Serikali ya Zanzibar yatetea Oil Tankers za Iran!!! Yasema iko tayari kuipa Iran Bendera za Zanzibar

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Serikali ya Zanzibar imesema haina kosa kusajiri hizo meli na kupeperusha bendera za Tanzania kwa sababu Zanzibar ni sehemu ya Muungano hivyo Meli hizo kupeperusha bendera ya Tanzania ni sawa.

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zenj bwana Hamad Masoud Hamad anasema kama watanzania tunaona hatari hizo meli kupeperusha bendera ya Tanzania wako tayari kuwapa wa Irani hao bendera za Zanzibar.

Serikali pia ikasema kuwa Makam wa Rais wa Iran aliitembelea zanzibar katika kuhakikisha kuwa anaimarisha uhusiano kati ya Zanzibr na Iran........na serikali ikaahidi kuwa haitajuhusisha na mgogoro kati ya Iran na nchi za Magharibi.

Wazanzibari nao wameunga mkono huo msimamo kwa kusema kuwa sisi kujikomba kwetu kwa wamarekani na uingereza kusisababishe Seriakali kujikomba kwa Tannganyika katika kufanya urafiki na nchi zingine.

Pia katika hali ambayo mimi binafsi sielewi bendera ya Tanzania inaitwa bendera ya 'Mrima" Hebu angalia response za Wazenji hapa wanavyosema...........

"Rocket 01/07/2012 kwa 12:27 mu · Ingia kujibu
Ikiwa sheria ya usajili ni ya Zanzibar, inakuwaje wanaipeperushia bendera ya Mrima. Hawa watu sijui wakoje. Sheria inahusu Zanzibar, lakini wanaipeperusha ya Mrima sasa ina maana gani kutetea waziri wazir wa Zanzibar ikiwa ameruhusu bendera ya Mrima.

Nina hakika wataipachua madama mjomba obama kashatia mdomo wake na vyombo vya habari kama Bloomberg kutangaza kwa domo pana"

Mwingine huyu "
Ghalib 01/07/2012 kwa 12:38 um · Ingia kujibu

"Hapa kweli Hamad masoud kaenda mchomo,inakuwaje meli isajiliwe na zanzibar government ikisha wapewe bendera ya mrima ? Ujinga ulioje huu? Wapeni flag yetu wapeperushe acheni siasa mbovu zanzibar ni nchi, ndani ya bendera ya Znz kuna bendera ya Tz bado haitoshi?
Angalieni ujinga mwengine uliwahi kufanyika,rais wa zanzibar alienda Uturuki akaekewa bendera ya Tz wakati alitakiwa aekewa bendera ya Zanzibar,nafikiri ziara hio ilikuwa last year,ujinga mtupu"

Ghalib tena kaongeza nyingine hiiii

"Raza ameshawambia wajumbe wenziwe kuwa watanganyika washashiba tuacheni sie wenye njaa,tunataka mabara bara na mengineyo ya miundo mbinu hata katika wizara ya afya na elimu,sisi tunanjaa,ndo mana watanganyika wanatuekea vikwazo wao wameshiba kwa misaada yetu,basi na hayo mafuta wacha na sisi tuoge na tunywe,wapeni bendera yetu wapeperushe"

Kwa hili wadau mnisaidie kwa nini bendera ya TZ inaitwa "Mrima" pia msimamo wa Zanzibar kwa hili unatupeleka wapi?

Source: Zanzibar government defends Iranian oil tankers` registration | Mzalendo.net

Kwamba tumeshiba misaada mabayo ilipaswa ipelekwe Zanzibar hivyo tuacha waoge mafuta yao maana Zanzibar ni Nchi.
 
Ninachojiuliza hapa ni kuwa JK atajibu nini kwenye ile barua aliyoandikiwa na Marekani? maana wazenj wanasema ni sawa hata kama watapeperusha bendera za Zanzibar kwenye hizo tanker....Zanzibar bado inahesabika ni Tanzania......ihiii inakuwaje?
 
wazenj wameanza kuniudhi ngoja nichunge mdodmo wangu nisije kula BAn bureeeeeeeeeeee
 
hakuna taifa lenye haki yakuchagulia taifa jingine marafiki, raisi wetu anachopaswa kusema ni ukweli huo endapo tu hakuna agenda ya siri ndani ya urafiki huu na irani,

kama kuna maslahi binafsi yanayo hatarisha usalama wa m ataifa ya mgharibi nao watatumia sheria zao za mahusiano kuinyoosha Tanzania.

jambo linalo nishangaza ni kuwa mwenzetu Wazanzibari wanaitaja Tanganyika kama nhi inayonufaika na misaada ya marekani je wao kama sehemu ya Tanzania misaada hii haiwafikiagi? je Tanganyika ina exist bado au ndiyo hicho kinachoitwa mrima ?

