Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,850
Serikali ya Zimbabwe inayoongozwa na rais mkongwe Robert Mugabe imetoa taarifa ikikanusha uvumi kuwa rais huyo mwenye umri wa miaka 92 alizirai na kufa akiwa kwenye likizo ya mwisho wa mwaka.
Jarida la Herald lililoko nchini Zimbabwe lilimnukuu George Cheramba, msemaji wa serikali, akisema kuwa imekuwa jambo la kawaida watu kueneza uvumi kuhusu afya wa rais huyo mkongwe kila baada ya likizo yake ya mwisho ya mwaka. Uvumi kuhusu alipo Mugabe ulianza kuenea katika mitandao ya jamii mapema hii wiki baada ya rais huyo kukosa kuonekana tangu siku ya krismasi.
Mugabe ambaye alizaliwa mwaka wa 1924 ndiye rais mkongwe zaidi duniani na ameripotiwa kuenda Singapore mara nyingi kwa matibabu ya macho, huku ripoti zingine ambazo bado hazijadhibitishwa zikisema kuwa anaugua saratani ya kibofu.
Rais Mugabe ameongoza Zimbabwe kwa zaidi ya miongo miwili, tangu mwaka wa 1980. Huku hayo yakijiri, wenyeji wa kijiji cha Masvingo alikozaliwa Mugabe wanaendelea kuandaa karamu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa mwezi ujao.
Chanzo: BBC

Last edited by a moderator: