Serikali yaagiza hospitali, zahanati na Vituo vya Afya vya Umma, viweke watu maalum kwa ajili ya kuwahudumia wazee

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Agizo hilo limetolewa 23 Mei 2021, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma.

Dk. Gwajima aliagiza watu hao wawe na sare maalum, zitakazowawezesha wazee kuwatambua. “Kila kituo lazima kiwe na nesi mmoja, afisa ustawi wa jamii pamoja na daktari aliyepangwa zamu na lazima wavae sare, ambayo itamtambulisha na imeandikwa ‘Mzee ni Tunu, Tunakupenda, Tunakuheshimu’,” alisema Dk. Gwajima.

Aidha, Dkt. Gwajima aliagiza vituo hivyo kuweka mabango yanayoelekeza mahali wazee watapata huduma.

“Lazima kuweka mabango yanayomuelekeza au kumuongoza mzee, wapi atapata huduma anazozihitaji na ambayo yameandikwa “Mpishe Mzee apate huduma kwanza,” alisema Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima alisema wizara yake imeanza kufanya ufuatiliaji wa maelekezo hayo, ili kuboresha huduma za matibabu kwa wazee, kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Aidha, Dkt. Gwajima alisema wizara hiyo iko mbioni kutengeneza muongozo rasmi, ambao utaweka uwiano wa utekelezaji maagizo hayo, katika hospitali zote nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Vivian Wonanji, alisema idara yake imeandaa mkakati wa utoaji huduma kwa wazee wa miaka kumi. Ifikapo Juni 2021 itaanza kuandaa mpango wa utekelezaji wake.

Dkt. Wonanji alisema mpango mkakati huo utakuwa na mambo mbalimbali, yakiwemo kuzalisha wataalam wa kutoa huduma za wazee.

“Kama tunavyofahamu wazee wanahitaji mambo mengi, ikiwemo masuala ya lishe na utengamao. Hivyo mkakati huo utakua na maono muhimu, ambayo yatasaidia kuboresha huduma za wazee nchini,” alisema Dk. Wonanji.

Chanzo: Mwanahalisionline
 
Ujinga mwingine mzigo huyo mama hajielew atoe ajira izo watu wakafanye iyo kaz anayotaka.

Watumish hawatosh wa kuwatenga kwa ajili ya wazee tu.
 
Huyu Mama huwa simwelewi elewi,humo kichwani mwake sijui Kuna nini,anaongea utadhani mtu aliyesomea ulaya,hapa nilipo zahanati yangu ina wahudumu watatu,sasa hao watu anaotaka wahudumie wazee watatoka wapi?

Bure kabisa huyu mama
 
Serikali yetu SIKIVU ,ADHIMU NA BORA.....

Kongole kwake mh.Waziri Dr.Gwajima!!

Kongole mh.SSH!!

#KaziInaendelea👍👊🙏
 
Huyu Mama huwa simwelewi elewi,humo kichwani mwake sijui Kuna nini,anaongea utadhani mtu aliyesomea ulaya,hapa nilipo zahanati yangu ina wahudumu watatu,sasa hao watu anaotaka wahudumie wazee watatoka wapi?

Bure kabisa huyu mama
Zitaanza vile vituo vikubwa na Hospitali zenye WAHUDUMU WENGI....

#KaziInaendelea
 
ambayo itamtambulisha na imeandikwa ‘Mzee ni Tunu, Tunakupenda, Tunakuheshimu’,” alisema Dk. Gwajima.
Wewe Mama unahitilafu kichwani, hayo maneno ndiyo yanamtibu mzee? Kuna sababu gani kuandika porojo kwenye sare wakati hujaona namna wazee wanavyohangaika huko hospitali? Enzi za meneno ya lambishalambisha zilishapita, hizi ni zama za vitendo zaidi, hayo maneno yako ni siasa za kipuuzi kabisa hazina tija
 
Safari ya mabadiliko CHANYA huanza na hatua moja....

MANENO hayo yakitafsiriwa KIVITENDO hakika Dr.Gwajima ataacha ALAMA....

#KaziIendelee
 
Zitaanza vile vituo vikubwa na Hospitali zenye WAHUDUMU WENGI....

#KaziInaendelea
Mkuu kumbuka kule mwambao wa ziwa Tanganyika kuna wakati baadhi ya vituo vya afya zilitajwa kuwa na nurse mmoja tu hakuna mganga wala hao maafisa anaowataja
 
Ni kweli usemalo mkuu wangu ila kumbuka hatua stahiki zimechukuliwa....

DIRISHA la TAMISEMI la kuajiri WATAALAMU WA AFYA 2000 naa limefungwa usiku wa kuamkia leo...

Na lile la WIZARA YA AFYA la wale 400 naa litafungwa kesho tarehe 25 saa 9 alasiri!!!

Lakini changamoto iliyopo pamoja na ajira mpya kuwepo watumishi wengi hawaendi kwenye vituo hivyo vya pembezoni kwasababu mazingira ya kazi ni duni mno, nikupe mfano mmoja wa shule moja ya A level ilianzishwa maeneo hayo mwaka jana au mwaka juzi, shule haikuwa na walimu, wanafunzi waliopelekwa kusoma kidato cha tano wakaanza kujenga madarasa wao, wanafunzi wa kike wanasomba matofari wakiume wanajenga wakisaidiana na fundi kutoka mtaani, very likely hawa wa afya wakakutana na changamoto za aina hiyo au zaidi ya hapo.
 
Nilifikiri ataanza na swala bima za afya kwa wazee,sasa hayo maneno yatasaidia nini kama hakuna fungu maalum lilotengwa kwa ajili ya huduma za afya kwa wazee
 
Uyu mama km sio msomi vile anaongea pumba always anajiongelesha mambo ya kufurahisha jukwaa yaani siku mkeka ukicheza nae nitafurahi sana nakereka nae sana amebeba dhamana kubwa af anakua mpuuzi mpuuzi.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom