Serikali yaagiza Watoto Ombaomba na wazazi wao kukamatwa na kisha kushtakiwa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Serikali imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri na majiji kuwakamata watoto wanaombaomba mitaani ili washtakiwe kwa mujibu wa sheria inayokataza utoro shuleni.

Agizo hilo limetolewa bungeni leo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda ambaye amesema ombaomba bado ni tatizo katika jiji la Dar es Salaam.

Kakunda alikuwa akijibu swali la Ibrahim Raza Mbunge wa Kiembe Samaki, ambaye alihoji ni lini serikali itachukua hatua kuwaondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, alisema mara nyingi ofisi ya mkuu wa mkoa imekuwa ikichukua hatua za kuondokana na tatizo hilo kwa kuwarudisha makwao.

"Mfano Septemba 2013, ombaomba 253 na watoto 135 walirejeshwa kwao, ambapo watoto 32 walirejeshwa shuleni na hii inathibitisha kuwa wapo watu wazima wanaowatumia kuomba, nawaagiza wakurugenzi kuwakamata watoto wote wanao ombaomba mitaani ili washtakiwe kwa mujibu wa sheria inayokataza utoro mashuleni,” alisema Kakunda.

Chanzo; Mwananchi
 
Kwa Tlampu kwenyewe ambako wanasema uchumi uko vyema kuna homeless na beggars sembuse tz..!
 
Omba omba ni wengi sana Mwanza wamejaa watoto wanaoomba omba pale mataa ya nyerere road na round about ya kemondo ni kero kwa kweli,ila JPM anasisitiza watu wazaane tu
 
Hahaha alafu mtu huyo huyo anakuja mbele za watu Anawaambia watanzania fyatueniii , mwisho wasiku wanafyatuliwa watoto wasio weza kulelewa na mwishowe kunakuwa na ongezeko la machokoraa mitaani

Na mtu huyo huyo alienda kule kagera badala ya kuwaambia waathirika salamu za pole ndio kwanza akawapa makavu na kusema kuwa sitoi chakula, alafu huyo huyo anakuja kukwambia fyatuaa tu,

My friend zaa kwa kadri ya uwezo ulionao kulea usizae kwa kumsikiliza mtu, ni heri watoto wawili utakaoweza kuwapa matunzo mazuri kuliko kuwa na watoto 10 ambao utashindwa kuwatunza na kuleta kizazi cha mateja , wezi na machokoraa
 
mawziri wa sasa wanjisahau sana, badala ya kujikita kutafuta suruhisho la tatizo wanazidi kuongeza tatizo.!!!!
 
Hahaha alafu mtu huyo huyo anakuja mbele za watu Anawaambia watanzania fyatueniii , mwisho wasiku wanafyatuliwa watoto wasio weza kulelewa na mwishowe kunakuwa na ongezeko la machokoraa mitaani

Na mtu huyo huyo alienda kule kagera badala ya kuwaambia waathirika salamu za pole ndio kwanza akawapa makavu na kusema kuwa sitoi chakula, alafu huyo huyo anakuja kukwambia fyatuaa tu,

My friend zaa kwa kadri ya uwezo ulionao kulea usizae kwa kumsikiliza mtu, ni heri watoto wawili utakaoweza kuwapa matunzo mazuri kuliko kuwa na watoto 10 ambao utashindwa kuwatunza na kuleta kizazi cha mateja , wezi na machokoraa
Hamkumuelewa POMẞE alisema tuzaane huku tukijitahid kufanya Kaz ili tunaowafyatua tuwatunze vzr, akasistiza Kuwa Kama ww huwez kufanya Kaz My Friend Panga uzazi,, ukitathmin kauli zake hz znahamasisha kuzaa na kufanya Kazi ili kupata Kipato chako chakukimu family na. Watt wako ,,, May ße Kama Ni discussion inatakiwa tuidiskas hii kauli ya Leo je kukamata kutasaidia ama kipi kingefanyika then kukamata kukafata ẞaada ya kile Cha awali Kushindwa kutekelezeka🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom