Serikali yaagiza wakandarasi wote waliositisha ujenzi wa miundombinu kuanza kazi mara moja

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Serikali imeagiza wakandarasi wote waliositisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini kuanza kazi mara moja baada ya kufanikiwa kuwalipa madeni yao zaidi ya shillingi billion 400 kati ya deni la trilion 1.2 lililoachwa na serikali ya awamu ya nne.
Agizo hilo limetolewa na waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof, Makame Mbarawa mkoani Morogoro ambapo amesema katika kipindi cha miezi mitatu serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuwalipa wakandarasi kiasi cha shiling bilion 400 ambapo mpaka kufikia mwezi juni mwaka huu wakandarasi wote watakuwa wamelipwa fedha zao, huku agizo hilo likienda sambamba na kumtaka mkandarasi wa barabara ya Dakawa, Turiani kuendelea na ujenzi wa barabara.

Aidha katika hatua nyingine waziri Mbarawa akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro akiambatana na naibu wazi wake Mhandisi Edwin Ngonyani wametembelea katika karakana ya TRL ambako inafanyika na kuzungumza na wafanyakazi ambapo alikuwa mbogo kwa kuwaonya wale wote watakao bainika kutengeneza ajali za treni kwa makudi serikali haitawavumilia, watafukuzwa kazi sambamba na kufikishwa mahakani.

Nao wafanyakazi wa shirika hilo wamotoa malalamiko yao kwa waziri huyo wakidai serikali kuwasahau kwa kuimarisha miundo mbinu ikiwa ni pamoja na stahiki zao na kusababisha kuishi maisha ya kiumaskini.
Waziri Mbarawa katika ziara yake yakukagua miradi mbalimbali alitembelea barabara ya Magole Turiani, kitio cha mawasiliano cha Halotel, karakana ya reli pamoja na kituo cha mizani cha Mikese mkoani Morogoro.
 
Huko ndio kukurupuka na kutotumia busara zaidi ni kutafuta sifa kutoka kwa wananchi hivyo kupelekea kuiingiza serikali ktk hasara,unawezaje kumuamlisha mkandarasi leo hii aaendelee kuweka kifusi barabarani wakati mvua ndio kwanza zimeanza kunyesha?matokeo yake hivyo vifusi vitasombwa na maji
 
B

Bila kukurupuka mambo hayaendi.
 
Teeeeeeeeh teeeeeeeeh teeeeeeeeeh, ukishangaa ya mkwere utayaona ya ngosha
Unajua mabadiliko wewe? Kama unataka kufanya mabadiliko lazima kuna kuvunja taratibu na kuna kukurupuka. Siku hazigandi ukijifanya mshua ati usikurupuke ndo yanadoda. Hivyo Magu yupo sahihi na kundi lake
 
Kwahiyo unakili na kuutangazia umma wa watanzania kuwa magu na serikali ni wakurupukaji na kupelekea taifa kupata hasara?
 
Hayo ni ya kwako. Nasema hata akikurupuka ni ajali kazini. Kwa mtu uliye Genuine lazima uangalie kosa limetendeka kimakusudi au bahati mbaya. Kukurupuka kama kupo ni bahati mbaya. Hakuna aliye mkamilifu chini ya jua
 
Ni bahati mbaya?unataka kusema hao viongozi au waziri wa ujenzi hajui kuwa kipindi hiki ni cha mvua za masika?leo hii umwambie mkandarasi wa ujenzi wa barabara aweke kifusi barabarani anakuwa anatumia busara kweli?
 
Hivi unadhani tamko la Waziri ni lazima litekelezwe bil kuangalia hiyo kitu? Yeye ametoa tamko na si Contractor kufanya kazi kama robot. Afterall kuna sehemu hakuna mvua wake-up
 
Ukanda wa huku ifakara ni mvua tupu hiyo haina ubishi na hilo tangazo amelitoa kwa pia mkandarasi anaye endelea na barabara huku sehemu za ifakara,
 
Hivi huyu Waziri haoni hizi mvua?
Au ndo anataka ale asilimia kadhaaa?
 
Ukanda wa huku ifakara ni mvua tupu hiyo haina ubishi na hilo tangazo amelitoa kwa pia mkandarasi anaye endelea na barabara huku sehemu za ifakara,
Kwani kasema waweke vifusi? Kwani hakuna kazi zinazoweza kufanywa bila vifusi? Kutekeleza agizo bila kutumia akili yako ni UNAFIKI na mtu huyo hafai kuwa kiongozi wa sehemu husika.
 
Kwahiyo unatuhakikishia kuwa aliye toa agizo hilo hafai kuwa kiongozi?
 
Vibarabara vyenyewe ndio hivyo vya BRT

Hehehe my foot ni bora mkagawana hizo pesa ili ijulikane moja kuwa hamko tayari labda baada ya miaka 4000 mbele
 
Ukanda wa huku ifakara ni mvua tupu hiyo haina ubishi na hilo tangazo amelitoa kwa pia mkandarasi anaye endelea na barabara huku sehemu za ifakara,
Mkuu barabara ina vitu vingi kuna kazi zinaweza kufanyika hata wakati wa mvua, mfano structures, pia lazima mkandarasi awepo site muda wote kuhakikisha diversion zinapitika.
 
Back
Top Bottom