Serikali ya UKAWA itanyang'anya watumishi waliouziwa nyumba za serikali?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
Tofauti na ilivyokuwa katika kampeni za miaka ya nyuma ambapo ajenda hii ilibebwa sana na vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, sasa hivi vyama hivi havilizungumzii kabisa suala hili.

Je, sababu yake ni nini? Inajulikana kati ya waliofaidika na mpango huo wa serikali ya awamu ya tatu ni pamoja na waheshimiwa Sumaye, Kingunge, Magufuli na Lowasa.
 
Samahani kama hili swali limekuwa gumu. Nilichotaka kujua tu kutoka kwa wana UKAWA au wana CCM kama mmoja wenu atashinda kutinga Ikulu, jee mtatunyang'anya hizo nyumba za serikali tulizouziwa kwa upendeleo sisi watumishi wa umma na serikali ya awamu ya tatu chini ya Mzee William Benjamini Mkapa? Jibu la suala hili litatusaidia kutoa maamuzi yetu pale tarehe 25 Oct. Ninaamini hii ni haki yetu kujua.
 
haitekelezeki........... la sivyo itachukua miaka kumi kuhangaikia kesi tu
 
Mbona ni vingi sana vya kurudisha? Kuanzia viwanja vya mipira, majengo, viwanja vya wazi, nyumba za serikali na mali nyingine nyingi.
 
Samahani kama hili swali limekuwa gumu. Nilichotaka kujua tu kutoka kwa wana UKAWA au wana CCM kama mmoja wenu atashinda kutinga Ikulu, jee mtatunyang'anya hizo nyumba za serikali tulizouziwa kwa upendeleo sisi watumishi wa umma na serikali ya awamu ya tatu chini ya Mzee William Benjamini Mkapa? Jibu la suala hili litatusaidia kutoa maamuzi yetu pale tarehe 25 Oct. Ninaamini hii ni haki yetu kujua.

Serikali hiyo hiyo Iandae na mabilioni ya kuwalipa waliozinunua na kuzifanyia matengenezo. Kupanga ni kuchagua. Kazi kwetu.
 
Lakini na wote waliojenga nyumba zao kinyume na ramani ya mipango miji nao nyumba zao zibomolewe kama kulipwa walipwe. Hapo hakuna shida kwani ni pesa kwa pesa na watanzania kwa watanzania.
 
Watarudisha wawili SUNDI mzazi mwenzangu na MUSSA mdogo wake na push up pia kampuni ya ANBEN.Hao watatu na watoto wao lazima wazirudishe nyumba za serikali.Lakini pia serikali ya UKAWA itaunda utaratibu wa kisheria namna nzuri ambapo kama kuna ulazima mfanyakazi anayelipa kodi anaweza kuuziwa nyumba za serikali.Lowassa ana mambo mazuri kwa wafanyakazi wote hana JAZIBA,ROHO nyeupe,HATALIPIZA visasi,RAFIKI wa BODABODA,MAMA/BABA LISHE NA PIA WAFANYAKAZI WOTE
 
Back
Top Bottom