..Hamad Masoud Hamad anapaswa kutimuliwa kazi kwa kuidhalilisha Zanzibar.

..kama serikali ya Zanzibar ndiyo imetoa usajili kwa meli za Iran, basi bila shaka meli hizo zinapaswa kupeperusha bendera ya Zanzibar.

..narudia waziri amekiuka sheria, na ameidhalilisha Zanzibar.
 
CCM mlichokifanya Zanzibar kwa kurekebisha KATIBA huko bila ya kuoanisha marekebisho hayo kuendana na katiba ya Muungano; huko mlikoroga sasa ni juu yenu kuinywa kwa jinsi mambo ya Iran yatakavyokua hapo baadaye kidogo.
 
..Hamad Masoud Hamad anapaswa kutimuliwa kazi kwa kuidhalilisha Zanzibar.

..kama serikali ya Zanzibar ndiyo imetoa usajili kwa meli za Iran, basi bila shaka meli hizo zinapaswa kupeperusha bendera ya Zanzibar.

..narudia waziri amekiuka sheria, na ameidhalilisha Zanzibar.

Jamani acheni waweke bendera ya Zanzibar kama inakubalika kimataifa. Kutumia ya muungano sio muafaka kabisa. Huu muungano uvunjike mapema kila nchi ijue inaelekea wapi. Ni vizuri wa Bara walioko Pemba na Unguja wakaanza kurudi Tanganyika na wa Zanzibar (Unguja na Pemba) wakaanza kurudi kwao!
 
..Hamad Masoud Hamad anapaswa kutimuliwa kazi kwa kuidhalilisha Zanzibar.

..kama serikali ya Zanzibar ndiyo imetoa usajili kwa meli za Iran, basi bila shaka meli hizo zinapaswa kupeperusha bendera ya Zanzibar.

..narudia waziri amekiuka sheria, na ameidhalilisha Zanzibar.

Mwambieni JK aondoe bendara ya Tanzania kule Zanzibar?

Hivi Tanzania ni nini? bila Zanzibar
 
CCM na Kikwete walijiingiza kichwa kichwa kulirekebisha katiba ya Zanzibar simply for political expediency licha ya kutahadharishwa na wataalam wa sheria kamaa vile Mhe Tundu Lissu; sasa ndoano ndio hiyo imeanza nchini mwetu kutokana na hizi fikra mbayuwayu.
 
Kuna bendera ya Mrima?

Amma kweli mkiishiwa na hoja mnaanza viroja, eti mwenyewe ndiyo unaona umekweeepa kutumia jina Tanzania. Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Mwambieni JK aondoe bendara ya Tanzania kule Zanzibar?

Hivi Tanzania ni nini? bila Zanzibar

Topical,

..wa-Zanzibari ndiyo wanapaswa kuondoa bendera ya Tanzania iliyoko visiwani.

..msimlaumu JK, yeye ameukuta muungano.

..kama Zanzibar haina haja ya kuomba ruhusu ya Tanganyika ili kujitoa ktk muungano.
 
Kwanini wazanzibar kutumia bendera ya Tanzania kuna shida gani? si wao ni sehemu ya Muungano

Kama Tanzania (a.k.a Tanganyika) anaona wazanzibar hawastahili kutumia bendera ya Tanzania atoe amri hiyo ile bendera tanzania isitumike tena zanzibar..

Sijaona kwanini wazanzibar wajiingeza kwenye mambo yasiyo na gharama wakitumia hawaumii..so watumie..anayeumia aje achukue bendera yake kama anaona zanzbar haistahili kuitumia
 
mapokeo ya dini ni tatizo kubwa sana zanzibar. haya ya kuita bendera ya Tanzania mrima ni kutokana serikali ya muungano ni dhaifu
 
Kwanini wazanzibar kutumia bendera ya Tanzania kuna shida gani? si wao ni sehemu ya Muungano

Kama Tanzania (a.k.a Tanganyika) anaona wazanzibar hawastahili kutumia bendera ya Tanzania atoe amri hiyo ile bendera tanzania isitumike tena zanzibar..

Sijaona kwanini wazanzibar wajiingeza kwenye mambo yasiyo na gharama wakitumia hawaumii..so watumie..anayeumia aje achukue bendera yake kama anaona zanzbar haistahili kuitumia

Topical,

..kuna bendera ya Zanzibar ambayo inapaswa kutumika ktk masuala yasiyohusu muungano.

..suala la usajili wa meli si la muungano, ndiyo maana wengine tunasisitiza itumike bendera ya Zanzibar.

..Zanzibar kutumia bendera ya Tanzania kwenye masuala yasiyohusiana na muungano ni KUDHALILISHA utaifa wa ZANZIBAR.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom