza kuajiri madaktari wapya 610, watakaokwenda kutoa huduma kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, pamoja na kusaidia kukabiliana na janga la Virusi vya Corona.
Akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bw. Selemani Jaffo, amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha posho za kujikimu kwa madaktari hao wapya wanapewa kwa wakati, huku hakuna mabadiliko ya vituo vya kazi yatakayofanywa.
Aidha, Waziri Jaffo akawa na ujumbe mahususi kwa madaktari hao wapya wanaotakiwa kuripoti kati ya tarehe 11 hadi 25 ya mwezi huu, na kwenda kuhudumu katika Hospitali za wilaya 98, vituo vya afya 433 na zahanati 368.
Kuajiriwa kwa madaktari hao 610, kunafanya sasa toka serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, madaktari 9,839 waweze kupata ajira serikalini.