Serikali ya Uholanzi imeidhinisha mipango ya kuruhusu kifo cha mapema au mauaji ya huruma kwa watoto wenye ugonjwa usiopona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Serikali ya Uholanzi imeidhinisha mipango ya kuruhusu kifo cha mapema au mauaji ya huruma kwa watoto wenye ugonjwa usiopona kati ya mwaka 1 na miaka 12.

Jumanne, Waziri wa Afya Hugo de Jonge amesema mabadiliko ya sheria hiyo yatazuia baadhi ya watoto "wasiteseke tu kwa machungu wanayopitia".

Sasa hivi mauaji ya huruma yanaruhusiwa nchini Uholanzi kwa watoto wenye umri wa zaidi ya miaka 12 kwa sharti la idhini ya mgonjwa na wazazi wake. Aidha, utekelezaji wa kifo cha mapema kunaruhusiwa kwa mtoto wa hadi mwaka mmoja kwa idhini ya mzazi.

Lakini mauaji ya aina hiyo hayajaelezwa kisheria kwa watoto kati umri wa mwaka mmoja hadi miaka 12 kwa wanaougua ugonjwa usio na tiba. Suala hilo tata limezua mjadala mkali kwa miezi kadhaa katika muungano wa vyama tawala vinne vinavyounda serikali.

Pia hatua hiyo imepata upinzani kutoka kwa vyama vya wakristo wenye msimamo mkali.

Lakini kufuatia idhinisho kutoka kwa serikali kuhusu mpango huo, Bwana de Jonge alisema atatayarisha kanuni mpya kwa ajili ya kitendo hicho. Alisema utafiti uliofanywa na wataalamu ulionesha umuhimu wa kubadilishwa kwa sheria hiyo.

"Utafiti ulionesha kuna umuhimu wa maisha kukatizwa miongoni mwa madaktari na wazazi wa watoto wanaougua magonjwa yasio na tiba, ambao wanapata tabu bila usaidizi wowote na hatimaye watakufa tu siku zijazo," Bwana de Jonge alisema katika barua aliyoiwasilisha bungeni.

Aliongeza kwamba utafiti huo unaonesha karibu watoto watano hadi 10 kwa mwaka wataathirika kwa sheria hiyo iliyobadilishwa.

Sheria za sasa hazitabadilishwa lakini madaktari hawatashtakiwa kwa kutekeleza mauaji ya huruma kwa mtu ambaye umri wake ni kati ya kundi lililotajwa.

Kwa watoto wenye umri wa zaidi ya miaka 12, idhinisho kutoka kwa wazazi itakuwa ni lazima kulingana na sheria iliyopendezwa kubadilishwa.

Wagonjwa pia watahitajika kuthibitishwa kuwa wanapitia machungu na tabu kweli zisizojulikana mwisho wake na angalau madaktari wawili wanastahili kukubali kutekelezwa kwa mchakato huo wa kutekelezwa kwa kifo cha mapema.

Mabadiliko ya sheria yanatarajiwa kutekelezwa miezi michache ijayo.

Utekelezaji wa kifo cha mapema na kusaidia kumtoa mtu uhai kumeruhusiwa nchini Uholanzi tangu 2002, na nchi jirani ya Ubelgiji ikafuata mkondo.

Nchi hizo mbili ndio zilikuwa za kwanza kuhalalisha vifo vya aina hiyo licha ya masharti makali.

Mwaka 2014, Ubelgiji ilikuwa nchi ya kwanza kuruhusu mauaji ya kukusudia kwa watoto watakaotaka kufanyiwa mchakato huo ikiwa wanaugua ugonjwa usiotibika na wanapitia machungu yasiokifani, iwapo wazazi wao watatoa idhini.

Na muda mfupi baadae, Uholanzi ilianzisha sheria hiyo hiyo kwa watoto zaidi ya miaka 12.
 
Huo ni ujinga wa kiwango cha mwisho.

Kudhania kwamba siku moja mgonjwa atakufa, hivi ni nani ambaye hatakufa? Na je vipi wale wanaokufa ghafla?na wale wa ajali je?
Hii mizungu ni bure kabisa.

Mabeberuuuuuu zao
 
Back
Top Bottom