Serikali ya Zimbabwe inastahili kuongezewa vikwazo, ni Serikali katili kweli kweli

..siyo kweli.

..labda wawe wanafanya vurugu na kuharibu mali.

..na hawapigi waandamanaji kama vile ni wanyama.

Kuna nchi chache sana zinazoheshimu haki za binadamu. Haya mataifa makubwa yanaongoza kwa kuzikiuka.
Sitetei ukatili wa watu wasio na hatia. Nashangaa sana tunapotaka kufanya reference point ni za hao wanaotupigia kelele.
 
Rais wao anafahamika kama Black Mamba. Unadhani uongozi wake utakuwa wa aina gani kama sio wa kibabe babe ?
 
..oneni Polisi wa Zimbabwe wanavyopiga wananchi wao.

..wanapiga hata wanawake wenye umri wa mama zao.

..kwanini Tz tuwe mstari wa mbele kutetea serikali katili kama ya Zimbabwe?


Uliwahi ona wapi shetani anawaonea huruma watu? siku zote shetani anamtetea shetani mwenzake
 
Vikwazo ni tools za kuamsha waliolala waamke wachukue hatua kuufurusha mfumo kandamizi unaovunja haki za watu.Viongozi wa kiafrica bila mfumo wowote wa kuwadhibiti ugeuka laana Kwa wanaowatawala Maana wako bize kukomoa watu kuliko kuleta maendeleo. Thus trump na Putin wanawadharau sana watawala wa kiafrica na Kuwaita wezi wanaibia wanyonge wanaficha ulaya.
Zimbabwe ina vikwazo kwa miongo mitatu,na mpaka sasa hao waliolala ndo kwanza usingizi ndo umekolea.

Mugabe hajatoka sababu ya vikwazo bali issue ya kutaka kumrithisha urais mkewe.
ZANU PF bado ni mvinyo ule ule Ila chupa ndo imebadilishwa.

Hivyo vikwazo vimeua maelfu and no changes na hata matumaini ya mabadiliko hamna.

Kurudia kitu kilekile kwa namna ileile huku ukitegemea matokeo tofauti is what is called Insanity.
 
Bavicha huwa nawaonea huruma!

Hivi huwa mnafikiriaga kweli katika kutenda mambo yenu? Si mlishangilia Mugabe kuondolewa?

Nenda Libya ile ya Gadafi mliyeshamgilia sana kuondolewa kwake ukaone. Sasa hivi wanakula democrasia waliyoitamani toka kwa mzungu.
Ndege ishaachiwa sauzi?
 
yaani upinzani kwa afrika ulipaswa uwepo miaka kama 300 ijayo.

ukichunguza sana upinzani wao hauna dira, yaani sera ya january haiwezi kusimamiwa bila kubadilika angalau hadi june. likijitokeza tukio kama march wao hujitenga na dira/sera zao za toka january na kudakia tukio jipya, bora tu wamesikika.

kwa mujibu wa taratibu za habari; hii habari inapoteza credibility maana haijazingatia vigezo vyote vya kuitwa habari na inabaki kuwa majungu. hata kama demokrasia haijakomaa afrika sidhani km serikali kupitia hao polisi walianza kushambulia na kugawa virungu kiholela pasna kutekeleza adhabu ya ukiukwaji wa sheria.

ndiyo, tunatambua fahiwa ya uhuru lakini nao wajue upo utaratibu na sheria za nchi.

kwa mchafukoge huo nilichagua kutokuwa sehemu ya chama kiwacho chochote japo wananzuoni walikemea kuegea neutral!!

Ishu sio kuwashambulia,mwanaume mzima unampiga vipi mwanamke tena sawa na mama yako mzazi wengine uonekana walienda shopping, wengine awajui hata Maana ya maandamano wanajipitia vyao au wamekutwa eneo La biashara zao
 
Hakuna Serikali duniani isiyo fanya hivyo ukikaidi amri yake. Amerika ndiyo zaidi

Unatetea kwakuwa hayo pia yako hapa nchini kwetu. Halafu eti viongozi wetu wanataka Zimbabwe iondolewe vikwazo. Wekea vikwazo hiyo nchi mpaka akili iwakae vizuri ili yotekee machafuko hao viongozi wenye uchu wa madaraka watolewe haraka sana.
 
Bavicha huwa nawaonea huruma!

Hivi huwa mnafikiriaga kweli katika kutenda mambo yenu? Si mlishangilia Mugabe kuondolewa?

Nenda Libya ile ya Gadafi mliyeshamgilia sana kuondolewa kwake ukaone. Sasa hivi wanakula democrasia waliyoitamani toka kwa mzungu.

Watu walishangilia Mugabe kuondolewa kwakuwa ni katili kama jiwe, na pia wanaunga mkono huyu mpuuzi mwingine anachokifanya awekewe vikwazo. Libya kinachoendelea kisingetokea iwapo Gaddafi angeachia madaraka kwa amani.
 
Hawa polisi ni kama vijibwa vinavyotumwa kulinda udikteta tu!

Wakishalipwa vihela uchwara na hao masultan wao wanawehuka!

Ukijumlisha na ujinga walio nao vichwani wanageuka vijibwa vitiifu pasipo kufahamu wanatumika tu!

Ukiwa mwanasiasa Afrika, ni rahisi mno kuwaendesha polisi jinsi unavyotaka!

Unawaswitch tu kwa remote kama misukule!
 
Hivyo vikwazo ndo vinawapiga mara dufu kuliko hata hicho kipigo cha polisi.

Mtu anayefikiri vikwazo ndo suluhisho huwa napata tabu kuelewa utimamu wa akili yake.

Kwenye hizi nchi zetu anayebeba msalaba wa vikwazo ni huyo mwananchi wa kawaida zaidi kuliko waliosababisha matatizo.

Maisha yakiwa magumu lazima wananchi watasimama kidete kuondoa huo ushenzi. Wekea vikwazo Zimbabwe ili viongozi walevi wa madaraka wakae pembeni.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hawa polisi ni kama vijibwa vinavyotumwa kulinda udikteta tu!

Wakishalipwa vihela uchwara na hao masultan wao wanawehuka!

Ukijumlisha na ujinga walio nao vichwani wanageuka vijibwa vitiifu pasipo kufahamu wanatumika tu!

Ukiwa mwanasiasa Afrika, ni rahisi mno kuwaendesha polisi jinsi unavyotaka!

Unawaswitch tu kwa remote kama misukule!

Thus kuna kazi ukiwa msomi aliyeelimika ni heri ukalime bamia utaishi kuliko kutumika kuumiza watu.Kazi ya polisi ni kulinda maslai ya wanasiasa Kwa ujira wa pipi.Polisi nao upiga watu kuondoa stress.
 
Maisha yakiwa magumu lazima wananchi watasimama kidete kuondoa huo ushenzi. Wekea vikwazo Zimbabwe ili viongozi walevi wa madaraka wakae pembeni.

Ile nchi ilikuwa vizuri sana kiuchumi ajira tele,mzunguko wa pesa tele,biashara zinatoka kila mmoja anapata pesa ni speed yake tu kuisaka.Ilipokabidhiwa Kwa kibabu kila kitu kikawa hovyo hovyo huku kikitumbua Kwa kuwasomesha no watu wake.
 
Back
Top Bottom