Serikali yaagiza Halmashauri Nchini kujenga vituo vya kupumzikia watoto sokoni

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Serikali yaagiza halmashauri nchini kujenga vituo vya kupumzikia watoto sokoni

SERIKALI imeziagiza halmashauri nchini kujenga vituo vya kupumzikia watoto katika masoko yote ili kuwaondolea adha wanawake ya kunyonyesha wakati wakifanya biashara zao.

Agizo hilo linakuja ikiwa halmashauri ya Jiji la Mwanza imeshindwa kutoa fedha za kukamilisha ujenzi wa soko la Mirongo na kituo cha kupumzikia wanawake, licha ya wadau wa maendeleo kutoa fedha za awali za ujenzi.

Amesema halmashauri hizo endapo watajenga vituo maalumu vya kupumzikia watoto ili kuwapa nafasi wanawake wenye watoto kufanya shughuli zao kwa urahisi zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu mkuu Wizara ya Afya Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu wakati alipotembelea soko la kiloleli wilayani Ilemela.

Amesema halmashauri nyingine zinapaswa kuiga mfano wa soko la kiloleli, ambalo limejengwa na wadau wa maendeleo wakiwemo Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanawake na wasichana la Kivulini.

Amesema ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona wanawake wakifanya shughuli zao wakiwa na watoto mgongoni kitendo ambacho alizitaka halmashauri hizo kujenga vituo vya kupumzikia watoto na wanawake.

"Mlinzi wa kwanza wa jamii ni mwanamke, watoto wakizaliwa hata wakiwa tumboni akina ***** ndio wanawalea, tumeona leo hapa (Kiloleli) limejengwa soko lenye eneo la kupumzikia watoto.

"Ili wakina mama hawa watimize wajibu wao wakufanya biashara zao, tumeona mmeanza kujenga soko hapa na mimi nitakuwa balozi wenu popote pale nitakapopita nitawaambia wajifunze hapa Kiloleli," amesema DK. Jingu.

Hata hivyo, DK. Jingu amelipongeza Shirika lisilo la kiserikali la Kivulini ambalo limeshirikiana na uongozi wa Manispaa Ilemela kukamilisha ujenzi wa soko hilo huku akiliomba shirika hilo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufanya shunguli za maendeleo.

Mkurugenzi wa Shirika hilo la Kivulini Yasin Ally, amesema wanawake zaidi ya asilimia 60 ndio wanaofanya shughuli ndogondogo za ujasiliamali katika masoko mengi mkoa wa Mwanza.

Amesema mazingira wanayofanyia biashara zao zilikuwa ni changamoto kubwa kutokana na kuambatana na watoto wao mgongoni jambo ambalo lilikuwa ni hatari zaidi kwao na kwa watoto wao.

Ally amesema kutokana na hali hiyo, iliwalazimu kuja na wazo la kujenga soko hilo, kituo cha kupumzikia na kunyonyeshea akina mama na kituo cha daladala ambavyo vitawasaidia kufanya biashara zao kwa mazingira rafiki.

"Ujenzi wa soko hilo linaenda kutoa mfano wa namna ambavyo utekelezaji wa agizo la Rais Dk John Magufuli kuboresha mazingira ya wafanyabiashara inavyotakiwa kuja na ubunifu wa masoko," amesema Ally.

Afisa maendeleo ya Jamii mwandmaizi Manispaa ya Ilemela Raphael Mfuru, amesema maeneo yaliyoboreshwa ni soko, ujenzi wa kituo cha kupumzikia watoto, kituo cha daladala na vyoo vya kisasa.

Amesema soko hilo la kisasa litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara wadogo 120 hususani ni wanawake wanaouza ndizi.

Ujenzi wa soko hilo ambalo limekamilika umegharimu kiasi cha Tsh. 152 na sasa kilichobaki katika soko hilo ni kugawanya vizimba kwa wafangabiashara.

Mwisho
IMG20200824091635.jpg
IMG20200824092114.jpg
IMG20200824093228.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom