serikali ya umoja wa kitaifa ya zanzibar siielewi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

serikali ya umoja wa kitaifa ya zanzibar siielewi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dubu, Feb 20, 2012.

 1. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  1. Makamu wa kwanza wa Rais (Seif) haruhusiwi kuachiwa nchi. Rais akisafiri nchi anaachiwa makamu wa pili wa Rais, Jaji na Spika.
  2.Mawaziri wote wanatoka Chama chenye rais.
  3.Hii serikali ya kitaifa ni kwa ajili ya Ccm na Cuf tu. Vyama vingine sjui Chadema, Pona, Cck Dp nk havihusiki.
  Je hii ni serikali ya kitaifa kweli? Mimi naona cuf baada ya kuahidiwa nafasi ya juu serikalini hasa Seif aliyekuwa na nguvu Zanzibar alikubali haraka bila kujali maisha ya baadae baada yake. Hapa Cuf walikosea.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... angalia tu hako ka-mdudu SERIKALI YA UMOJA wa kitaifa inavyokitafuna KAFU huko visiwani mpa huruma tena!!!!
   
 3. Bablii

  Bablii Senior Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo maana ukaitwa DUBU....ungeuliza (ukawa mjinga) ukafahamishwa, badala ya kuonesha upumbavu wako!

  1. Nikweli makamu wa kwanza wa rais haachiwi nchi endapo raisi atakuwa hayupo, hii ni kwa sababu sera zinazotumiwa kwa mujibu wa serkali hii (inayokutia homa) ni sera za chama kilichotoa raisi, hivyo haiwezekani makamu wa kwanza wa rais akawa ndo anachukuwa nafasi ya raisi pindi akiwa hayupo! Nimakubaliano waliyokubaliana wazanzibar! Huenda leo ni zamu ya CCM kutoa rais, lakini huenda 2015 ikawa CUF, the same will apply!

  2. SIKWELI kwamba mawaziri wote wanatoka chama chenye raisi, CUF wana mawaziri karibia sawa ya wale wa CCM (wamezidi wawili tu)!
  Tena wengine wakiwa kwenye wizara nyeti, kama vile afya, katiba na sheria, Habari, mawasiliano, na viwanda na biashara!

  3. Hii serkali ya kitaifa ni kwa ajili ya vyama vyenye kutoa wajumbe wa baraza la wawalilishi (nchini zanzibar) na kwa anaeshika nafasi ya kwanza na ya pili ya urais wa nchi ya Zanzibar. Hata CHADEMA wakifanikiwa kutoa wawakilishi au kushika namba 1 au 2 katika cuhaguzi wa rais Zanzibar nayo itaingia katika Serkali ya kitaifa (mseto)!

  Question: Nyinyi wafuasi wa CHADEMA, ambao kutwa mnaidhihaki na kuilaani CUF kwa kuunda serkali ya mseto na CCM, jee CHADEMA ikifanikiwa kushika namba 2 katika kura za urasi Zanzibar na ikapata wawakilishi katika majimbo ya zanzibar, kitakataa kuunda serkali ya mseto? Kumbuka serkali hii ya mseto ipo kwa mujibu wa KATIBA ya Zanzibar! Jee nyinyi wapiga kelele hapa JF mtajitoa CHADEMA au kwa CHADEMA itakuwa sawa lakini kwa CUF ni ndoa ya mkeka? Au ndo mshajuwa haiwezi kutokea mkapata hiyo nafasi ndo maana mnaitukana hiyo serkali ya mseto?
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nimeona waziri wa afya zanzibar aibu analalamika kama si waziri bana anailalamikia serikali wakati yeye ni sehemu ya serikali.Imetoka mlimani tv
   
 5. C

  Comreed Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Ama kweli mtu anaweza kujidanganya mwenyewe alafu ule uwongo wake akadhani anaweza kudanganya watu wengine, serikali ya umoja wa kitaifa znz ingelikuwa sahihi kuita serikali ya kuwagaia uwongozi cuf wasipige kelele hebu niambie serikali gani ya umoja wa kitaifa inayotekeleza ilani ya chama hasimu yake wapi duniani? mwisho 2015 mutawambia nini wananchi wenu? chama cha cuf kinaisaidia ccm kutekeleza ilani yake 2 baada ya mawaziri na manaibu wake ni nani mwengine aliechaguliwa kutoka cuf? kuleni mtakachokipata umri wenu ndio unamalizika tena.
   
 6. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Cuf zanzibar imeisha kwa sababu wakazi wa zanzibar wanalalamika kwamba wawakilishi wao hawazungumzii matatizo yao badala yake wamekazana na mambo ya Muungano wakati wakazi wa zanzibar wakiishi maisha duni ya umasikini. hamna shule, huduma za afya za kutosha na maisha kupanda bila kupandisha mishahara.
   
Loading...