Serikali yaagiza hospitali zote nchini kuwa na ICU za watoto wachanga

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameziagiza Hospitali za rufaa zote nchini kuwa na ICU kwaajili ya watoto wachanga ili kupunguza vifo vifo vyao.

Waziri Ummy amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

Waziri Ummy ameagiza hayo kupitia kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo kuwa ahakikishe watoto wachanga lazima wawe na ICU yao ili kuhakikisha vifo vya Watoto wachanga vinapungua nchini. "Watoto wachanga wagonjwa, wawe na ICU yao, lengo letu kama Serikali ni kupunguza Vifo vya Watoto wachanga, kwasababu tukipunguza vifo vya Watoto wachanga, tutakuwa tumepunguza vifo vya Watoto wanye umri wa chini ya miaka mitano," alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa karibu 40% ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila Watoto 100, Watoto 40% ni Wachanga, hivyo Serikali inaendelea kuchukua jitihada za makusudi ili kupunguza vifo hivi, ikiwemo kusisitiza kila Hospitali nchini kuwa na ICU. "Karibu 40% ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila Watoto 100, Watoto 40% ni Wachanga, kwahiyo Daktari ni lazima tulifanyie kazi agizo hilo," alisema Waziri Ummy.

Licha ya changamoto alizokutana nazo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatarajia kujenga jengo mahususi kwaajili ya huduma za Dharura katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini ili kuokoa maisha ya wagonjwa, hasa waliopata ajali. "Nafurahi kusema, Serikali imeahapata fedha kwahiyo tutakuwa na jengo mahususi kwaajili ya huduma za Dharura na wagonjwa wa ajali, na hii tunataka iwe katika Hospitali za Rufaa za Mikoa zote ili mgonjwa aweze kuokolewa maisha muda mfupi anapofika Hospitali," alisema Waziri Ummy.

Pia, Waziri Ummy ameridhishwa kwa kiasi kikubwa juu ya hali ya upatikanaji wa dawa nchini, huku akiwatoa hofu Mwananchi kuwa Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ina dawa zakutosha.
 
Wayoto ndio kitu gani
 
Back
Top Bottom