Serikali yaagiza waliovunja nyumba Dar watimuliwe kazi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Pia waliovunjiwa nyumba walipwe haki zao katika bei ya nyumba hizo kwa sasa

Posted Date::3/6/2008
Serikali yaagiza waliovunja nyumba Dar watimuliwe kazi
Na Kizitto Noya
Mwananchi

SERIKALI Mkoani Dar es Salaam imeagiza Mhandisi na Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, wafukuzwe kazi kwa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kusimamia ubomoaji za nyumba za baadhi ya wakazi wa Tabata Dampo.

Mkuu wa Mkoa huo Abbas Kandoro asema jana jijini Dar es salaam kuwa adhabu hiyo pia itamhusishe, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Lubuva endapo atabainika kuhusika moja kwa moja ama kwa kuamuru kufanyika au kubariki ubomoaji wa nyumba hizo.

" Nimeagiza watendaji wote wa Manispaa ya Ilala waliohusika katika zoezi hilo wafukuzwe kazi hasa Mhandisi, Mwanasheria na hata Mkurugenzi akibainika alishiriki moja kwa moja," alisema Kandoro.

Akielezea sababu za hatua hiyo kali kwa watendaji hao, Kandoro alisema imetokana na ama uzembe au kutowajibika kwao katika maamuzi yao, hivyo kusababisha uvunjaji wa haki za wakazi wa eneo hilo kutokana na nyumba zao kuvunjwa Februari 29, mwaka huu.

Alisema kitendo cha uongozi wa manispaa hiyo, kuwabomolea nyumba wakazi hao, siyo cha kiungwana na kimekiuka misingi ya haki za binadamu na utawala bora, taratibu na sheria.

Akifafanua zaidi alisema, Manispaa hiyo, ilikurupuka kuchukua hatua ya kuvunja nyumba hizo.

"Sisi kama serikali kuu hatukuwa na taarifa ya kuvunjwa nyumba hizo, tumesikia kwenye vyombo vya habari tu na baada ya kufuatilia tumegundua kulikuwa na ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu ambazo ama zilifanywa kwa makusudi au kutoelewa," alisema

Alisema uchunguzi wa kina uliofanywa na ofisi yake umebaini kuwa eneo la Tabata Dampo lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu na mtu anayejulikana kwa jina la Allied Cargo Freight, ambaye amedai kumilikishwa kihalali mwaka 2002.

" Freight Eneo hilo limeanza kuvamiwa na watu na hivyo akaamua kufungua kesi mahakamani ambako alipata haki kwamba arudishwe eneo lake na waliovamiwa wakati ule walikuwa watu 17, " alisema.

Lakini walalamikiwa wakakata rufaa Mahakama Kuu ambako mwaka 2003, chini ya Jaji Masati mahakama hiyo haikutoa haki kwa upande wowote bali iliamuru kesi hiyo irudishwe katika baraza la usuluhishi

" Tangu wakati huo hakukuwa na mtu aliyeenda kwenye baraza hilo na ilipofika Januari 28, mwaka huu mmiliki huyo alimwandikia Mkurugenzi wa Ilala kulalamika kuwa ametoa hati za makazi kwa wakazi hao, "alisema Kandoro.

Alisema ilipofika Februari 5, mwaka huu Freight alifungua kesi katika Baraza la Ardhi Ilala, kuishtaki manispaa hiyo kwa kutoa vibali hivyo vya makazi, kesi ambayo hukumu yake ilitolewa Februari 18 kwa kutaka wakazi hao waondolewe eneo hilo kwa gharama za Manispaa yenyewe.

Katika kutekeleza hukumu hiyo, Februari 27 mwaka huu Manispaa hiyo, ilipeleka notisi kwa Afisa Mtendaji wa Tabata kumtaka awatangazie wananchi hao kuondoka au kusubiri kubomolewa nyumba zao.

'Siku mbili baada ya notisi hiyo, yaani Februari 29 Manispaa ilienda kuvunja" alieleza Kandoro na kufafanua kuwa, kitendo hicho kimekiuka taratibu za kisheria zinazotaka utekelezaji wa notisi kufanywa siku 30 baada ya kutolewa.
 
Na kama ni kweli hiyo Halmashauri iliwapa hao wakaazi hati za kuishi hapo, na baadae ikagundua ilizitoa kwa makosa, bado inawajibika kurekebisha makosa hayo kwa kuwapa maeneo mengine na kuwafidia maendelezo waliyokwisha kuyafanya katika eneo hilo, licha ya kupaswa kuwapa notisi ya muda wa kutosha wa kuhama. Kwa mujibu wa maelezo hayo ya Bw Kandoro hakika manispaa imefanya blunder hasa. Pengine ni yaleyale ya kuweka wanasheria vilaza kwenye idara nyeti za serikali (imeonekana katika ofisi ya AG, mwanasheria wa serikali hakudurusu vizuri ile mikataba, yeye alikuwa anaingia tu vikaoni kukandamiza sambusa na soda, mwishoni anaweka saini)! Mwenye eneo kaishitaki Halmashauri kuwa imegawa upya eneo kwa watu wengine, mahakama imetoa hukumu kuwa watu hao waondoke kwa gharama za halmashauri (kumbuka ni halmashauri iliyoshitakiwa, si wakazi), sasa mwanasheria (nadhani kilaza huyu) wa halmashauri anawapa mabosi wake tafsiri "potofu" ya hukumu hiyo kuwa ni kubomoa nyumba za watu, anasahau ni wao halmashauri ndio waliowapa hao watu kibali cha kukaa hapo! Ameshindwa kutafsiri maneno "wahamisheni kwa gharama zenu" yalichomaanisha! Na mkurugenzi na maofisa wengine wote wakaona ni sawa! Au ndio lilelile genge la vilaza ambao vikao vya menejimenti na mambo mengine nyeti wanavichukulia kama fursa za kupata "lanchi" za bure? Sasa "lanchi", sambusa na soda zitawatokea puani, kudadadeki!
 
Hii ndio Tanzania bwana.Ilala sijui kuna nini,juzi wametangaza nafasi 2 za wanasheria wa manispaa,cha ajabu ni kuwa hizo nafasi tayari zimetengewa watoto/jamaa za watu fulani.Hata hilo tangazo ungeona lingekushangaza,halikuwa na deadline,yaani liliandikwa kuwa "Mwisho wa maombi ni tarehe _____ Februari 2008",sasa ni juu ya mwombaji kubashiri tarehe.

Ni kweli kuwa kuna tatizo kubwa sana katika idara hizi,kikubwa ni watu kufanya kazi kwa mazoea,na kwamba mtu hajui kwa nini yuko pale na/au anawajibika kwa nani.Kinachobaki ni watendaji kuvizia na kudandia semina,warsha,makongamano na upuuzi mwingine wa aina hiyo huku majukumu na maamuzi ya msingi ambayo kwayo ndo wameajiriwa yakiwashindwa.Utaona mijitu mizima na vitambi imefunga vioo ndani ya "mashangingi" kumbe kichwani uji mtupu.

Really there is a long way to go.
 
" Tangu wakati huo hakukuwa na mtu aliyeenda kwenye baraza hilo na ilipofika Januari 28, mwaka huu mmiliki huyo alimwandikia Mkurugenzi wa Ilala kulalamika kuwa ametoa hati za makazi kwa wakazi hao, "alisema Kandoro.

Mimi nadhani kuna siasa humu. Mkurugenzi anaweza kweli kutoa offer ( siyo hati) bila madiwani kuhusishwa? Mbona hii haijawekwa bayana kama kweli hizo hati zilitolewa? Hati nikimaanisha title inatolewa na wizara ya ardhi na si halmashauri. Wahusika wangesimamishwa kazi kwanza, halafu uchunguzi ufanyike. Kutokana na maamuzi ya serikali ya wilaya ( ikijumuisha madiwani) ndipo hatua ingetekelezwa. Na kama walifanya hivi kutokana na kamsukumo kutoka kwa mteja wafukuzwe na wafunguliwe mashtaka kuhusu rushwa. Ilivyo sasa, inaelekea kuna watu wanatafuta umaarufu wa kisiasa.
 
Fundi,ni kweli kuna watu wamenza kutafuta umaarufu wa kisiasa baada ya Mwakyembe (I mean Abby Kandy), kisheria ni kuwa hawezi kuwafukuza kazi bila kuwapa nafasi ya kujitetea (natural justice), cha msingi ni kuwasimamisha kazi na kisha kureview process yote ya kuhusu ubomoaji kuanzia mgogoro wa viwanja husika,nani alitoa "double allocation",na je waathirika walipewa notice ya kutoa kwa muda,nani waliengineer tukio lote na kwa nini,then ndo watoe maamuzi ya kuwafukuza au adhabu nyingine muafaka.Hapa ni Kina Abby kandy et al baada ya kuona mambo yamekwenda ndivyo sivyo ndo wanaibuka kuanza maneno yao.
 
Mimi nadhani kuna siasa humu. Mkurugenzi anaweza kweli kutoa offer ( siyo hati) bila madiwani kuhusishwa? Mbona hii haijawekwa bayana kama kweli hizo hati zilitolewa? Hati nikimaanisha title inatolewa na wizara ya ardhi na si halmashauri. Wahusika wangesimamishwa kazi kwanza, halafu uchunguzi ufanyike. Kutokana na maamuzi ya serikali ya wilaya ( ikijumuisha madiwani) ndipo hatua ingetekelezwa. Na kama walifanya hivi kutokana na kamsukumo kutoka kwa mteja wafukuzwe na wafunguliwe mashtaka kuhusu rushwa. Ilivyo sasa, inaelekea kuna watu wanatafuta umaarufu wa kisiasa.

Fundi Mchundo,

Nakubaliana na wewe hapa kuna siasa au rushwa imetumika. Taratibu za kutoka hati ni ndefu kidogo kunazia kwa mjumbe wa nyumba 10, kwenda kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa then kwa Diwani ndio zinarudi ofisi ya Arthi ya Wilaya, huko anatumwa Land officer aende huko kiwanja kilipo kuhakikisha iwapo mawe ya mipaka na alama nyingine zipo kama zinavyotakiwa kuwepo na kwamba eneo husika sio eneo la wazi n.k Ofisa wa Arthi akishahakikisha hayo ndipo anaandika ripoti na kumkabithi Mkurugenzi wa Arthi Wilaya...hapo ndipo Mkurugenzi akirithika na kila kitu anatoa Letter of Offer...sikumbuki kwa uhakika kama Hati zinaweza kutolewa Ofisi ya Arthi Wilayani.

Sasa katika process yote hiyo mpaka Hati imetolewa na bila mwenye Eneo lake kujua kuna harufu mbaya ya ukiukwaji wa taratibu za kisheria.

Out of Topic: Binafsi naona Ofisi ya Arthi Wilaya ya Kinondoni ndio yenye malalamiko makubwa na mengi kuliko Ilala, labda statistics zinaweza kuonyesha picha tofauti ila Kinondoni hakufai kabisa.
 
Mkuu Yebo Yebo, tatizo ni kuwa kwa kurupuka namna hii ndiyo tunawapa loophole wale waovu kukwepa kuajibika. Wanaenda mahakamani na serikali inaishia kuwalipa fedha kibao kwa kuwadhalilisha adding salt to injury. No doubt, Kinondoni pameoza. Ndio maana inabidi kuwa waangalifu wanapoamua kuwashughulikia. Ni lazima waovu waadhibiwe bila kuwapa nafasi ya kukwepa. taratibu zote na ushahidi ukusanywe ndio kazi ianze.
 
Nahisi harufu ya kukomoana katika sakata hili!
Kuna kitu hapa kinaendelea katika ya Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi.
Tutajua tu lakini.
 
Hata hilo tangazo ungeona lingekushangaza,halikuwa na deadline,yaani liliandikwa kuwa "Mwisho wa maombi ni tarehe _____ Februari 2008",sasa ni juu ya mwombaji kubashiri tarehe.

Kwa kweli umenichekesha sana...Ibambasi are you sure tangazo liliandikwa hivyo? sipendi kuamini
 
Chama na Serikali yake vimekosa mwelekeo, sasa wanaanza kutoa watu kafala. Hivi ni nani anayetoa lawama kwa manispaa kuhusu ujenzi holela kila kukicha kama sio serikali? hapa naona Kandoro kawahi kabla kina Zito na Mnyika hawajalifanya hili tukio kuwa ajenda. Kwi kwi kwi.
 
Alisema uchunguzi wa kina uliofanywa na ofisi yake umebaini kuwa eneo la Tabata Dampo lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu na mtu anayejulikana kwa jina la Allied Cargo Freight, ambaye amedai kumilikishwa kihalali mwaka 2002.

Mimi ningependa kujua huyu mheshimiwa alipewa vipi pale mahala? Matumizi ya hiyo sehemu kabla ya kupewa yalikuwa nini? Na nani aliyebadili matumizi na kumpa huyu jamaa? Kama lilikuwa dampo uchunguzi gani umefanyika kuhakikisha kuwa hakuna sumu katika eneo hilo? Hao wenye kiwanja, manispaa, wana sehemu ngapi kwa ajili ya wananchi (public spaces) kiasi cha wao kutoa hiki kiwanja? Na kadhalika na kadhalika na kadhalika!
 
Hao watu wanao amriwa kufukuzwa jukwaani hata sielewi inakuwaje maana baadaye watakuja na madai ya natural justice na kushinda kesi.Mimi nauliza ndugu Mkuu wa Mkoa , the damage inflicted kwa walalahoi ni kubwa . Wewe unasema wafukuzwe kazi then ndiyo imetoka na si kusimama Mahakamani kujibu mashitaka ya kuharibu mali za watu ?
 
109734zxziq4.jpg

A displaced woman lies on the ground yesterday as she feeds her baby in a tent donated by Dar es Salaam Regional Commissioner Abbas Kandoro. She is from one of an estimated 500 families displaced when 96 houses were demolished at Tabata Mandela.

Mtu wa kufukuzwa ni nani? Mkuu wa wilaya au Mkoa? Ilikuwaje hadi nyumba kiasi hicho zivunjwe bila wao kufahamu kinachoendelea? wanakuja kujitetea kwa kuwasaidia waliopoteza mali zao? Au kuamuru mlolongo wa wafanyakazi wa mgazi za chini wafukuzwe.
 
Chama na Serikali yake vimekosa mwelekeo, sasa wanaanza kutoa watu kafala. Hivi ni nani anayetoa lawama kwa manispaa kuhusu ujenzi holela kila kukicha kama sio serikali? hapa naona Kandoro kawahi kabla kina Zito na Mnyika hawajalifanya hili tukio kuwa ajenda. Kwi kwi kwi.

Utawala huo dhaifu Sasa hivi umeshaondoka Sasa ni mwendo wa kanyaga twende, utavunjiwa hata ukimbilie Mahakamani kuomba stop order

Jana Tanesco wameambiwa wasiende Mapumziko ya Sikukuu kabla hawajasafisha pale Ubungo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom