Serikali ya Venezuela yadai dhahabu yake ilohifadhiwa benki kuu ya Uingereza. Je, Tanzania nayo ina dhahabu BoE? na je, ina thamani ya kiasi gani?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,641
2,000
Serikali ya Venezuela imefungua kesi ya madai nchini Uingereza kudai kiasi cha dhahabu yake yenye thamani ya dola bilioni 1 ilohifandhiwa katika benki kuu ya Uingereza.

Kesi hiyo itakayosikilizwa kwa siku nne mjini London itahusisha pande mbili ambapo ni wawakilishi wa serikali ya Venezuela na wale wanomwakilisha bwana Juan Guaido ambae anatambulika na nchi za Uingereza na Marekani kama raisi.

Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa jumatatu wiki hii ilisikiliza madai ya wawakilishi wa serikali ya Venezuela kudai kuwa kwa kuwa Uingereza inatambua mamlaka za Venezuela ambazo zinaongozwa na raisi Maduro basi pasipo shaka yoyote benki kuu ya Uingereza maarufu kama BoE inapaswa kuachia dhahabu hiyo ambayo serikali ya nchi hiyo inataka kuitumia ili kuweza kupata fedha za kuendesha shughuli za serikali ya nchi hiyo.

Pia sehemu kubwa ya fedha hiyo inahitajika ili kuweza kuwekeza fedha katika kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19 na katika sekta ya elimu khasa kwenye kulipa mishahara walimu na watumishi wengine.

Mzozo huu ulianzia pale benki kuu ya Venezuela Banco Central de Venezuela BCV, ilipozungumza na Shirika la Umoja wa mataifa la maendeleo UNDP na ambapo ilikubaliana na shirika hilo kuwa serikali ya Venezuela inahitaji kuagiza vifaa mbalimbali vya Afya, madawa na chakula ili kukabiliana na ugonjwa wa COVID -19.

Lakini sakata hilo likakolezwa na majibizano na kauli tofauti ambapo bodi ya BCV iloundwa na Maduro kuagiza fedha hizo huku bodi iloundwa na bwana Guaido kuagiza BoE kutoidhinisha fedha hizo kufanyiwa muamala kwenda BCV.

Mwanasheria anaeiwakilisha serikali ya Venezuela bwana Nick Vineall amedai mahakamani kwamba kuna serikali moja tu inayofanya shughuli zake nchini Venezuela ambayo ni ile ya raisi alieko madarakani bwana Maduro.

Mwanasheria huyo aliendelea kusema kuwa serikali ya Uingereza inasema haikubaliani na kuwepo kwa Maduro na serikali yake lakini inaendelea kutuma balozi wake nchini humo na pia kumpokea balozi wa Venezuela London.

Bwana Veneall alisema kuitambua serikali ya nchi fulani hakuhusiani na kuikubali au kuihalalisha kuwepo kwake.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa hadi Alhamisi na hukumu yake haitawekwa wazi.

Nchi ya Venezuela pamoja na dhahabu hiyo pia ina mali zingine au Assets katika akaunti mbalimbali nje ya nchi hiyo zenye thamani kiasi cha dola bilioni tano ambazo mpaka sasa zimezuiwa kwa maagizo ya serikali ya Marekani ikiwa ni moja ya vikwazo vya kiuchumi.

Kabla ya kupata uhuru nchi nyingi zinazoendelea hazikuwa na uwezo wa kuwa na sehemu maalum za kuhifadhia mali kama dhahabu ambayo hutumika kama rehani kunapokuwa na matatizo ya uhaba wa fedha katika serikali.

Nchi nyingi zilizoendelea zikiwemo Marekani na Uingereza ambazo tayari zilikuwa pia na masoko ya mitaji ndizo zilizokuwa zikitawala soko na kuamua bei na thamani ya bidhaa mbalimbali ikiwemo dhahabu.

Hivyo nchi nyingi ikiwemo Tanzania baada ya Uhuru ziliweza kukaa chini na wakoloni ambao kabla ya kuondoka walitiliana saini makubaliano fulanifulani likiwemo suala la kuhifadhi mali zetu huko kwao.

Je, Tanzania nayo ina mali kama dhahabu na zingine kiasi gani huko Ulaya au Marekani?

Kama ni hivyo je, mali hiyo ina thamani kiasi gani?

Kama ni hivyo je, ni kwanini mali hiyo isitumke kupunguza madeni tunayodaiwa na vyombo vya fedha kama IMF na World Bank?

NB: Uchambuzi na vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo shirika la habari la Uingereza Reuters.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom