MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,408
Habari za hivi punde,
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imekanusha usemi ambao unadai kwamba wao walisema ile sumu ya Novichok imetokea nchini Urusi. Hili limekuja baada ya Wanasayansi wa jeshi nchini Uingereza kudai kwamba wamepima na hawajui ile sumu imetokea nchi gani tofauti kabisa na ambavyo Serikali kupitia Wizara yake ya mambo ya nje imedai.
Sambamba na hilo,
Wizara ya Mambo ya nje inasema imefuta kabisa ile Tweet ambayo ilikuwa inadai kwamba Urusi wamehusika na hili jambo. Pia Warusi wamesema kwamba Organization Against Chemical Weapons (OACW) inabidi iwahusishe Warusi katika huo uchunguzi wao ili kuzuia Uingereza kuharibu na ushahidi.
MASWALI:
1. Kwanini Serikali ya Uingereza inajikanyaga katika hili ???
2. Hivi hata kule Syria Assad alitumia silaha za sumu kweli au nako walikurupuka tu ???
3. Je, tunatakiwa tuwaamini hawa watu na vyombo vyao vya habari wakati wana ndimi mbili ??
4. Je, kwanini walikuwa radhi kuhatarisha Usalama wa dunia kwa madai yasiyo na ushahidi ???
5. Nchi ndogo za Afrika ambazo hazina vyombo vikubwa vya habari tutakuwa tumesingiziwa mangapi kwa tabia hii ya kukurupuka ???
CHANZO:UK Foreign Office denies claiming nerve agent from Russia, despite tweet and Boris Johnson interview
====================================
UPDATES:
Imefahamika na wataalamu kwamba sumu ya Novichok inaweza kutengenezwa na mataifa zaidi ya Ishirini hapa duniani.
NB: Raisi wa Urusi V.Putin kasema haitaji Urusi iombwe msamaha kuhusiana na kuchafuliwa kwa Urusi katika hii skandali, bali akili ya kawaida (Common Sense itumike)
Chanzo: We don’t want apologies, we want common sense to triumph – Putin on Skripal saga
========================================
UPDATES:
Urusi imeitisha kikao cha dharura cha Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Matifa ili kuzungumzia suala la jaribio la mauji ya Skripal na bintiye. Balozi wa kudumu wa Urusi kamwandikia Raisi wa Baraza hili kwamba matumizi hayo ya kemikali za sumu hayakubaliki popote pale duniani.
Chanzo:Russia calls for UN Security Council meeting over Skripal affair
CC: TUJITEGEMEE , Palantir , zitto junior , weed , BlackPanther, Red Giant, Victor wa happy