Serikali ya umoja ni umbumbumbu wa demokrasia na Uchu wa madaraka!!

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
381
225
Inasikitisha kuona viongozi wengi wa vyama vya upinzani Afrika wanaamua kuungana na viongozi wa vyama tawala katika nchi mbalimbali Afrika eti kwa kisingizio cha kudumisha amani.
Lengo la chama chochote cha siasa ni kuona siku moja kinashika dola. Viongozi wanaokuwa madarakani pindi wanaposhindwa katika chaguzi hukataa kuachia madaraka haya. Na kwa kuwa wapinzani walioshinda huwa wanapenda madaraka sana, basi hukubali kuunda serikali wanazoita za umoja. Tujiulize, umoja huo huja vipi na vyama ambavyo huwa na sera tofauti?
Waafrika tujifunze demokrasia ya kweli ya kushindanisha sera na pindi upande mmoja unaposhindwa, ukubali matokeo na upande wa pili ushike dola kama vile wenzetu Wamarekani wanavyofanya.
Napo hapa Tanzania tumeshaanza kujidanganya eti mtindo huo ni demokrasia. Hii si demokrasia hata kidogo.
Tukomae kidemokrasia. Twende majukwani, tunadi sera zetu na wananchi wakishasema, wawe wamesema maana ndo wenye mamlaka ya kuweka viongozi wanaowataka. Leo hii Tanzania inataka kupoteza dira ya upinzani kabisa eti kwa kisingizio cha serikali ya umoja. Wajanja wenzenu wanachofanya wakiona wameshindwa wananga'ang'ania ili angalau wabaki kwenye serikali ya umoja.
Sisi tujenge demokrasia ya kweli ambayo maamuzi ya wananchi ndo unakuwa msingi wa wa utekelenzaji wa yale tunayoahidi kuzingatia wakati wa uendeshaji wa nchi. Kwa kweli serikali ya umoja ni bango linaloonesha kuwa viongozi wetu si wale tuliowaamini katika masuala tuliyowatuma kufanya. Inaonesha kuwa ubinafsi ndo unatawala na ndio maana viongozi wetu wa vyama vya upinzani wakiambiwa watapewa madaraka tayari wanageuka na kuwa wasaliti wakubwa wa wananchi wao!
Tuwaulize hao walio kwenye serikali ya umoja, je, wanawezaje kutekeleza sera zao mbadala wakati wamemezwa kwisha kabisa na sasa hatuoni wakiongea lolote kuhusa vyama vyao ila kumsifia bwana mkubwa aliyekubali kuwapa madaraka kidogo angalau ya kulindwa na kuwa na misafara ya magari angalau kumi? Nyie viongozi tuliowaamini tafadhalini sana msitusaliti sisi wafuasi wenu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom