Serikali Yaagiza Bajaji: Hapo Inakuwa Je?

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
683
115
Jamani nilikuwa nasikiliza radio maria kutoka magazetini nikasikia habari ya kushangaza sana. Yaani serikali imeamua kuagiza Bajaji badala ya Ambulace kubebea wagonjwa! Jamani sijui nyie mnnaona je mimi naona ni kichekesho jamani. Inanikumbusha mwaka 2004 nilienda Lindi nikakuta jamaa anabeba Maiti na baiskeli!

Hapo inakuwa je kuwa mama mjamzito anabebwa na Bajaji? nadhani bajaji sio salama hata kubeba abiria wa kawaida tuu labda zitumiwe kusambaza bidhaa kama sigara na maziwa.

Yaani serikali inapata pesa za kununua mashangingi inashindwa kununua Ambulace? Jamani natamani kulia hivi mgonjwa wako yupo kwenye Bajaji inaruka ruka kumwahisha hospitala huku katundikiwa dripi sijui inakuwa je jamana naona na lose temper hapa sasa.
 
Judy

Senior Member
Aug 13, 2007
191
1
EE Mungu tusaidie. hivi jamani haya ni kweli hebu tuletee hata hilo gazeti uweke hapa tujue nani kasema haya. na kama ni kweli basi hii nchi inaongozwa na wendawazimu nba sijui hata mishipa ya aibu ishawatoka. Hawana haya jamani, tuwafanyeje hawa mbona wameshindikana kama ngoma?
 
Kasana

JF-Expert Member
Apr 3, 2007
415
27
Jamani natamani kulia hivi mgonjwa wako yupo kwenye Bajaji inaruka ruka kumwahisha hospitala huku katundikiwa dripi

Hapa umenichekesha sana...., na zile barabara zetu za vumbi/mchanga.

Anyway, saa nyingine ukitafakari vizuri, zinaweza kuleta ahueni kwa rufaa zinazotoka zahanati kwenda vituo vya afya.
Hali halisi ya mikoani wagonjwa/wajawazito wanabebwa kwenye baiskeli. Kuwepo kwa bajaji kwa kiasi fulani kunaweza kusaidia.

Hata hicho kidogo kikipatikana, kitasaidia refferals za hapa na pale.Inawezekana pia zitakuwa modified kuhimili njia za huko zinakolengwa kupelekwa.

Ambulance ni ghali na pia logistics zake ni tatizo, (mafuta, maintanance na pia matumizi yasiyosahihi kwa watendaji wetu.
 
Mkuu hayo mashangingi ya wakubwa kwani ni rahisi? unajua yana CC 4500? kwa hiyo mzee nadhani tatizo hapa ni vipaumbele tuu mkuu.
 
Mnhenwa Ndege

JF-Expert Member
Dec 5, 2007
242
19
serikali inajaribu kupunguza gharama na vilevile kuwafikia watu wengi, basi kama ni hivyo viongozi wa juu pia wapewe magari aina Land Rover 109 pia ni cost efficient and effective, inadumu muda mrefu na wangefanya safari zao kudumu hata kwa vipindi viwili vya bunge.
 
MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,143
707
1. Huwezi kuwapa wakurugenzi wote- na hata walio tu ucharwa mashangingi ya 100m each- halafu unasema serikali haina pesa- Health Centres zipewe Bajaji za laki 9. Priority setting- we give kipaumbele kwa elites wachache wa serikali- au kutoa kipaumbele magari ya ambulance kwa watu wa vijijini!

2. Shangingi moja ni Bajaji 100! Je mno hapo?
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom