Serikali yaagiza Shule kuwa na Ofisi za matatizo ya saikolojia kwa Wanafunzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Prof. Ndalichako amewataka Walimu Wakuu Shule za Msingi kufungua Ofisi maalum za kuwasikiliza Wanafunzi wenye matatizo ya kisaikolojia “Wanafunzi wote hawawezi kuwa kwenye hali sawa, fungueni ofisi Wanafunzi wafahamu wamuone nani wakiwa na vitu vya kifamilia vinawatatiza.”

“Hii itasaidia kupunguza hata changamoto za Wasichana, fungueni hizo sehemu za ushauri/unasihi, Watoto wana changamoto na hawana Watu wa kuwaeleza matokeo yake wanaacha Shule sababu ya shida ndogondogo ambazo wangepata sehemu ya kuzisemea wangepona” - Prof. Joyce Ndalichako.
 
Muajiri wataalamu wa ushauri nasaha sasa sio mnang'ang'ana walimu ndiyo wawe washauri nasaha maana mmezoea!

Wataalamu wa maabara hamuajiri mnatumia walimu,wahasibu hamujiri mnatumia walimu tena badala ya mkuu washule mngeajiri meneja wa shule kabisa huyohuyo awe mshauri nasaha mjali professional za watu na mlipe vizuri msilete janjajanja.
 
Prof. Ndalichako amewataka Walimu Wakuu Shule za Msingi kufungua Ofisi maalum za kuwasikiliza Wanafunzi wenye matatizo ya kisaikolojia “Wanafunzi wote hawawezi kuwa kwenye hali sawa, fungueni ofisi Wanafunzi wafahamu wamuone nani wakiwa na vitu vya kifamilia vinawatatiza.”

“Hii itasaidia kupunguza hata changamoto za Wasichana, fungueni hizo sehemu za ushauri/unasihi, Watoto wana changamoto na hawana Watu wa kuwaeleza matokeo yake wanaacha Shule sababu ya shida ndogondogo ambazo wangepata sehemu ya kuzisemea wangepona” - Prof. Joyce Ndalichako.
Toeni ajira hizo Sasa
 
Prof. Ndalichako amewataka Walimu Wakuu Shule za Msingi kufungua Ofisi maalum za kuwasikiliza Wanafunzi wenye matatizo ya kisaikolojia “Wanafunzi wote hawawezi kuwa kwenye hali sawa, fungueni ofisi Wanafunzi wafahamu wamuone nani wakiwa na vitu vya kifamilia vinawatatiza.”....
Sijui tunaelekea wapi? Yaani wameshindwa kuajiri waalimu ni wanasaikolojia wataweza? Au ndo kuongezea yale masomo matatu na ushauri juu?
 
Halafu watalipwa na nani? Maana hao Walimu tu wanalipwa kwa manati na hawatoshi, labda shule za serikali wao ndio waongeze hiyo kada.
 
Back
Top Bottom