Serikali yaahirisha kuanza kutumika kwa viwango vipya vya mishahara katika sekta binafsi hadi Januari mwakani

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,967
10,461
Mishahara sekta binafsi mwakani

na Irene Mark, Dodoma

SERIKALI imeahirisha kuanza kutumika kwa viwango vipya vya mishahara katika sekta binafsi.
Tangazo la kuahirishwa kuanza kutolewa kwa mishahara hiyo mipya, lilitolewa mjini hapa jana na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Kapteni John Chiligati, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kapteni Chiligati alisema kuwa, imeamriwa sasa kuwa, viwango vipya vya mishahara ya watumishi wa sekta binafsi vitaanza kutumika rasmi Januari mwakani.

Mapema mwezi uliopita, serikali iliwataka waajiri wa sekta binafsi kuongeza viwango vya mishahara ya watumishi wao, kulingana na hali halisi ya maisha, nyongeza iliyotakiwa kuanza leo.

Kwa mujibu wa Chiligati, uamuzi huo wa serikali umekuja baada ya kupokea maombi kutoka kwa waajiri binafsi wa sekta mbalimbali, wakiomba muda zaidi ili kuweka sawa bajeti zao.

Alisema baada ya serikali kutamka viwango vipya vya mishahara ya watumishi binafsi, waajiri wao walipeleka malalamiko wizarani, wakiomba kuongezewa muda ili wapange upya bajeti zao.

"Serikali iliwataka waajiri wa sekta binafsi waongeze mishahara ya watumishi wao ili kwenda sambamba na hali ngumu ya maisha kwa watumishi wa sekta hiyo... kwa zaidi ya miaka minne watumishi wa sekta binafsi hawajawahi kuongezewa mishahara," alisema Chiligati.

Alitaja baadhi ya sababu zinazotajwa na waajiri ni fungu dogo la mishahara lililopo kwenye bajeti yao na kwamba taarifa ya serikali imekuja katika kipindi kifupi hali iliyowapa mshtuko, hasa walipotembelewa na Bodi ya Mishahara.

Kapteni Chiligati alitaja sababu nyingine kuwa ni wazalishaji wa bidhaa za nje watalazimika kuongeza bei ya bidhaa zao na kusababisha kupanda kwa gharama ya uuzaji hali itakayoporomosha soko la kazi zao nje ya nchi.

Aidha, Waziri Chiligati aliwaonya waajiri wanaowafukuza kazi watumishi wao kwa kisingizio cha kupanda kwa gharama za malipo, kuwa watapelekwa mahakamani.

Pamoja na hilo, waziri huyo aliwataka wote waliowafukuza kazi watumishi wao kuwarejesha kazini na kuendelea kuwalipa kwa viwango vya zamani hadi Januari watakapoanza kuwalipa mishahara ya nyongeza.

Chanzo: Tanzania Daima, 1/11/2007

Ina maana mpaka waziri na kamati yake waanapanga mikakati hii ya mishahara mipya walikuwa hawajajadiliana na waajiri binafsi?

Ona sasa wafanyakazi wengi wameachishwa kazi kutokana na kukurupuka huku!
Aibu!!
 
Kwanza, kunatakiwa kuwe na only one minimum wage, sio minimum ya serikali na minimum ya sekta binafsi. Minimum means the minimum amount of money that any citizen can be paid. This doesn't stop different organizations from paying higher than this. This is just the boundary, which ideally, should be based on minimum amount of money required for one to survive.

Pili, kazi ya kugombania mishahara bora zaidi katika sekta mbalimbali za uchumi ni ya vyama vya wafanyakazi na sio serikali.

Na tatu Serikali ipo kwa ajili ya kuingilia pale migogoro inapotokea kati ya wafanyakazi na waajiri. Serikali haitakiwi ichukue upande wowote bali isuluhishe bila kudictate kama ilivyofanya.

Kudictate mishahara, tena kuigawanya kwa sekta mbalimbali na kwa biashara za ukubwa mbalimbali ni UJINGA. Sasa unawaambia watu wasiwe ambitious kuexpand business zao kuepuka kubanwa na serikali? Hii itasababisha sheria kubakia vitabuni na kuleta mkanganyiko na hapo serikali kukosa nguvu. Migogoro haiwezi kwisha kwani kila wafanyakazi watadai kwanini sekta ile inapata kima cha chini juu yetu zaidi, Sisi hatuna umuhimu? nk

Serikali inatakiwa iwe transparent na ihusishe wadau wote katika kupanga mishahara/mikakati mipya na isiegemee upande wowote. Wote tunajua hivi vyama vya wafanyakazi vina historia ya kutokea juu na sio kwenye grassroots (JUWATA type). Havitakiwi kupweteka na kuitumia serikali katika kupigania haki. Wao ndio wawe mstari wa mbele kuongea na waajiri wao na sio kukimbilia serikalini kila kukicha.

Uvivu wao na kutafuta shortcut ya kuitumia serikali kupata haki zao mara zote kunasababisha vyama hivi kuwa vichekesho. Vyama hivi vinatakiwa viwe makini na realistic ili kujenga mahusiano ya kuaminika na waajiri. Hatuko kwenye enzi za Ujamaa wandugu, someni wenzetu wanafanyaje!

Shortcut aliyotumia Waziri HAIFAI.
 
Back
Top Bottom