Serikali ya tz na kisa cha mfalme agmemnon wa ugiriki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya tz na kisa cha mfalme agmemnon wa ugiriki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by silent lion, Jul 10, 2012.

 1. s

  silent lion JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 537
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Wadau kwanza kabisa napenda kushukuru Serikali yetu kwa kuruhusu freedom of speech.

  Kuna kisa kimoja, kwa wale wapenzi wa Movies kuna mchezo unaitwa TROY nyota wake akiwa ni Brad Pitt. Sasa katika mchezo huu kuna mfalme niliyemtaja hapo juu. Huyu mfalme alikua tamaa sana.

  Wakati mmoja ilibidi aivamie Troy. Kwa bahati nzuri wakafanikiwa kuiteka kirahisi pwani ya Troy. Sasa jeshi la Ugiriki likaona litachukua kirahisi nchi yote.

  Sasa wakati vita vimepamba moto, majeshi ya ugiriki yakawa yamezidiwa sana na yanakaribia kushindwa. Kamanda wa ugiriki Odysey akamwambia mfalme;
  Odysesy: you must pull back the army.
  Mfalme; my army has not lost the battle yet.
  Odysey; You wont have an army if u dont pull back

  Yaani Odysey alijua kama vita vigumu na wakiendelea kwenda mbele wanaweza kushindwa lakini Mfalme bado anang'ang'ania kwenda mbele. Mwishowe Mfalme akakubali kusalimu amri na ikawa ndio salama yao, kwani walikwenda kujipanga upya na kurekebisha makosa

  Sasa wadau kama mnavyojua TRA imepandisha ushuru wa magari bila ya kujali hali za watz huku mabilioni yakiendelea kutafunwa na mafisadi. Magari kama ya abiria na mizigo hivi sasa nayo yatalazimika kulipiwa uchakavu tofauti na hapo awali. Mwishowe ni watu wachache tu ndio watakaoweza kuleta magari kwa hali hii, hivyo na Serikali itakuwa haikufanya jambo lolote kwani walitakiwa kupull back na sio kuwakamua wananchi kila kukicha. Kwani walilazimishwa kuwa madarakani?
   
Loading...