Serikali ya umoja wa kitaifa tanzania haihitajiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya umoja wa kitaifa tanzania haihitajiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BWIRU BOYS 2001, Mar 8, 2011.

 1. B

  BWIRU BOYS 2001 Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mojawapo ya maamuzi ya baraza la siasa ni kuwa kuwepo na serikali ya umoja wa kitaifa Tanzania bara ili kumaliza malumbano yaliyopo. Binafsi naona kwanza hakuna malumbano ila kilichopo vyama vya siasa kufanya shughuli zao za kila siku za kuikosoa serikali na hata kama yapo suluhisho si kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itashirikisha vyama vyenye wabunge kwani kufanya hivyo ni kuuwa upinzani na hivyo kukosa watu wa kuiwajibisha serikali, wabunge watabaki kuwa mashabiki wa mawaziri na watasahau majukumu yao. sisemi kuwa serikali za umoja wa kitaifa hazifai la, ninachosema kwa Tanzania na Afrika bado hatujafikia ukomavu wa kuweza kuunda serikali hizo na kuwaletea wananchi maaendeleo, angalia mfano wa Kenya na Zimbabwe. kwa nchi zilizoendelea hili linawezekana mfano ni UK

  Kama kweli haya maamuzi yameungwa mkono na vyama vya upinzani basi naweza kuhitimisha kuwa shida yao si kuwakomboa watanzania ila ni kuingia serikalini ili nao watembelee STK na mishahara minono.
   
Loading...